Matumizi ya Sh10, 000 kwenye familia yamtoa mume utumbo

Johnny Sins

JF-Expert Member
Nov 4, 2019
2,538
3,826
Benedictor Gogogo (48) mkazi wa kijiji Cha Itabagumba Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza nchini Tanzania amenusurika kifo kwa kuchanwa tumbo na kitu chenye ncha kali hadi utumbo kutoka nje baada ya kutokea ugomvi kati yake na mke wake.

Akizungumza na Mwananchi kwa simu leo Alhamisi Januari 2, 2020, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Jumanne Murilo amesema tukio hilo lilitokea jana Jumatano.

“Tunamshikilia mtuhumiwa kwa mahojiano na uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo,” amesema Kamanda Muliro
Akisimulia tukio hilo akiwa katika wodi ya Hospitalini ya Wilaya ya Sengerema anakopata matibabu, Gogogo amesema mzozo kati yake na mke wake aliyemtaja kwa jina la Mama Asteria ulitokana na kuhoji matumizi ya Sh10,000 aliyoacha nyumbani asubuhi ya siku ya tukio.

“Wakati naondoka kwenda kwenye shughuli zangu za uvuvi, asubuhi ya siku ya tukio, niliacha Sh10,000 ya matumizi. Niliporejea nilimwomba mama Asteria anipe Sh1,000 kati ya fedha nilizoacha ili ninunulie vocha ya simu lakini akaniambia fedha yote imeshatumika,” amesema
“Nilipohoji zaidi akaanza kunitolea majibu yaliyonikasirisha na kunifanya nimpige kofi na kutokea mzozo kati yetu ambao hata hivyo uliisha na mimi kuingia ndani kujipumzisha.”

Anasema akiwa ameanza kupitiwa usingizi, mke wake ambaye wameishi mwaka mmoja na nusu sasa alimvizia na kumchana na kitu chenye ncha kali tumboni hadi utumbo kutoka nje.

Anawashukuru majirani kwa kujitokeza kumsaidia kwa kukodisha mtumbwi na kumkimbiza hospitalini anakoendelea kutibiwa.

Mganga mkuu wa Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema, Sista Mery Jose amesema hali ya mgonjwa huyo inaendelea vema na bado wamemweka chini ya uangalizi wa karibu kitabibu.




Gazeti la Mwananchi


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wamama wa Kisukuma wameanza mwaka kwa style yake,mmoja kakata uume wa mmewe,mwingine kamtoa utumbo mmewe,kanda ya ziwa kulikoni?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio kweli hao watakuwa wanawake wa kutoka nchi jirani za: Rwanda au Burundi wanawake wa kisukuma hawana hasira za hivyo na tabia hizo za matumizi ya silaha hasa visu
 
Back
Top Bottom