Matumizi zaidi ya shampoo zaidi ya yale ya kuoshea nywele tuu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,481
9,242
Sabuni ya maji
Shampoo hutumika vizuri kama sabuni ya mikono, na ni rahisi kuliko sabuni ya kununua.
Tia robo shampoo kwenye kifungashio changanya na maji, tikisa ichanganyike vizuri.



Shaving Cream
Punguza kununua shaving cream katika list ya matumizi yako.Tumia shampoo na inafanya vizuri, na haiachi uchafu wa madoa ya kutu katika bafuni au tub yako.

Tip: Changanya shampoo na conditioner pamoja au tumia zote kwa pamoja huifanya ngozi kuwa laini na nyororo.




Sabuni ya kuogea
Save hela na punguza namba za chupa za sabuni ya kuogea bafuni kwako kwa kutumia shampoo mwilini kwako. Hulainisha ngozi na hukuacha na manukato mazuri mwilini.

Tia shampoo kwenye maji ya kuogea kupata mapovu wakati wa kuoga
Changanya chumvi au sukari kwa shampoo tumia kama scrub ya mwilini





Kufulia nguo
Sahau kununua sabuni ya kufulia.Nyunyiza shampoo kwenye beseni au sink la kufulia lenye maji, inatumika kwa nguo za ndani, sweta, na aina ya nguo za kawaida.
Fua kwa mkono.



Kuondoa madoa
Nyunyizia shampoo kwenye doa la nguo. Haswa aina ya mafuta, na madoa ya damu.
Tia shampoo kwenye doa iache kwa muda kidogo, fikicha, suuza vizuri.
Rudia ikilazimika.



Madoa ya carpet
Huondoa madoa kwenye carpet , sofa, kochi.
Tia shampoo ni rhisi sugua na kitambaa au sponji mpaka pawe safi.
Muhimu: Ondoa madoa kwenye carpet na sofa au kochi mara tu lichafukapo.

Tip
: ondoa wasiwasi wa kuvujia rangi kwa kujaribu eneo lingine kwanza.



Jikoni
Tumia shampoo kuondoa mafuta jikoni yaliyogandia kwenye counters,ukutani,stove,na vifaa vilivyopo.Tia shampoo kidogo kwenye kitambaa cha unyevu nyevu.Safisha sehemu chafu,iache kwa muda kidogo.
Suuza mpaka pawe safi.
Tip: Changanya shampoo na baking soda huondoa uchafu haraka zaidi.

Sakafu(Floor) na Bafuni (Bathroom)
Changanya shampoo kidogo na maji ya uvuguvugu .Hung’arisha vizuri tiles, aina ya tarazo, na harufu nzuri.
Tumia kusafishia tub au shower kwa kutumia kitambaa, utapunguza muda wa kusugua.
Iache kwa muda kidogo, suuza na safisha vizuri.
Utastaajabu uchafu wote umesafishika na pameng’aa.


Shampoo imetengenezwa kukata au kusafisha mafuta kirahisi na kukuza nywele, inafanya vizuri katika kufyonza mafuta kama sabuni. Spray ya nywele imegandia kwenye ukuta wa bafuni kwako?shampoo pia huondoa uchafu huo.


Chanzo; cleansakamia
 
Asante kuanzia leo watajuta home yaani kila kitu nitawaambia tumieni shampoo!
 
it's not cheap also hasa kwa sisi wenye familia kubwa na ustaarabu F utanunua kila siku watumie otherwise uwe na familia ndogo na inayoelewa matumizi,
 

Similar Discussions

6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom