Matumizi ya neno "Lugha ya kitaalam"

luangalila

JF-Expert Member
Jan 12, 2014
6,325
6,868
Kumekuwa na kasumba kwa baadhi ya wa Tanzania wa kada mbali mbali pale wanapo elezea jambo sasa inapokuja kuli tafsiri ilo neno au msamiati kutoka English kuja kiswahili, au kiswa kwenda Eng utasikia mtu anasema eti kwa lugha ya kitalaam inaitwa.

Mfano:

Mtalaam wa lishe labda anaelezea kiwango cha lishe kilichopo ktk bidhaa flani. Sasa una kuta anaelezea iyo alafu ana switch eti anasema kwa lugha ya kitalaam kinaitwa NUTRITION VALUE. Sijui wadau mmeelewa.

Mfano wa pili una kuta mtalaam wa kada ya ukaguzi wa majanga. Anaelezea hatua za ukaguzi sasa anafikia hatua ya kuelezea hatua ya chujio la athari sasa hajui basi ana chomekea eti au kwa lugha ya kitalaam inaitwa SCREENING. Kumbe hhapo ni msamiati tu na sio lugha ya kitaalaam.

Tuache izi mambo wa Tanzania.. tabia ya kuiita misamiati ya kingereza eti lugha ya kitaalam ni uchuro.
 
Mkuu kwa hawa wataalam wetu wasiokuwa na uwezo wa kugundua chochote zaidi ya koroboi na kibao cha mbuzi.

Bila kuongea maneno hayo ya kingereza basi hawana cha zaidi kudhihirisha utaalam wao kwa wengine..

Maneno kama .

Of course.
By the way.
In the matter of fact.
Actually.
Effective.
You know

Hayo ni ya kawaida kuyasikia kwako.
 
Kuna maneno ya kitaalam kweli. Sio kwamba hamna. Maneno ya kitaalam ni yale ambayo yanakuwa mahsusi katika eneo fulani na hutumika owa wingi katika eneo hilo. Na ambayo ukitafsiri kuwa kiswahili basi huwa magumu zaidi kuliko ukiyaacha kama yalivyozoeleka.
 
Kuna maneno ya kitaalam kweli. Sio kwamba hamna. Maneno ya kitaalam ni yale ambayo yanakuwa mahsusi katika eneo fulani na hutumika owa wingi katika eneo hilo. Na ambayo ukitafsiri kuwa kiswahili basi huwa magumu zaidi kuliko ukiyaacha kama yalivyozoeleka.
Ni kweli kuna maneno ya kitaalam

Lkn kuna maneno mengine ni misamiati tu mfano ukisikia neno carbon seqwetration unaweza ukazani ni lidude kumbe ni msamiati tu ..au ukisikia carbon footprint. Yote ni misamiati tu
 
Kumekuwa na kasumba kwa baadhi ya wa Tanzania wa kada mbali mbali pale wanapo elezea jambo sasa inapokuja kuli tafsiri ilo neno au msamiati kutoka english kuja kiswahili, au kiswa kwenda eng utasikia mtu anasema eti kwa lugha ya kitalaam inaitwa ... Mfano

Mtalaam wa lishe labda anaelezea kiwango cha lishe kilichopo ktk bidhaa flani ... Sasa una kuta anaelezea iyo alafu ana switch eti anasema kwa lugha ya kitalaam kinaitwa NUTRITION VALUE . Sijui wadau mme elewa

Mfano wa pili una kuta mtalaam wa kada ya ukaguzi wa majanga. Anaelezea hatua za ukaguzi sasa anafikia hatua ya kuelezea hatua ya chujio la athari sasa hajui basi ana chomekea eti au kwa lugha ya kitalaam inaitwa SCREENING . Kumbe hhapo ni msamiati tu na sio lugha ya kitaalaam.

Tuache izi mambo wa Tanzania.. tabia ya kuiita misamiati ya kingereza eti lugha ya kitaalam ni uchuro .

Hapa kwa lugha ya kitaalam tunasema kimeumana
 
Ktk taarifa ya habari ya itv, kisa cha kifo wa kijana huko Mara, polisi kaelezea ya kuwa sababu ya kifo ni kuvuja damu kwa ndani basi waandishi waka uliza kwa kitalaam kina itwaje jamaa akajibu internally bleeding
 
Back
Top Bottom