Matumizi ya -to- au -ta- kwenye Kiswahili (mfano sitasahau/sitosahau)

Kama kichwa cha uzi kinavyoeleza hapo juu, ninahitaji kujua matumizi hasa ya -to- na -ta- . Je ni sahihi kutumia maneno mfano "Kama hutojali" badala ya "Kama hutajali" au "Sitosahau" badala ya "Sitasahau", Kama ni sahihi, je yanatumika vipi na wakati gani?
Hayo ni mambo ya lugha ambayo hayana makosa ndani yske ni sahihi tu zote kutumia.

Ni kama neno "HAVE"
husomeka "hav" na husomeka pia "hev"

Zote sahihi na zinaeleweka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo ni mambo ya lugha ambayo hayana makosa ndani yske ni sahihi tu zote kutumia.

Ni kama neno "HAVE"
husomeka "hav" na husomeka pia "hev"

Zote sahihi na zinaeleweka.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uandishi na utamshi wa neno "sitofahamu" ni tofauti na uandishi na utamshi wa "sitafahamu", lakini kwa matamshi "hav" na "hev" yote yana uandishi mmoja tu "have" tofauti na hapo ni makosa. Lengo langu ni kujua kiswahili sanifu kinatambua neno gani kuwa sahihi kati ya linalotumia -to- au -ta-?, na kama yote ni sahihi, ni wakati gani wa kutumia lipi?
 
Kwa kuwa yote ni kanushi
Yote yanadokeza njeo ileile
Basi utokeaji uamuliwe na upatanisho kisarufi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kuwa yote ni kanushi
Yote yanadokeza njeo ileile
Basi utokeaji uamuliwe na upatanisho kisarufi

Sent using Jamii Forums mobile app
Chief Editor Asante kwa maelezo, ila sijakupata vizuri kwenye hyo upatanishi wa kisarufi kama unaweza kunielewesha vizuri kwa sentensi mifano ya huo upatanishi ambao utaamua matumizi hasa hapa kwenye -to- kwa sababu sina uhakika sana na matumizi yake. Je, ni wakati gani matumizi ya -to- yanakuwa sahihi zaidi kuliko -ta- katika sentensi. Pia kama unaweza kuniambia blogu/website/kamusi/kitabu cha kiswahili kinachoelezea matumizi na tofauti ya hivi vitu viwili utakuwa umenisaidia sana
 
Mimi naamini Lugha za asili ndizo zilizoyumbisha kauli hii ila usahihi zaidi ni -ta- na siyo -to-

Sent using Jamii Forums mobile app
🤝Naunga mkono hoja mia fili mia kisa na maana kwamba, viambishi hivyo vyapaswa kutokea nafasi ya NJEO na katika lugha aali ya Kiswahili tuna njeo za wakati uliopita /li/, wakati uliopo Hali timilifu /me/, wakati uliopo/na/ na wakati ujao /ta/. Sasa hiyo -to- ipo katika wakati gani?

Huu ndio mtazamo wangu, ruksa kukosolewa.
 
Mimi naamini Lugha za asili ndizo zilizoyumbisha kauli hii ila usahihi zaidi ni -ta- na siyo -to-

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi pia naunga mkono kuwa kiambishi sahihi cha wakati ujao ni -ta-, nadhani watu wanaotumia kiambishi -to- wanajaribu kuelezea wakati ujao katika hali ya kuendelea , kwa mfano ; sitokusahau katika maisha yangu ( kuanzia muda huu ninao ongea na kuendelea ).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom