Matumizi ya mafuta kwenye jeep cherokee grand, naomba ushauri

ligolyser

Senior Member
May 9, 2013
155
15
Nina jeep cherokee grand limited ya mwaka 1996,fuel consuption yake kidogo hainipi matumain,kuna fundi akaniambia ni kwakua haina return ya mafuta (wataalam mnanielewa) ivo mafuta yakienda yameenda tofauti na magari mengine yenye return,

So nikagusia ishu ya kuibana isinywe bado sijapata fundi mzuri,naomba kuuliza je,nikiibana itapunguza uwezo wake na nguvu?ni cc3995.

Shukran.
 
Mkuu baada ya kufikia umri huo wa gari!! ni lazima ubadilishe Air filter ktk kila service ya gari itakusaidia uunguzaji wa mafuta...
 
ligolyser,

cc3995 petrol..... jipange tu ndio utaratibu wake huu... cheap to buy expensive to run!
 
Last edited by a moderator:
Ukiibana itapungua nguvu, kuanzia speed 100 kwenda juu ndo inakula sana wese,chini ya hapo ulaji ni wa kawaida.hebu twambie inakula lita ngapi kwa kilometa, na kwa speed ipi?
 
mkuu fafanua vizuri ili tukusaidie suala la gari kutokuwa na return sio ishu hapo coz asilimia kama 80 ya magari ya sasa hivi hayana return.

mkuu labda tukuulize kuwa hiyo gari mwanzo ilikuwa inakula mafuta kiasi gani na sasa inakula mafuta kiasi gani??

kuna vitu vingi sana hapo vya kuangalia kama plug,air clener,nozzel, ignition coil and wire.

je gari haina miss yoyote??
kitu kingine hapo jaribu kucheki oxygen sensor na idle sensor hivyo vikiwa vibovu huongeza uraji wa mafuta
 
nazan itakua 5km/ltr
 
ushauri mzuri sana huu mungu akubarik,,nilinunua kwa mtu ila nikaja kugundua kua inakunywa mafuta saana kama 5km/ltr,miss ipo boss
 
Mkuu sijui uchumi wako lakini maadam umeanza kulalamika kuhusu wese ni wazi utakuwa sio fisadi. Hiyo gari haikufai, fuel consumption hiyo hata VX V8 haioni ndani (7 km/litre). Huo ni ulaji mafuta unaokaribiana na wa Lori. Mafundi wakianza kuchokonoa chokonoa sana wataiharibu. Itumie mara mojamoja hivo au iuze tu. Lakini ni muhimu kuwa na gari yenye hadhi ya jeep home. Inalinda heshima mtaani.
 
umeongea kitu kizuri sana mkuu,asante boss
 
Back
Top Bottom