Matumizi ya Over Drive (OD) kwenye gari automatic | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matumizi ya Over Drive (OD) kwenye gari automatic

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Albedo, Aug 24, 2009.

 1. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Wakuu naomba kufahamishwa, ni mahala au muda gani natakiwa kutumia OverDrive funcionality kwenye auto transmission. Ni kwa Ufahamu tu

  Nawakilisha
   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Acha uvivu search the internet ha ukigugo tu unapata straight!
   
 3. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Huko napata theory tu, nataka watu wanieleze kutokana na exerience zao na kutokana na ukweli road conditons za bongo ni tofauti na zao akina google na yahoo au bing
   
 4. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Bonyeza overdrive ukiwa kwenye highway, especially kama unakwenda mwendo wa kasi ambapo hutasimama mara kwa mara k.m. ukiwa katika safari ndefu.

  '...
  Overdrive can refer to two different things. An overdrive is a device which was commonly used in [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Automobiles"]automobiles[/ame] to allow the choice of an extra-high overall [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Gear_ratio"]gear ratio[/ame] for high speed cruising, thus [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Fuel_efficiency"]saving fuel[/ame], at the cost of less [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Torque"]torque[/ame]. Usually the final or [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Top_gear"]top gear[/ame] is called overdrive. Non direct drive gears increase torque multiplication at the expense of higher engine rpm and thus, decreased fuel economy.
  It also refers to a combination of gearing inside a transmission or [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Transaxle"]transaxle[/ame] which results in the output speed being greater than the input speed. In the latter case, "overdrive" does not refer to a physically separate identifiable part/assembly.'
   
 5. Jephta2003

  Jephta2003 JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2009
  Joined: Feb 27, 2008
  Messages: 3,592
  Likes Received: 1,894
  Trophy Points: 280
  Mkuu Over drive inakuja unapotaka kwenda speed zaidi ya 80,so gari inakuwa na uwezo wa kuingia gia no 5
   
 6. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #6
  Aug 24, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,647
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280


  Kwa hiyo mkuu utaona kuwa kwa mazingira yetu ya Dar mara nyingi OD inabidi iwe on (na ikiwa off huwa inawaka taa either kwen dashboard ) kuonyesha kuwa iko off na u have to think kwa nini iwe off,

  Mi binafsi naiweka off kama ninataka kuachieve speed kubwa kama kuovertake chap chap kisha kuirudisha on. Ikiwa off inakula sana wese.

  Source: Wikipedia.
   
 7. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2009
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Keizer, Ndege ya Uchumi salaam!

  Kwa lugha rahisi, OD ni gia namba 5 ambayo inakupa mwendo uliotulia, wa kasi lakini kwa mzunguko mdogo wa injini (RPM). Hii hukuwezesha kuwa na matumizi madogo ya mafuta pengine kwa kasi zaidi.

  Unaweza kuitumia pia ikiwa unataka kuipita motakaa nyingine, mathalan, kwenye kilima ambapo nawe motakaa yako inakuwa umepungua nguvu, hivyo unaweza kuiweka off (hapa unakuwa kama umerudisha namba 4), na injini itabadili kasi ya mzunguko, utaiweka uklisha maliza tena matumizi yake.

  Eneo lingine, ni mara gurudumu la motaklaa yako linapopasuka. Ikitokea hivyo, unaweza kuondoa OD, huku ukiwa umeacha kukanyaga pedeli ya mafuta, kwa maana ndiyo utakuwa unaomba mwendo upungue pasi na kukanyaga breki. Katika hali kama hii, utakuwa umesaidia kupunguza mwendo wa gari wakati ukithibiti muelekeo wa motokaa pia.

  Watu wengine katika hali kama hii huwa wanakanyaga breki. Kufanya hivi ni hatari, maana unasimamisha kabisa mwendo wa gurudumu lililopasuka, na matokeo yake mwendo wa motokaa, badala ya kwenda mbele, itajaribu kutii amri ya gurudumu linalogomea motokaa kwenda mbele na kuamua kwenda upande wa gurudumu lilipasuka, nikiwa na maana kwamba hapo motokaa itakuwa inaacha njia na au kupinduka.

  Kwa giaboksi zenye kujibadili zenyewe, ni vema basi tukaziacha OD zijiendeshe zenyewe, maana kuziondoa hatari yake ni kuwa unaweza kusahau kuiweka tena unapokwenda zaidi ya km 70 kwa saa, mfano barabara ya Nyerere, na kusababisha matumizi makubwa ya nishati ya kuendeshea mtambo.
   
 8. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #8
  Aug 24, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mbalamwezi Shule kubwa sana hii na inabidi watu wengi zaidi waifahama maana kila kukicha bei ya Mafuta inapaa kama Ndege ya Uchumi ya EL.

  Asanteni wakuu kwa maelezo yenu mazuri na Jengefu
   
 9. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #9
  Aug 24, 2009
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  mimi nilikuwa naitumia kwenye rafu roads kwani nikiweka huwa gari inakuwa zito hivyo nikitaka kuwahi huwa nazima kweli wajapani tunawahitaji kwa maelezo ya product zao
   
 10. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  hii thread imenielimisha sana jamani,asante kw aalieuliza na waliotoa majibu mazuri na murua kabisa,ninatumia auto sometimes so nitaiweka OD on mda wote!!
   
 11. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #11
  Aug 24, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Mkuu asante umesomeka vizuri sana.
   
 12. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #12
  Aug 24, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  JF ni kila kitu, Majibu ya Maswali yako yote yako hapa Jamvini Mkuu, wewe ni sula la ku initiate, Watu si Wachoyo hapa.

  Asanteni
   
 13. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #13
  Aug 24, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
   
 14. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #14
  Aug 24, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Ila drive gari manual kuna raha yake. Bongo siku hizi waendeshaji ni wengi sana, madereva ni wachache. Nilikuwa na gari yangu manual kutaka kuiuza kila mtu akiiona anasema ingekuwa automatic angenunua kwa bei ninayotaka mimi, vinginvyo nipunguze bei. Nikaamua kuahirisha mpango wa kuiuza LOL!
   
 15. MduduWashawasha

  MduduWashawasha JF-Expert Member

  #15
  Aug 24, 2009
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 1,568
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  huyo aliyesema ukivuka 80 kpm unatumia mafuta kidogo sidhani kama ni mkweli.unavyokanyaga zaidi ndo mafuta yanakwenda zaidi.theory hiyo inawork kama uko kwenye speed kubwa zaidi kama 140 kmp au zaidi au chini ya 80.otherwise overdrive ni kwenda gear number 5 na kwa mazingira ya day iweke off daima kwani wataalam wanasema kuiacha on saa zote ina damage engine kinamna achilia mbali suala la consumption kubwa
   
 16. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #16
  Aug 24, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,647
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
   
 17. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #17
  Aug 24, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  nami nimepatapata hapo. nashukuru wengi mliochangia. Tumeelimika wengi
   
 18. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #18
  Aug 24, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkuu na wewe unaendesha auto? kwani wewe ni mlemavu? Gari manual bana.....
   
 19. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #19
  Aug 24, 2009
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Mdudu,

  acha kudhani dhani juu ya mambo ya kitaalam. motakaa katika hali ya kawaida, na kwa wastani, inatumia mafuta mafuta kidogo kabisa ikiwa kwenye mwendo wa kati ya 70 km kwa saa na 110 kwa saa. Ukizidi hapo, unakuwa kwenye matumizi ya juu kabisa.

  RPM (Revolution per minute) ni kiwango cha mzunguko wa injini. Ikiwa unatumia gia namba 4 hadi mwendo kasi wa 70 km kwa saa, basi inawezekana, kama injini ni nzuri, RPM ikawa kwenye 2600-2800 hivi kama uko kwenye mpango wa OD, basi motokaa yako itabadili gia na kuingia kwenye 5, ambayo ni OD, na ukizidisha hadi kati ya 80 na 90 hivi, basi RPM itapungua hadi kufikia 2200 hadi 2500 hivi.

  Maana yake nini? Maana yake injini sasa itazunguka mara chache zaidi kwa mwendo kasi zaidi (70km/h hadi 110 km/h).

  Ukizidisha toka 120km/h na kuendelea, basi na RPM zitaongezeka na mafuta yatanywewa mengi tu.

  Auto zinafaa sana kwenye foleni kama za Dar, ambako unaepuka sana matumizi ya kilachi (clutch), maana unajikuta mguu wa kushoto unakuwa busy kukanyaga kanyaga ndani ya mita pengine 200 tu katika dk 45 pale Moroko saa mbili asubuhi.

  Manual zinafurahisha long trips, unajidai na unajisikia hasa unaendesha. Unaweza kuiamuru gari kwenye milima iende upesi zaidi, si kama auto ambayo inapanga yenyewe. Unaweza kumpita mwingine kwa wepesi wa hali ya juu, si kama auto ambayo itabidi uondoe OD ndo uongeze kasi ya kumpita.
   
 20. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #20
  Aug 24, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Sasa hivi magari ya manual ya kutoka Japan yanauzwa bei ghali zaidi kuliko ya automatic.
   
Loading...