Matunda ya chanjo yaanza kuonekana, kazi nzuri ya Rais Samia

Hapo jana, Serikali ya Uingereza kupitia ubalozi wake hapa nchini ulieleza kuwa Tanzania ni miongoni mwa mataifa yaliyoondolewa katika orodha ya Mataifa hatari kwa maambukizi ya Corona ambapo mataifa katika orodha hiyo yamepungua kutoka nchi 54 hadi 7. Kwa mujibu wa taarifa hiyo mabadiliko hayo yataanza Jumatatu (Oktoba 11, 2021)

Kwa hatu hiyo ina maana kwamba sasa Watanzania, Raia wa Uingereza na wasafiri wote kutoka Tanzania hawatakaa tena Karantini ya lazima wafikapo nchini Uingereza ikiwa tu watakuwa wamepata moja kati ya chanjo nne ambazo zinatambuliwa na Uingereza.

JAMBO HILI LINA TIJA GANI KWA TANZANIA.

Ni wazi kuwa, jitihada kubwa za Serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Samia Suluhu kuhakikisha taarifa, elimu na huduma ya utoaji chanjo na elimu dhidi ya UVIKO-19 inatolewa kwa Watanzania wote kwa hiari kumesaidia sana hatua iliyofikiwa sasa.

Utoaji wa chanjo ya UVIKO-19 ni moja kati mambo mkuu yaliyopelekea Tanzania kuondolewa katika "Red list".
Na, kwa hatua hiyo sasa ni wazi kuwa ajira za wadau na washirika wengi wa sekta ya utalii zitarejea.
Watalii kutoka Uingereza wataanza kumiminika kutembelea vivutio mbalimbali nchini.
Wote walioko kwenye mnyororo mzima wa thamani kuanzia wasafirishaji, wahudumu wa hoteli, watoa huduma za chakula n.k watanufaika na hili linaenda kupunguza ukali wa maisha kwa kiasi fulani.

View attachment 1967898

View attachment 1967899
Subiri uteuzi
 
Wakati mnakwenda airport kupokea ndege hamkujiona kama ni mataahira?

Umemuona leo mama kuzuzuka na upumbavu kama huo?

Tulieni dawa iwaingie wajane na mayatima wa chizi wa chattle.
Yeye Mama kaamua kuwaanyoosha Magaidi hapa Nchini, Mwendazake alikua anawachekea chekea sana! Mbowe kwisha habari yake!!
 
Imekaa vizuri...cheti chango Cha chanjo ya J&J Vaccine bila shaka kitaniruhusu. Hongera Sana kwa Madame President Samia kwa uongozi bora
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom