Matumizi ya madawa ya kulevya

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,293
33,078
Unahitaji kupata usaidizi dhidi ya matumizi mabaya ya pombe na dawa zengine. Bonyeza ili upate maelezo zaidi kuhusu uvutaji wa sigara, unywaji pombe na madawa ya kulevya.

Tumbaku na uvutaji sigara

Tumbaku ndio inayotumika vibaya ikilinganishwa na madawa mengine.Kuvuta sigara au kiko husababisha magonjwa haya, ugonjwa wa moyo, pigo, ugonjwa wa mapafu, saratani ya koo, kibofu cha mkojo, firigisi n.k
Watu wengi wanaovuta sigara wanajua kuwa ni mbaya kwa afya yao, jaribu kuwacha au usianze kuvuta.
Ukweli kuhusu tumbaku:

  • Tumbaku huleta saratani yam domo, ulimi, na 80% ya watu wanaovuta sigara walianza wakiwa vijana.
  • Kampuni za sigara huongeza madini ya ammonia kwa hivyo ubongo hufunikwa na nikotini.
 
Pombe na uraibu


Watu wengi hunywa mvinyo, ukinywa kwa kiasi hupunguza magonjwa ya moyo, lakini unywaji wa kupindukia utadhuru wote wanao kutegemea.

Pombe hudhuru viungo vyako, macho na kutoweza kujimudu. Kuendesha gari ukiwa mlevi na ulevi ukiwa mamba ni hatari kwa maisha yako, kwani husababisha ugumba, kuharibu ubongo, na mishipa ya damu pamoja na kuweza kukumbuka mambo.

Walevi hunywa pombe ili kusahau matatizo walio nayo, walevi wanaweza kufutwa kazi,na kukosa makao.

Dalili za matumizi mabaya ya pombe ni:

  • Kunywa zaidi ya chupa 1au 2 kila siku
  • Kutoweza kujizuia kunywa hata ukihapa
  • Kushikwa na polisi,kupigana,kutofika kazini
  • Kufikiria huna shida hata ukielezwa.
 
Madawa ya kulevya na uraibu

Ukishikwa na uraibu wa madawa ya kulevya, jamii yako, marafiki, wote huathirika, unakuwa na shida kazini na unajiweka hatarini mwa kupata magonjwa hatari kama Ukimwi.
Watu huanza kutumia madawa ya kulevya wanapokuwa na shida fulani kwa hivyo hutumia nafasi hii kujificha ndani ya uraibu huu. Madawa ya kulevya husababisha vurugu na uhalifu. Ikiwa una uraibu huu tafuta usaidizi.

Ukweli kuhusu matumizi ya madawa.

  • Moshi wa bhangi una kiwango kikubwa cha gesi ya dioksidi ya kaboni kuliko sigara ya kawaida
  • Unapotumia kokeini utazoeya na ukivuta nyingi waweza patwa mshituko wa moyo
  • Dawa ya Ecstasy yaweza kumfanya mtu anyauke na kukosa maji mwilini na kuleta matatizo na magonjwa ya figo.
  • Unapokuwa mlevi na madawa, uamuzi wako unakuwa mbaya huoni vizuri na umo katika hali ya juu kushiriki ngono bila kujikinga.
 
Aina ya madawa ya kulevya na madhara yake


Kuna aina tatu ya madawa ya madawa ya kulevya: Yanayoleta msisimko wa nguvu mwilini, yanayo zubaisha watu na yanayo lewesha watu.

  • Yanayoleta nguvu ni kama, kokaini, ecstacy, methamphetamines na kadhalika
  • Yanayozubaisha ni kama, pombe, bhangi na heroine.
  • Yanayolewesha ni LSD na mescaline.
Ni rahisi pia mtu kuwa na uraibu na madawa yaliyohalalishwa, hasa madawa ya kupunguza maumivu.
 
Bhangi

Majani ya bhangi huvutwa kama sigara pia inaweza kuchanganywa na vyakula na kuliwa.
Madhara yake ni tofauti kwa kila mtu. Kwa watu wengi hupumbaza kama pombe. Humfanya mtu kusahau au kuelewa mambo, kutoweza kuwasiliana vyema, na magonjwa mengine.
Walio na uraibu huongea wakivuta maneno na macho yao huwa kama yenye usingizi.





Crystal Meth

Methamphetamine ilitengezwa kutoka kwa Amphetamine na ina matokeo mamoja. Hupoteza hamu ya kula, kuongeza nguvu na kujiamini sana. Ina tengezwa kinyume cha sheria kote ulimwenguni
Huwa katika hali tofauti,y aweza vutwa, nuswa, kuliwa au kudungwa.
Methamphetamines humfanya mtu kuwa na tabia za kihalifu na kufanya vitu kwa mabavu.


Heroini


Huwa katika hali ya poda nyeupe au rangi ya mchanga. Hudungwa kwa sindano moja kwa moja kwenye damu,au hunuswa au kuvutwa kama sigara. Muda mfupi baada ya kutumia miili yao huwa mizito hisia zao hupotea.

Watumizi katika hatari ya kuitegemea kwa maisha yao ambapo ikikosekana kufa ni rahisi. Husababisha ugonjwa wa mapafu, moyo, na afya kudhoofika.

Kwa sababu ya kutumia sindano wamo hatarini mwa kuupata ugonjwa wa Ukimwi kwa sababu ya kutumia sindano moja.

Methadone ndio dawa inayosaidia wanaotumia kuwacha lakini pia inaweza kumfanya kutegemea dawa hii lazima maagizo ya daktari kufuatwa.


Kokeini

Rock kokeini ni bei rahisi na hupatikana kwa urahisi. Madhara yake ni kuwa humpa mtu msisimuko wa nguvu mwilini jambo linaloweza kuwaelekeza vijana kusuka na uhalifu au ngono bila kujikinga.

Huvutwa kwa kutumia kiko na baadhi ya vifaa vingine ni:

  • Neli ya majaribio
  • Bomba
  • Waya
  • Mifuko ya plastiki
  • Kiberiti cha sigara
  • Nyaya za stima
Dalili zinazoonyesha kuwa mtu anatumia kokeini:

  • Kutokwa na kamasi
  • Kutokwa damu puani
  • Kupunguka uzito kwa haraka
  • Kuzubaa
  • Ushari
  • Kujiamini zaidi
  • Wasiwasi
  • Mkakamavu

Rohypnol

Ni dawa inayofahamika ulimwenguni, hutumbukizwa katika kinywaji cha mtu hasa wasichana kisha kupoteza fahamu na kwenda kunajisiwa bila ya hata yeye mwenyewe kufahamu. Liwe onyo hasa unapokuwa katika vilabu vya pombe au sherehe popote, jihadhari dhidi ya kuwacha pombe yako bila mtu kuichunga. Huzidisha nguvu za pombe na kumlewesha mtu haraka.


Sukari


Sukari ni mchanganyiko wa madawa kama kokeini na heroini, ni dawa iliyo mfano wa poda, watumiaji hutajika kuwa na mrija ili wavute. Sukari sio bei ghali na wanaotumia hushindwa kuwacha matumizi yake
 
Ya kuzingatia

Ukishuku mtoto wako, jamaa yako au rafiki yako kama anatumia madawa ya kulevya, ishara ni kama zifuatazo:

  • Mabadiliko ya wakati wa kulala
  • Kupoteza hamu ya chakula
  • Kuwa na afya mbaya
  • Kutokuwa na umakinifu
  • Msiri
  • Muongo
  • Mchokozi na mwenye hasira
  • Kutokuwa mchangamfu
  • Kiwango cha chini cha kujistahi
  • Kupoteza fahamu
  • Kutokuwa na nguvu
Watumizi wa madawa huwa na vifaa kama:

  • Sigara au karatasi ya kusokota sigara au bangi
  • Bomba au kiko
  • Mimea ya ajabu poda na vidonge
  • Mbegu, matawi ya ajabu mfukoni
  • Marashi kufunika harufu
Ukimshuku mwanao, jifahamishe kwanza na madawa yanayo julikana kasha ongea naye kuwa unashuku kwa utaratibu ili wasiwe na hasira na bughudha.
Kumkinga mtoto kutokana na madawa huanza na uhusiano bora na mwanao, uaminifu kujua marafiki zake na tabia zao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom