Matumizi ya mali za serikali kwenye shughuli za kichama ina tija kwa walipa kodi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matumizi ya mali za serikali kwenye shughuli za kichama ina tija kwa walipa kodi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KOMBAJR, Oct 1, 2012.

 1. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Katika kile ambacho kinaonekana ni mwendelezo wa yale ambayo yamekuwa yakifanywa na chama tawala kutumia rasilimali ya nchi kwenye shughuli za chama mapacha wao CUF nao wameingia kwenye huo mtego!Katika kile ambacho wananchi wamekuwa wakikipigia kelele kimejitokeza Juzi Wakati Malim Seif alipokwenda Arusha kwenye Mkutano wa Kichama ambao hauna uhusinano wowote na akatumia ndege ya serikali na akapokelewa na viongozi wa serikali wa mkoa.

  Wadau hii imekaje? Picha zinajieleza zenyewe hapo chini: DSCF1540.jpg DSCF1537.jpg pembeni unaona ndege ya serikali.
   
 2. iron2012

  iron2012 JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 358
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  naomba kukufafanulia jambo ndege za serikali hata wewe unaweza kukodi hivyo si ajabu kumwona Seif akiwa nayo, kuhusu kupokewa na viongozi wa serikali ni sawa kwa kuwa bado nin kiongozi wa serikali
   
 3. T

  Tiger One JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 569
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Hilo la ndege ya serikali wala sio issue kwani mimi mwenyewe nshaikodi na kupeleka msiba nyumbani kwetu bila taabu.
  Issue ni kubeba wafuasi kutoka dar magari zaidi ya 15.
  Hiyo galama si matumizi mabaya ya fedha za umma?
  Imekaajee hii ya kujaza uwanja wa mkutano arusha kwa wafuasi toka zanzibar, pwani, tanga na dar?
   
Loading...