Matumizi ya Marais Wengine wa Afrika Yanatisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matumizi ya Marais Wengine wa Afrika Yanatisha

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Sep 8, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,229
  Likes Received: 4,022
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Rais wa Cameroon, Paul Biya na mkewe Sunday, September 06, 2009 4:40 AM
  Wakati wananchi wake wakifa njaa, rais wa Cameroon Paul Biya ameshtumiwa kwa matumizi mabaya ya pesa za serikali kwa kukodisha vyumba 43 kwenye hoteli ya nyota tano nchini Ufaransa na kutumia karibia dola milioni moja kwaajili ya likizo yake ya siku 20. Rais Paul Biya wa Cameroon ameshtumiwa kwa matumizi mabaya ya pesa za serikali kwa kufanya likizo ya wiki tatu katika ufukwe wa La Baule nchini Ufaransa na kukaa kwenye hoteli ya nyota tano ya L'Hermitage Barriere hotel.

  Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Ufaransa, Rais Biya, mkewe na ujumbe wake wamekodisha jumla ya vyumba 43 kwenye hoteli hiyo na watakaa siku 20 kwenye hoteli hiyo wakati wa likizo yao nchini Ufaransa.

  Rais Biya inasemekana anatumbua kiasi cha dola 40,000 za Marekani kila siku na kufanya gharama za matumizi yake mpaka likizo yake ya siku 20 itakapoisha kukaribia dola milioni moja.

  Likizo hiyo imeamsha hasira toka kwa wananchi na baadhi ya viongozi nchini Ufaransa kutokana na kwamba Ufaransa ilitangaza mwezi julai mwaka huu kuwa itatoa msaada wa euro milioni 573 kwa Cameroon ili kusaidia kulipia madeni yake na kupambana na umaskini.

  Kipato cha wastani cha raia wa Camroon kwa mwaka mzima ni takribani Shilingi za Tanzania Milioni 1.5 na karibia nusu ya raia wake wanaishi maisha ya kifukara chini ya mstari mwekundu wa umaskini.

  Waziri wa mawasiliano wa Cameroon, issa Tchiroma amepingana na shutuma hizo dhidi ya bosi wake na kusema kuwa rais Biya ana haki ya kufanya likizo.

  Vyombo vya habari vya Ufaransa kwa kulinganisha matumizi ya marais wa Marekani wanapofanya likizo zao binafsi sehemu mbali mbali duniani , walipingana vikali na matumizi hayo ya rais Biya.

  Wakati rais Obama na familia yake walipofanya likizo yao katika kisiwa cha Martha's Vinehard kilichopo kwenye jimbo la Massachusetts, mwanzoni mwa mwaka huu, hawakukaa hotelini na walitumia pesa zao wenyewe kukodisha nyumba kwaajili ya likizo yao.

  Televisheni maarufu ya Ufaransa, France 24, ilihoji katika taarifa yake ya habari inakuwaje rais wa wa mojawapo ya nchi maskini duniani anaweza kutumia kiasi hicho cha fedha kwaajili ya likizo yake.

  Rais Biya akiongea na gazeti la Ouest France la Ufaransa alisema: "Hii ni mara ya tatu tumefanya vakesheni katika mji wa La Baule. Tumevutiwa na mji huu na tunafikiria kuja tena siku nyingine".


  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3013466&&Cat=2
   
Loading...