Matumizi ya stempu za karatasi mwisho Aprili 30

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
1074265


MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) imepiga marufuku matumizi ya stempu za karatasi kwa bidhaa zote za sigara, pombe kali, mvinyo, bia na aina zote za vileo zenye stempu zisizo za kielektroniki na zile zisizo za stempu kabisa, i kapo Aprili 30, mwaka huu.

TS)Juni mwaka jana serikali kupitia TRA ilianzisha mfumo wa Stempu za Kodi za Kielektroniki (E kwa bidhaa zinazostahili kutozwa ushuru wa bidhaa badala ya stempu za karatasi za kubandika ambapo mfumo huo mpya ulianza kutumika rasmi Januari 15, mwaka huu.

Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere alisema Dar es Salaam jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa mfumo wa stempu za kodi za ETS kwa bidhaa zinazotozwa ushuru wa bidhaa.

Kichere alisema kutokana na changamoto za mfumo wa stempu za kodi za karatasi, serikali iliamua kuanzisha mfumo wa stempu za kodi za kielektroniki mfumo ambao unaendeshwa kwa ushirikiano wa TRA na kampuni ya SICPA SA yenye makao makuu yake nchini Uswisi.

Alisema kampuni hiyo ndiyo ilifunga mfumo kama huo katika nchi za Kenya, Morocco, Malaysia, Brazil, Albania, Uturuki na sasa Uganda. Alisema mfumo huo unatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza inahusisha bidhaa za sigara, mvinyo, pombe kali, bia na aina zote za vileo wakati awamu ya pili ikihusisha bidhaa za vinywaji baridi, maji, juisi, CD na DVDs.

“Kwa sasa tunatekeleza awamu ya kwanza ambapo wazalishaji na waingizaji wa bidhaa nchini kwa awamu hii ya kwanza walianza rasmi matumizi ya mfumo huu tangu tarehe 15 Januari, 2019,” alisema. Alisema hadi sasa jumla ya mitambo 44 katika viwanda 23 vya bidhaa za awamu ya kwanza imefungwa katika viwanda hivyo na inafanya kazi vizuri.

Alitaja viwanda vilivyofungwa mitambo hiyo kuwa ni viwanda vyote vine vya sigara nchini, viwanda vyote saba vya bia nchini na viwanda vya mvinyo na pombe kali 12. Vile vile alisema waingizaji wa bidhaa nchini wapatao 14 wameshajiunga na mfumo huo na wanautumia vizuri, huko wengine wakiendelea kujiunga.

Alisema kwa upande wa ufungwaji wa mfumo huo kwa viwanda vya bidhaa za awamu ya pili umekwishaanza na hadi sasa mitambo 45 katika viwanda 19 vya vinywaji baridi imefungwa na tarehe rasmi ya kuanza kutumika mfumo huo kwa bidhaa za vinywaji baridi ni Mei mosi, mwaka huu.
 
Back
Top Bottom