Matumizi ya Magari ya Serikali baada ya muda wa Kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matumizi ya Magari ya Serikali baada ya muda wa Kazi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Eeka Mangi, Dec 19, 2010.

 1. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #1
  Dec 19, 2010
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Jamani mi naomba tu kukumbushwa maana sio kila kitu unaweza kukijua. Miaka ya nyuma niliwahi kusikia kuwa kuna muda maalumu wa matumizi ya magari ya serikali na umma.

  Sheria hii ilikuwa kali sana kiasi cha kuwafanya mabosi kutumia magari yao binafsi.

  Sasa ninachouliza , Je, sheria hii bado inatumika ama ilishabadilishwa? nauliza hivi kwa kuwa naona magari ya serekali kwenye harusi ama ubarikio mchana na hata usiku mwingi pia.

  Je, wakati ka huu gari huandikiwa liko wapi na kwa kazi gani.

  Kama sheria haijabadilishwa kwa nini wanaotoa vibali kama hivi (Maana dereva hawezi kujiamulia tu) wasichukuliwe hatua za kinidhamu ili kunusuru makali ya majasho ya wavuja jasho wa nchi hii. Kwa wale waliokwazika naomba mniwie radhi.
   
 2. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #2
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hili kweli limekuwa tatizo kubwa sana na limekuwa likiliingizia hili taifa hasara kubwa mno. Wahusika waliangalie tena hili na kulifuatilia. Tatizo la hili taifa ni kwamba, wana sheria za zima moto. Leo wakisema bomoeni vibanda hii ni op ya miezi miwili. Wanaunda tume ya kusimamia ubomoaji na op kwa ujumla. Hawana mwendelezo baada ya muda kwisha wanasahau na hakuna tena mtu wa kusimamia hivyo vibanda kutojengwa tena. Pale masaki 4 ways wamerudi na vitanda vyao full na vibanda vidogo vidogo vimeanza ota likini tukumbuke kuwa watu walitumia pesa kukomesha vibanda pale.
   
 3. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #3
  Dec 19, 2010
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mimi naamini kuwa wafanyakazi wa mashirika ya uma wengi wao wenye madaraka wana magari yao binafsi! Kwa nini kwenye shughuli zao binafsi wasitumie mali zao? Gari hili likipata ajali usiku huwa linaandikwa vipi? Lilikuwa nje kikazi? Linajazwa mafuta na nani? Kwa kibali cha nani. Serekali yetu inaacha mianya hii na inafikia mahali tunaanza kutembeza bakuli kuomba msaada wa kuendesha serikali. We are no where to depend on someone while we are misusing our resources. Viongozi nao ifike mahali waone aibu. Emagine leo naona magari 3 ya shirika moja yanashughulikia ubarikio wa mmoja wa wafanyakazi? Fikiria landcruizer 3 na madereva wa uma watatu ubarikio tuu! Je harusi? No serikali ifikirie tena!
   
 4. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #4
  Dec 19, 2010
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nasikia eti siku hizi kuna na wizara (kama sio idara ndani ya wizara fulani) ya maadili ya uma. Hao viongozi wa mashirika hayo wamefundishwa maadili kweli?
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Dec 19, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  tena utakuta haohao wa idara ya maadili ndio wanavunja hizo sheria na kanuni za maadili.
   
 6. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #6
  Dec 19, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Katika Tanzania ya leo sheria ni kwa wadogo, wakubwa hao kwasasa wako juu ya sheria. Si kila kukicha unamsikia mtendaji mkuu wa serikali Pinda naye akilalama kama yeyote yule juu ya matendo hayo. Sasa kama mtendaji mkuu anajiona hana uwezo wa kuyakomesha, nana mwingine amfunge paka kengere.
   
 7. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #7
  Dec 19, 2010
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  ndg kumbuka hii bogo ina ongozwa na katiba. Hivo jambo lolote mtu yyte haruhusiwi kufanya jambo lolote kinyume na katiba.labda niseme hivi hapa kwetu sharia zipo ila hazifuatwi.mfano kuvuta sigara hadharani.yan hata kituo cha polis mtu anaweza kuvuta na hakuna atakae uliza.mimi nadhani watanzania tungekuwa tunaifahamu sheria labda hata mimi ningeweza kujua mtu flan kakosea na anastahili nini.
   
 8. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #8
  Dec 19, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,537
  Trophy Points: 280
  Sheria bado ipo. Mwisho wa kutumia gari za serikali (STJ/STK) na mashirika ya umma (SU) ni saa 12 jioni. Sasa kwavile hakuna utawala wa sheria wenye manufaa kwa wananchi,ndo mana si ajabu kuyakuta magari hayo sehemu kama izo,tena hata weekends,na hata kwny bars and pubs! Pengine Bwana Pombe ataliona hili,kama kawaida yake ya kucheza na jukwaa!
   
 9. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #9
  Dec 20, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  we mangi embu tuache baba zetu wale na mana na wao wafwate hao hao waakina rostam ...jamani ebo sasa na sie landcruiser tutpanda lini kama si wikiendi
  kafomeku
   
 10. semango

  semango JF-Expert Member

  #10
  Dec 20, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  mi ninaimani iko siku mambo yote yatafikia kikomo.inatia uchungu sana jinsi tunavyokamuliwa PAYE halafu wachache wanakula bata tu.
   
 11. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #11
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  Wazazi wetu walisemaga hivyo hivyo ipo siku mpaka wanaondoka dunian ..la maana na we tafuta channel utokee basi ukisubiri siku utasubiri mpaka YESU anakuja ndugu m sitaki kudanganya watu hasa vijana kama wewe...pagawa na maisha ukisikiadili inaita pasua songa mbele kama dereva anaendesha shangingi jiulize linitaendesha lako...anza sasaXMASS NJEMA JAMANI KAMA MTAIONA MKIKAWAWA KILA LA KHERI MUENDAKO
   
Loading...