MADA: Fahamu kuhusu matumizi au ulaji wa mafuta kwenye gari aina ya Toyota harrier 3.0L (2990CC)

muuza ubuyu

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
3,508
3,474
Habari za mapumziko waungwana!

Ningependa kujua utumiaji wa mafuta wa gari tajwa hapo juu, Toyota harrier! Najua watu wanaiponda sana katika utumiaji wake kwa sababu ya ukubwa wa injini! Sasa kutoka kwa wataalamu, mafundi na wazoefu wanipatie figure halisi ya utumiaji mafuta wa gari hili hasa nje ya miji yaani km ngapi kwa lita moja ya mafuta.

Nishawahi kuwa na gari yenye cc2500 ilikuwa natumia wastani wa 10km/Litre. Mie siishi miji mikubwa kama Dar ila pia mazingira yangu yananihitaji kusafiri kwenda mbali in a limited time na pia nahitaji a comfortable car ndo maana nika-opt toyota harrier 3.0L.

Je, consumption yake ipo below 8km/L?

Please nahitaji mzoefu wa gari hili anipe maelezo mazuri na ya kina!

Thanks.
1587281476727.png
===
BAADHI YA MAJIBU YALIYOTOLEWA NA WADAU
Harrier 3.0L ina engine ya 1MZ VVTI ambayo pia ipo kwenye Kluger na magari mengine mengi.

Consumption ndugu bila kudanganya ni 5.5-6.5km/l kwenye urban areas, halafu inatembea 6.5 hadi 8 kwenye safari.

Gari hii unaweza fikisha 10-12km/l kama hautazidi speed 80 (yani speed 60,70-80) ukiwa safarini, lakini nachoweza kukwambia kwa nguvu ya engine na konfotabiliti yake huwezi heshimu mwendo huo na pia kwenye safari utachoka sana which means utajikuta unafall kwenye matumizi ya 6.5-8km per litre.

Asante
---
What are you talking about?

Harrier Hybrid ina engine ya 2.5L 2AR - FE au 3.3L 3MZ FE Engine which means hizi engine zinasaidiwa na electric motor kuongeza nguvu ya gari kwa kupunguzia pistoni kazi ya ziada kwenye speed na matumizi mengine ya umeme.

Kwa hiyo naweza kusema Harrier Hybrid haina engine ya 3.0L mkuu, na kutokana na kuongezewa kifaa kingine kwenye efficiency (yani electric motor) basi imesaidia kupunguza matumizi ya mafuta though cylinder capacity inaonekana kubwa kwenye 3.3L. Unaweza kutembea 10-13km/l kwa urban areas na unaweza fika 15km/l kwenye safari mkuu ikiwa engine yako bado ni nzuri na haina shida.

Hybrid ni level nyingine mkuu ambayo naona kama jamaa atahitaji kuongeza budget yake tena.

Nasisitiza tena factory made harrier hybrid haina engine ya 3000cc
---
Ndio mkuu, Harrier hiyo 2.4 ni bora kidogo kwenye matumizi kuliko ile ya 3.0

Ina engine ya 2AZ ambayo unaikuta kwenye RAV4,Alphard,Kluger na magari mengineyo pia.

Gari hii inatumia km8 kwa litre maeneo ya mjini na foleni ila kwenye high way inatembea kilometer 10-11 kwa lita mkuu.

Angalizo kama ukitembea speed 70-80 kwenye high way unaweza ukasave mafuta sana yani consumption inaweza range kwenye km13-15 kwa lita mkuu kama hutakua na papara kwenye driving
---
Ulaji mbovu wa mafuta ya gari unategemea na vitu vifuatavyo
1.uendeshaji wako kaka wewe ni mzee wa kukamua unaingia road unanza kwa kukanyagia lazima wese liende.

2.foleni za magari epuka kutembea kwny foleni sehemu ya dakika tano unatumia nusu saa aheri upaki gari utafute tz 11 uendelee hapo mafuta yanaenda km umewasha jiko la mchina.

3.oxygen sensor nzima kama mbovu lazima unywewe mafuta kama mademu wanavyokunyeea vyabe bulee.

4.plug mbovu feki usitegemee plug za buku 6 zikawa nzuri itakula kwako mazima nunua plug za ukweli huna hela park gari.

5.tafuta sweet speed yako kwny highway unatulia na kubarizii siyo ukamue 150 utegemee tank lisiwe na matobo walau izizidi 120.

6.usiache madirisha wazi kwny highway garibinakuwa nzito na wese linaenda jingi.

7.kama ni ya petroli mara mojamoja weka petrol treatment inasafisha njia za mafuta na kurahisisha uchomaji wa haraka.

8.epuka safari fupi fupi na sisizo na tija uokoe mafuta. Ukishindwa yote haya na unakuwa kinga'angaanizi basi usisumbue watu kwa maswali nenda baa tafuta mchemso saafi wa gari lako.
---
Ni kweli Mkuu nimeingia Google nikakuta upo sahihi na hata hizi za piston 4 zitumiazo 2.4 hazijaachana zinakula 11km kwa lita moja
Currently showing specs for 2.4 G (A)
  • ENGINE
  • Engine Capacity
    2,362 cc
  • Engine Configuration
    4-cylinder in-line DOHC
    Compression Ratio
  • 9.6
  • Bore x Stroke
    (88.5 x 96.0) mm
  • Fuel Type
    Petrol
  • Power
    119kW (160 bhp)
  • Fuel Consumption
    11 km/l
  • Transmission
    4-speed (A)
  • Drive Type
    Front-wheel drive
Na hiyo ya SIX CYILINDER ni
Specifications
498.jpg

Make ToyotaFamily HarrierModel Variant Harrier 3.0Year November 2000 to currentNew Price 269.5 ten thousand YenBody Type SUVSeating Capacity 5Engine Code 1MZ-FEEngine Type Water cooled V6 DOHC 24 valveEngine Size 3.0 litres (2994 cc)Bore � stroke 87.5mm � 83mmCompression ratio 10.5:1Fuel systemMax power 162kW @ 5800rpmMax torque 304Nm @ 4400rpmForced Induction NoFuel Tank Capacity 75 litresFuel type Unleaded premium gasolineFuel Consumption 10.5 l/100km Transmission Super intelligent 4 speed automatic (SupercEct)Drive Layout FF
---
Mkuu Joshua ok upo sahihi kwa Mji wa Dar lakini mimi wa Manyoni gas hiyo itakata tu nikivuka Morogoro kuelekea Msamvua.

lakini nikijaza Petrol ya 15,000/ nitapata lita 7 ambayo ni kama kilomita 80 Chalinze nitaongeza na kufika Manyoni.

Kwa sasa nimegundua Harrier New Model nyingi wameweka mashine ndogo ya Piston 4, hizi za 6 cyilinder wameziacha.

na hivyo kusababisha Harrier Old Model 3000cc kushuka hadi 5m


Cc LEGE ilonga
 
Sijui kuhusu Harrier ila nina uzoefu wa gari nyingine yenye injini kama hiyo. Highway inafikisha 10Km/L bila shaka na power yake inafurahisha. Ila mjini ndio hutakiwi kuwa na misele mingi kama mambo yako sio safi sana.
 
Sijui kuhusu Harrier ila nina uzoefu wa gari nyingine yenye injini kama hiyo. Highway inafikisha 10Km/L bila shaka na power yake inafurahisha. Ila mjini ndio hutakiwi kuwa na misele mingi kama mambo yako sio safi sana.
Thanks mkuu, mie si mpenzi wa mjini sana mkuu na mjini sipapendi sana maisha ya mbanano na foleni! Ila huwa nakuja mara chache chache kuosha macho !

Power ya injini hizo nazipenda sana, ngoja wajuvi wa harrier waje!!
 
Binafsi nafikiri Prado ya 2.7lts ingekua ideal kwako au unapenda harrier kwa kuwa C.G yake hiko chini hivyo si rahisi kupinduka.

Kitu kingine mbona kuna harrier za 2.7lts. au unazungumzia za diesel.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom