Matumizi ya modemu vs gharama za vifurushi vya muda wa kuperuzi na maongezi

Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Tafadhali simu yako simply ni GSM modem, iunganishe na internet na itumie kama universal modem. Mfano ukipata Tigo XTREME pack, una dk 15 za kuongea, sms 100, na mb 50 ndani ya masaa 24, kwa nini usitumie simu kama modem kama mimi hapa ili ufaidi hizo 50 mb or whatever package.

Lakini hii ni kwa matumizi ya kawaida sio kudownload mafile makubwa.
 
Mabwana na mabibi nashukuru kwa ushauri wenu sasa nafikiria kutupa hizi MODEM za AIRTEL na ZANTEL,kabla sija fanya hivyo naomba mnijulishe bei ni shilingi ngapi kwa modem ya TTCL.
ASNTENI SANA KWA UJUMLA
Hii kitu tumeshaijadili hapa jukwaani na gharama zake jm unatupa Moderm ya Airtel utajuta hasa km ni ya Zain hii ni modem inayobeba 400mb kwa 2,500/ kwa wiki ww weka hata line ya tiGo kwa bei ya 450/ utatumia 50mb saa 24 wakati TTCL haiwezi
Hawa Airtel ni kiboko wameungana na BlackBerry wanashusha kwa saa 24 kitu inaitwa GENGE kwa 700/ tu au 3,500/ kwa wiki TTCLHakuna bora tiGo lkn tafuta modem ya Zain (kabla ya Aitel)
 
Nafikiri kwa unlimited downloads hata zantel wana offer nzuri kuliko hii ya ttcl. Kwa shiling 10000 (elfu kumi), unaweza kutumia siku tatu kwa data size yeyote ile.

Mkuu mimi hapa nina modem 3, moja nimechakachua lkn 2 (ttcl & voda) zimegoma, sasa sina tena mpango wa kuongeza nyingine(zantel), vipi naweza kutumia line ya zantel kwenye modem hii niliyochakachua(unlock) na nikapata speed nzuri?
Nimechakachua ya zain.
 
mimi nina AIRTEmodem ambayo napata mb150 kwa shs 2500,Je kwa wale wanaopata mb 400 kwa sh2500 mnafanyaje?
 
mimi nina AIRTEmodem ambayo napata mb150 kwa shs 2500,Je kwa wale wanaopata mb 400 kwa sh2500 mnafanyaje?

Tuma sms INTERNET kwenda 15444 salio yako lazima iwe 2505 na kuendelea... ukitumiwa meseji inayosema hauna salio la kutosha kujiunga na huduma hiyo... we endelea kurudia rudia kutuma tena hadi ufanikiwe...
 
Mkuu mimi hapa nina modem 3, moja nimechakachua lkn 2 (ttcl & voda) zimegoma, sasa sina tena mpango wa kuongeza nyingine(zantel), vipi naweza kutumia line ya zantel kwenye modem hii niliyochakachua(unlock) na nikapata speed nzuri?
Nimechakachua ya zain.

Unaweza kuitumia line yako ya zantel kwenye modem ya zain uliyoichakachua....
 
Back
Top Bottom