Je, matumizi ya mafuta kwenye Toyota Crown Athlete yapoje?

Ndo hicho kinafanya niipende Mazda. Nilikua na Mazda Axela Sports cc 1490 ya mwaka 2006. Aisee power yake ilikua kubwa mno. Nlitoka axela nikachukua rx8. Axela mpaka sasa imenipa experience nzuri zaid
Umechanganya mafile mazda axela. Haitumii rotary engine inatumia engine za kawaida zenye piston ... Sio gari zote za mazda zinatumia rotary engine ni matoleo mawili tu rx7 na rx 8

sent from HUAWEI
 
Kuna 3S-GE hio ipo kwenye Altezza RS200 Z - Edition hio hua ni manual nadhani ndo 220 HP ila nadhani hio 3S-GTE ipo kwenye Celica
3sge in stock mwisho ni 207 hp ikiwa manual na Automaic ni 197hp, wewe unazungumzia 2jzge kwenye is300 ndio ina 220hp
 
kuna mtu nimeona anapost fb kuwa watu wana imani mbaya na hili gari & kuwa halili mafuta kama inavyodaiwa bali ni kawaida sana..
sasa sijui analipamba sababu amekuwa analitangaza la kwake tangu january & bado hajapata mnunuzi
Uchumi ukiwa vizuri huwezi kuona mafuta ni tatizo kwako ukizingatia gari unalipenda.
Malalamiko yanatokana na mfuko kutokuwa vzr.
 
Wewe sasa ndio umeongea kitaalamu na kwa uzoefu. Kimsingi 4GR-FSE (Crown na Mark X) ni engine iliokuja ku replace 1JZ japo haiifikii kwa pulling ila imefanyiwa modification isile sana mafuta hata katika uendeshaji wa kawaida tu tofauti na ulaji wa 1JZ engine ilioko kwenye Brevis.

Kinachowaponza wabongo wengi ni poor car maintanance na poor driving skills. Economical driving watu hawazingatii wamekazana kusema gari flani ni 6 cylinder inakula wese. Kuna jinsi ya kuendesha gari sio ukishuka bumps unagandamiza mguu mpaka injini inavuma, taa zikiruhusu unabonyeza wese mpaka gia zikishift gari inastuka. Kwa uendeshaji mmbovu hata IST utaona inakula wese tu hamna namna.

Eco driving: Hakikisha mshale wa RPM hauvuki pale kwenye namba 2 kabla ya gear kuongezeka. Weka mguu taratibu kwenye pedeli ya mafuta hakikisha gari inaenda gear ya pili kiwepesi bila kuvuka zaidi ya namba 2 kwenye mzunguko wa engine. Hapo hata ukitumia V8 utaona haili wese!
Wewe unajua mkuu, elimu inahitajika hapa,nitakutafuta unipe mbinu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom