Matumizi ya M- Kwenye Auto - Manual Cars. Wengi wanashindwa kufahamu watumie nini na wakati gani?

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,355
11,499
Kwenye hizi gari ndogo za Mjapan ambazo nmefanikiwa kumiliki nimekuwa nikipenda kuwa na Gari ambazo ni Auto Manual- Binafsi mimi ni mpenzi sana wa Gari Manual. Ingawa kwa hizi ndogo ni nadra sana kuzipata Manual. kwa hizi ndogo nimekuwa na Toyota Harrier, Toyota Crown, Toyota Rumion na Toyota Prado. Hizi gari zimekuwa na mfumo wa gears ambao ni Auto na pia hapo hapo unakuta kuna Manual imeandikwa M/S kwa gari mbalimbali. M ikiwa na maan ya Manual na S maana ya Sports.

Nimeona kwenye gari toyota Rumion ikiwa kwenye M- inakuwa na gears zipatazo 7 kwa maelezo toka kwa watengenezaji. na ikiwa kwenye Normal Auto zinakuwa 5. labda hili wataalamu waje waelezee. mimi ninayo Rumion moja ambayo inanisaidia kwa mizunguko ya Town. Nimependa sababu ni nzito, inatulia barabarani na mwendo upo. lakini sijaweza tumia gears zote hizo kama ambavyo nimeelezewa. Nilitamani watu wenye uelewa nazo watoe darasa la kutosha. maana pia kwenye Toyota Crown nimeona na sijawahi tumia kabisa kitu ambacho kinanitamanisha niweze jua.

Mara nyingi napoenda safari za mikoani hutumia gari kubwa ambayo ni manual. so hizi sijajua zinakuaje kutokana na melezo ya watengenezaji. jambo lingine ambalo labda wataalamu au wenye uzoefu wataotole ufafanuzi ni kuwa gari nyingi tumezoea zinakuwa na gear P,R,N,D,1,2,L au tofauti kidogo.

Lakini nina gari ya mwaka 2014 yenyewe ina P,R,N,D halafu M ambako utakuta + na - hakuna 1,2 au L. je inapotakiwa kutumia low mfano kwenye Mlima Mkali au Mtereko Mkali inakuaje? Au unapotaka vuta gari nyingine. au unapokuwa kwenye barabara inayoteleza? nliwaza hilo nikafikiri au ndo badala yake unatumia Manual gear no1 au 2?

Tupeane uzoefu please katika hili.
 
Tukianza na PRND2L iko hivi; kazi ya 2 na L ni kuilock gearbox isibadili gia zaidi ya hapo, kwa mfano ukiiweka kwenye 2 itakuwa inatembelea gear # 1 na 2 tu haitozidi hapo, na ukiweka L itakuwa inatembelea gear #1 tu. Hapo natumai ushaelewa sasa ukitaka kuvuta gari nyingine au ukiwa mlimani ufanyeje ukiwa na auto ya mfumo huo.

Kwenye PRND ukikuta gari mfumo wake wa gear uko hivi lazima iwe na hiyo option ya
-/+ ili utakapotaka kuilock kwenye gear flani utumie huo mfumo.
 
Nikiwekqga S mode sipati matokeo yoyote zaidi ya mafuta kuisha haraka na gari kuvuma mno inatoa mlio kama alteza.
 
Mfano mimi iko hivi hizi zina kazi gani nisije haribu mambo maana😀😀

62641c91-023a-4782-9216-92d0037430e3.jpeg
 
Mfano mimi iko hivi hizi zina kazi gani nisije haribu mambo maana😀😀

View attachment 2781030
Hapo kuna drive "D" na sport mode "S" na hiyo "B" ni break (hii inatumika kama unapanda mlima mkali pia hata kama unashuka mteremko mkali unatumia )
Sport mode "S" inaifanya gari kuchanganya mapema na Ile RPM itapanda zaidi juu huku gari ikifikia speed kubwa zaidi Kwa sekinde chache
 
Nikiwekqga S mode sipati matokeo yoyote zaidi ya mafuta kuisha haraka na gari kuvuma mno inatoa mlio kama alteza.
Matokeo mazuri utayapata kama gari yako ina M +/- hapa gear box inakuwa kwenye mfumo wa manual na mara nyingi gari za namna hii zinakuwa na 6 speed transmission na kuendelea
 
Back
Top Bottom