Matumizi ya Picha za Wanyama Katika Fedha za Tanzania

Nkamu

JF-Expert Member
Dec 14, 2007
223
84
Amani kwenu wanajamvi!

Nimekuwa nikitafakari muda mrefu kuhusu matumizi ya picha za wanyama katika fedha (noti) zetu Tanzania, na sijapata jibu hadi sasa. Nimeangalia katika noti za nchi kadhaa za kiafrika na hata Ulaya na Marekani kote huko sijaona matumizi ya vitu au wanyama kuwa kama picha ya fedha zao. Zaidi sana nimeona wengi wanatumia picha za waasisi wa mataifa hayo au viongozi waliopo madarakani au wale waliofanya jambo kubwa katika historia ya taifa husika.

Sasa mimi nikaanza kutafakari kuhusu nchi yetu inavyokwenda kama vile haina mwenyewe katika kila nyanja, tukianza na fedha yetu kushuka kila iitwapo leo na mengineyo dhidi ya matumizi ya picha za wanyama katika fedha zetu. Nikafikiria kwamba, inawezekana nchi yetu mambo yanaenda kombo sababu tunaongozwa na Tembo, Simba na Twiga!! Maana picha ya kwenye noti ina uhusioano na mamlaka inayoifanya ile sarafu ifanyekazi.

Sasa ndugu zangu watanzania hebu tulijadili hili suala na tuone kama ni sawa au si sawa. Kama si sawa tufanye nini?

Karibuni!
 
Watanzania, ina maana hakuna mwenye mchango katika hili jambo sababu sijataja CCM au CDM?
 
Italy ama uingereza wataweka pichaya mnyama gani wakati hata nzi na mbu hawana?
 
Mimi nafikiri tulipaswa kuweka kitu ambacho kinaitofautisha Tanzania na nchi nyingine na si kuweka vitu tulivyo navyo. Kama ni simba, tembo, twiga na wengine wapo katika nchi nyingi tu katika Afrika. Lakini Nyerere na Karume walikuwepo Tanzania tu!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom