matumizi ya teknoligia kwenye usafirishaji wa mitihani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

matumizi ya teknoligia kwenye usafirishaji wa mitihani

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by nrashu, Sep 18, 2012.

 1. n

  nrashu Senior Member

  #1
  Sep 18, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wanabodi,
  Natumaini hamjambo na kila mmoja anaendelea na ujenzi wa Taifa letu la Tanzania. Leo hapa Mwanza kuna jambo limenishangaza sana. Nimekutana na Gari la polisi likisindikiza gari la idara ya Elimu. Nilipofuatilia zaidi nikajulishwa lilikuwa limebeba mitihani ya darasa la saba kutoka Mwanza airport. mitihani imetoka Dar es salaam.

  Na katika hiyo mitihani kulikuwa na mitihani ya kanda mbalimbali ikiwemo tabora, mara, bukoba na mikoa mingine.
  Ninachopenda tujadili hapa ni kujua kama bado ni muhimu kusafirisha mitihani kwenye hard copy.

  Bila Jazba kwa wale wasiopenda uongozi wa baraza la mitihani, je sio wakati muafaka wa technologia kutumika kusafirisha hata flush disk, au kuprint kwenye wilaya husika? gharama za usafiri nilizoziona hapa ni kubwa sana. Pia wasindikizaji zaidi ya kumi pamoja na polisi. Je huu mfumo wa hard copy hauongezi risk ya mtihani kuvuja?
  Au ndio mfumo wa kuhakikisha perdiem zinaliwa kipindi hichi?

  Kwa mawazo yangu wakati umefika wa kuhakikisha technologia inatusaidia kupunguza gharama na kuepusha mitihani kuvuja. Naomba Dada Dr ndalichako apokee hii changamoto.

  Naomba kuwakilisha kwa majadiliano.
   
 2. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Ni mawazo mazuri endapo miundombine ya nchi hii ingeruhusu hilo unalolisema. Utakubaliana na mimi sio kila aina ya printa ya ofisi inayoweza kufanya kazi ya kuchapa mitihani hiyo. Hasa kwa mwaka huu kwani mitihani hii itakayosahihishwa kwa kutumia teknolojia ya OMR.

  Labda kwa sasa tuzungumzie uwepo wa miundombinu msingi kwa kanda (zonal) na katika muendelezo huo hapo baadae kila wilaya iwe na uwezo huo. Lakini hapohapo tusisahau kujadili swala la uaminifu, tumezoea kusikia kuhusu wizi/udanganyifu wa mitihani. Wizi ambao unafanywa kwa ushirikiano na wahusika wakuu kabisa wa mitihani yenyewe. Tunapaswa kujiuliza kama tumefikaia mahali ambapo tunaweza kuwaamini watendaji wa idara za elimu katika wilaya na kuwapa jukumu hili kubwa pasi na shaka kwamba hapatakuwa na udanganyifu wa aina yeyote.

  Naunga mkono hoja!
   
 3. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hoja zingine bwana
   
 4. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,629
  Likes Received: 9,842
  Trophy Points: 280
  suala la mitandao tanzania ni shida sana...technology bado iko poor na nina wasiwasi na mifumo hii kama itatumika kusafirisha mitihani kwani hackers seems ni wengi sana na wanawazidi hawa jamaa ujanja kila kukicha
   
 5. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,739
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Bora waendelee kusafirisha mitihani katika makaratasi. Usalama wa teknolojia, umahiri katika matumizi ta teknolojia, uaminifu, teknolojia ya usahihisaji n.k haviruhusu kusafirirshaa taarifa zikiwa katika soft copy.
   
 6. Njunwa Wamavoko

  Njunwa Wamavoko JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2012
  Joined: Aug 11, 2012
  Messages: 5,577
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  kingvix umerudi?niliku-miss!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Mjanga

  Mjanga JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 1,246
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  kimsingi hoja ni nzuri lakini mazingira hayajaruhusu! tatizo kubwa ni uaminifu ndani ya jamii nzima,
  kuanzia wazazi, watendaji, mifumo, na hackers wanaopenda kupata maisha kwa short cutz!
   
 8. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #8
  Sep 19, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Ukitaka mitihani hiyo ivuje as if maji yamewekwa kwenye gunia basi sambaza kwa soft copy...Hata |JF itawekwa...unaijua bongo wewe?

  Dont try it at home
   
 9. S

  Sine r Winters Senior Member

  #9
  Sep 19, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  wana hiyo njia ni hatari coz wa2 c waaminifu na wale wazeiya wa kuvujisha hadi mock,hiyo hawatoiacha.
   
 10. mtumishidc

  mtumishidc JF-Expert Member

  #10
  Sep 19, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 489
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  tatizo teknologia taifa hili imeiva upande mmoja wa nchi na upande mwingine wa nchi hata kupandwa haijapandwa, mfano si mikoa yote yenye maeneo ya kudurufia nakala kwa wingi kiasi cha kukidhi hitaji lakini pia usalama wa maeneo hayo si wa uhakika hata kama yakiwepo!
   
Loading...