Matumizi ya mafuta - Nissan X-Trail

ASHA NGEDELE

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
784
326
Habari wadau.

Naomba ushauri kwa mwenye ujuzi na gari za Nissan Xtrail model ya 2002 sababu ninahisi ya kwangu inatumia mafuta mengi sana. Nina miezi mitatu nayo toka niiagize kutoka japan.

Ulaji wake: 6.5km kwa lita (nishaipima mara tatu kwa kujaza full tank na kuhesabu mileage kabla ya refill)
Mileage: 120,000km
Check engine: Haiwaki kwahio nina-assume sensors zote ziko sawa.
Plugs: Nimeshabadili na zote zinachoma vizuri
Gearbox: Iko poa sababu gear zinabadilika kwa haraka tu.
Service: Nishafanya.

Naomba yeyote mwenye kujua nini cha zaida natakiwa kufanya ili walau ifike 8.5km kwa lita moja ya petroli.

Asante
 
Gari yangu ni toyota allex kuna kipind ilikuwa haizid spidi 100 ínAkuwA nzito nikaipeleka kwa fundi akakata exhaust akazibua km mmaudongo akayatoa akarudishia. Sa hv bia km kawa je kutolewa kwa hizo ndude kwenye exhaust haiwez leta tatizo kwenye injin
 
Tafuta mtu uliuze hilo ndio yanaanzaga hivyo litakuua kwa presha,then tafuta gari ya wastani tu Vvti engine 1500 cc below,itakusaidia kwa mizunguko yako.
 
Wakati mwingine ulaji wa mafuta unachangiwa na uendeshaji wa gari. Ukanyagaji wa mafuta bila kuwa na mpangilio unaweza kusababisha fuel consumption kuwa kubwa. Ili matumizi ya mafuta yawe economical zingatia yafuatayo:
(1) Jizuie kukaganya mafuta kws ghafla kwa ni utajikuta rpm imepanda ghafla huku speed haijaongezeka.
(2) Jizuie kuendesha gari huku rpm ikiwa 3 au zaidi. Mara nyingi rpm ikiwa 3 au zaidi mafuta hutumika mengi sana.
(3) Chunguza brake pad kama ziko ok. Brake pad zinapoanza kuchoka husababisha matumizi makubwa ya mafuta.
 
Nimekusoma mkuu
 
Gari yangu ni toyota allex kuna kipind ilikuwa haizid spidi 100 ínAkuwA nzito nikaipeleka kwa fundi akakata exhaust akazibua km mmaudongo akayatoa akarudishia. Sa hv bia km kawa je kutolewa kwa hizo ndude kwenye exhaust haiwez leta tatizo kwenye injin
Hapa mkuu nakushauri ungeanzisha uzi wako ktk hili!
 
hiv kwa nn hizi xtrail zisipigwe BAN kuingia TZ. tushachoka habari zake
Gari ni nzuri sana hizo isipokuwa spare zake ghali. Mafundi wengi ni wezi tu. Shida kubwa ya xtrail ni kuchemka na hatimaye kuunguza cylinder head gasket au cylinder head yenyewe. Hakikisha maji yapo sawa ktk radiator yako na uwe makini na gauge ya temperature ukiwa safarini
 
Back
Top Bottom