Matumizi ya "price index" kupima mfumuko wa bei nchini yanapotosha ukweli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matumizi ya "price index" kupima mfumuko wa bei nchini yanapotosha ukweli

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Byendangwero, Apr 4, 2011.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ni jambo la kawaida kwa viongozi wa serikali kupima hali ngumu inayowakabili wananchi wake kwa kigezo cha "price index". Wakati mwingine, viongozi hao wanazunguka huko vijijini wakinukuu takwimu hizo za "price index" katika kuonyesha ya kuwa serikali yao imefanikiwa kudhibiti mfumuko wa bei. Mara nyingi wananchi hao huwa wanawashangaa viongozi wao, kwakuwa hizo takwimu wanazozinakili zinakuwa ni tofauti sana na hali halisi. Pengine ni vema tukajiuliza mkanganyiko huo unatokana na nini? Mkanganyiko huo unatokana hasa na kutumia mfumo uliopitwa na wakati katika kukokotoa hiyo "price index". Aina budi ieleweke ya kuwa katika mfumo wa sasa, Chakula upewa uzito wa zaidi ya asilimia 60 katika hesabu za ukokotoaji wa hiyo "price index". Inafanyika hivyo kwa imani kwamba Mtanzania wa kawaida anatumia zaidi ya asilimia ya pato lake kwa chakula. Wakati hiyo inaweza ikawa kweli kwa wakazi wa mijini kwa wakazi wa vijijini hiyo siyo kweli. Wakazi hao ni "subsistance farmers" hivyo kwa kiwango kikubwa wanajitosheleza kwa chakula. Pato kidogo wanalopata kutokana na shughuli zao nyingine, linatumika kukidhi matumizi mengine mbali na chakula. Katika miaka ya karibuni pato lao hilo limeahiriwa sana na kupanda mara kwa mara kwa bei ya mahitaji yao muimu kama sabuni, mafuta ya taa, matibabu, elimu ya wototo wao n.k
   
Loading...