Matumizi ya mabomu dhidi ya raia mara kwa mara ni dalili ya serikali kushindwa uongozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matumizi ya mabomu dhidi ya raia mara kwa mara ni dalili ya serikali kushindwa uongozi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Nov 15, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,915
  Likes Received: 83,387
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Migogoro haitakomeshwa kwa mitutu ya bunduki [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Monday, 14 November 2011 20:43 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] Mwananchi

  PICHA zilizopamba kurasa za magazeti mengi wiki iliyopita zilionyesha askari wa Jeshi la Polisi katika sehemu kadhaa nchini wakitumia silaha za moto dhidi ya wananchi, huku wakisababisha vifo na majeraha kwa baadhi yao. Picha hizo zilionyesha polisi hao wakitumia nguvu kupita kiasi na kuibua maswali mengi yaliyohoji kama kweli jeshi hilo lilikuwa linalinda usalama wa wananchi na mali zao au limeegemea upande mmoja na hivyo kuwa sehemu ya tatizo.

  Huko Mbeya, risasi na mabomu ya polisi vilitawala sehemu kubwa ya jiji hilo na kusababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi watu kadhaa. Vurugu hizo zilitokana na operesheni iliyofanywa na askari wa Jiji la Mbeya iliyokuwa na lengo la kuwaondoa wafanyabiashara wadogo (Wamachinga) katika mitaa ya jiji hilo. Katika vurugu hizo, watu 235 walikamatwa na polisi.

  Jijini Dar es Salaam, polisi waliwatia nguvuni wanafunzi 46 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kuandamana kuishinikiza Serikali kuwapa wenzao 1,000 mikopo ya elimu ya juu. Kabla ya kuwakamata, polisi walitumia mabomu na kutoa vipigo kwa wanafunzi hao waliokuwa wanaelekea sehemu za Ubungo kupeleka ujumbe huo kwa wananchi. Katika baadhi ya picha kuhusu tukio hilo, askari wawili wa kiume walionekana wakimdhalilisha mwanafunzi wa kike, huku wenzao saba wakiwa wameelekeza mitutu ya bunduki zao kwa mwanafunzi huyo.

  Wakati huohuo, jijini Arusha polisi walikuwa katika mapambano makali na viongozi na wafuasi wa Chadema waliowatia mbaroni na kuwafungulia mashtaka kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria na kukataa kutii amri halali ya polisi. Picha zilizopamba kurasa za mbele za magazeti zilimuonyesha mgombea wa kiti cha urais wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu uliopita, Dk Willibrod Slaa akiletwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Arusha kama mhalifu.

  Hayo ni matukio machache yaliyowahusisha polisi na wananchi katika kipindi cha siku saba tu. Matukio kama hayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara katika sehemu kadhaa nchini, hasa mijini. Ghasia zilizotokea katika majiji ya Arusha na Mwanza mapema mwaka huu yanatoa picha kwamba Serikali haioni tena umuhimu wa kutafuta suluhu kwa kufanya mazungumzo na makundi mbalimbali ya kiraia na kijamii pindi pande hizo mbili zinapotofautiana.

  Matokeo ni kwamba, Jeshi la Polisi limeegemea upande wa Serikali kukandamiza makundi ambayo yanadai haki zao za kikatiba kwa njia ya amani. Kwa mfano, jeshi hilo linapotumia maji ya kuwasha, mabomu na risasi za moto kuzima maandamano ya amani linachochea hasira za wananchi ambao wanaona haki zao za msingi zikizimwa na vyombo vinavyopaswa kuzisimamia na kuzilinda.

  Tukio la Mbeya mwishoni mwa wiki bila shaka litakuwa limetoa fundisho kubwa kwa Serikali na Jeshi la Polisi kutokana na hasara kubwa iliyotokana na kitendo cha polisi kutumia nguvu kubwa kuwaondoa Wamachinga katika mitaa ya Jiji hilo pasipo kuwaandalia sehemu stahiki za kuhamia. Tumeelezwa kuwa, ghasia hizo zimeharibu kilomita tatu za barabara, ambazo gharama yake ni Sh3 bilioni, licha ya uharibifu wa miundombinu nyingine uliotokana na vurugu hizo zilizochochewa na polisi.

  Polisi na Serikali vimeshindwa kuelewa kwamba, tangu majanga ya moto yateketeze Soko Kuu na masoko ya Mwanjelwa na Sido jijini humo katika vipindi tofauti, Wamachinga na wafanyabiashara wadogo wengi wamekuwa wakihangaika kutafuta sehemu za kufanyia biashara pasipo mafanikio. Haikuwa busara hata kidogo kuwatimua katika mitaa ya Jiji bila kuwatafutia sehemu nyingine stahiki.

  Tunampongeza Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi kwa kuacha kikao cha Bunge mjini Dodoma na kwenda mjini Mbeya na kufanikiwa kuzima vurugu hizo. Hili ni somo jingine kwa viongozi wa Serikali na vyombo vyake vya ulinzi na usalama kuwa, wananchi wanahitaji kiongozi anayewasikiliza na kutafuta suluhisho la matatizo yao, kwa maana kwamba migogoro kamwe haitazimwa kwa mitutu ya bunduki.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Nov 15, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Dalili moja kubwa ya kwanza kuoneysha kuwa serikali iko out of step na raia wake ni pale serikali hiyo inapokuwa inatumia nguzu za kuua mara kwa mara dhidi ya raia wake inaotakiwa kuwaongoza. Miaka ya hivi karibuni, serikali ya Tanzania imakuwa na matumizi ysiyokuwa na mwisho dhidi ya raia: Chuo Kikuu Dar, Arusha, Iringa, Mbeya, Mwanza, Dodoma. nadhani hizi ni dalili za serikali kushindwa jukumu lake la kuongoza. Haiwezekani kila mara iwe ni wapinzani wanazoa raia wote wale hadi serikali itumie mabomu. Iwapo serikali ingekuwa inaongoza vizuri raia wake, basi wapinazani wasingepata wafuasi wa kiasi cha kusababisha matumizi ya mabomu.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Nov 15, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,915
  Likes Received: 83,387
  Trophy Points: 280
  Halafu mimi kinachoudhi zaidi ni Kikwete na Pinda kukaa kimya kabisa kama vile hakuna baya lolote lile lilitokea nchini au kutoa kauli ya kuhakikisha kwamba malalamiko mbali mbali ya Watanzania kila kona ya nchi yetu yanasikilizwa badala ya kuamua kupiga tu mabomu na risasi hovyo hovyo na hatimaye kuleta maafa.
   
 4. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #4
  Nov 15, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Tuiombee nchi yetu chini ya uongozi tulio nao. Uongozi hautupeleki pazuri; unafanya raia waichukia nchi na serikali yake, jambo ambalo ni la hatari sana. Imani yangu ni kuwa kama serikali haitajiangalia vizuri kuhus migogoro yake na wanachi, basi itafikia siku moja tuna jeshi la polisi upande mmoja na rfaia upande wa pili kwa nchi nzima. Mwanzo wa ngoma ni lele.
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Nov 15, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,915
  Likes Received: 83,387
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kichuguu, mimi siku hizi hata kuwaita "viongozi" naona ni kichefu chefu tu maana sioni chochote kile wanachoongoza zaidi ya kuiangamiza nchi yetu na hata kuhatarisha amani katika siku za usoni kutokana na jinsi wanavyokurupuka na maamuzi yao mbali mbali ambayo hayaungwi mkono na Watanzania walio wengi. Kama unavyosema ni kweli kabisa mie sitashangaa kabisa kabla ya mwisho wa mwaka huu au 2012 kusikia Watanzania wameua polisi au FFU kutokana na manyanyaso makubwa wanayoyapata toka kwa vyombo hivi vya dola, labda hili likitokea ndio Kikwete na Pinda wataelewa kwamba Watanzania tumechoshwa na manyanyaso yasiyokwisha.
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Nov 15, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nchi ina Ombwe la uongozi!
   
 7. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #7
  Nov 15, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,659
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Asiyesikia la mkuu.................. Mwalimu alionya kuwa mtu yeyote anayeitafuta ikulu kwa njia ya kuhonga aogopwe kama ukoma, JK alitumia mabilioni ya EPA kuingia pale magogoni, matokeo yake ndiyo haya.Huyu JK hakuwa na ajenda ya kuongoza taifa hili bali alichotafuta ni utukufu ambao tayari ameshaupata hivyo hana lingine la kufanya zaidi ya kula bata kwa kwenda mbele mpaka amalize muda wake. Hili ni fundisho kwa wabongo watu wa jinsi ya JK wasipewe nafasi tena ya uongozi.
   
 8. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #8
  Nov 15, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Itabidi policcm waue sana raia ili wawezeshe chama cha muauaji kuendelea kubaki madarakani.
   
 9. brightrich

  brightrich Senior Member

  #9
  Nov 15, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Sikio la kufa halisikii dawa, Nyerere alisema ukiona mtu anakimbilia kuingia Ikulu ni "Mwendawazimu" Ikulu sio mahali pa kukimbilia, leo jiulize JK hadi kuchakachua kura wakati watanzania tunajua kuwa aliyeshinda urais 2010 alikuwa ni Dr. Slaa ni nini? Leo kila mahali ni mabomu, wanafunzi wa Makumira University wamekaa barabarani kusisitiza Tanroads waweke Bumps kubwa kwa ajili ya kuepusha vifo vya wanafunzi wenzao, polisi kuja tu kukuta mkusanyiko wa wanafunzi wao wakaanza kurusha mabomu na risasi! WHY!!? Mbeya wamachinga wanajitafutia riziki yao wanahamishwa hawana pa kumbilia tayari mabomu na risasi, nini hatma!? Yote haya mwisho ni lini?
   
 10. Malipesa

  Malipesa JF-Expert Member

  #10
  Nov 15, 2011
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 310
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Dalili ya mvua ni mawingu, mvua ikinyesha mawingu hayaonekani tena kwa maana ya kwamba zile dalili zimeshaleta matokeo. Kwa kinachotokea TZ sio dalili tena kwani wakati wa dalili umeshapita sasa hv ni matokeo, hapa ni kwamba serikai imeprove failure.
   
Loading...