Matumizi ya Kiswahili na Kiingereza

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
1,606
Nikisoma baadhi ya maandishi katika jengo hili ninaona tunachanganya Kiswahili na Kiingereza.
Bila ya nia ya kukebehi bali kwa heshima zote, naomba tujadili ni zipi katika sababu hizi zinazotufanya kutumia lugha zote mbili:
1. Hatujui Kiswahili hivyo tunaziba pengo kwa kutuma Kiingereza?
2. Hatujui Kiingereza hivyo tunaziba pengo kwa kutumia Kiswahili?
3. Kiswahili hakijitoshelezi hivyo tunaposhindwa kupata neno sahihi tunakimbilia Kiingereza?
4. Hatuzifahamu lugha zote mbili?

Naomba kuwasilisha.
 
Jengo lipi ilo, linalo kushangaza... MAMMAMIA!?
 
X-Paster, nilikusudia katika ukumbi huu wa JF - The Home of Great Thinkers.
 
Labda kwa sababu lugha zote ni za taifa.

Nadhani jibu ni namba 3 & 4.
.
smile1.jpg
 
Nikisoma baadhi ya maandishi katika jengo hili ninaona tunachanganya Kiswahili na Kiingereza.
Bila ya nia ya kukebehi bali kwa heshima zote, naomba tujadili ni zipi katika sababu hizi zinazotufanya kutumia lugha zote mbili:
1. Hatujui Kiswahili hivyo tunaziba pengo kwa kutuma Kiingereza?
2. Hatujui Kiingereza hivyo tunaziba pengo kwa kutumia Kiswahili?
3. Kiswahili hakijitoshelezi hivyo tunaposhindwa kupata neno sahihi tunakimbilia Kiingereza?
4. Hatuzifahamu lugha zote mbili?

Naomba kuwasilisha.

As long as you don't break any law your are free to use any language as you like!
 
Nikisoma baadhi ya maandishi katika jengo hili ninaona tunachanganya Kiswahili na Kiingereza.
Bila ya nia ya kukebehi bali kwa heshima zote, naomba tujadili ni zipi katika sababu hizi zinazotufanya kutumia lugha zote mbili:
1. Hatujui Kiswahili hivyo tunaziba pengo kwa kutuma Kiingereza?
2. Hatujui Kiingereza hivyo tunaziba pengo kwa kutumia Kiswahili?
3. Kiswahili hakijitoshelezi hivyo tunaposhindwa kupata neno sahihi tunakimbilia Kiingereza?
4. Hatuzifahamu lugha zote mbili?
Naomba kuwasilisha.

Majibu:
1) Hapana, lakini kila lugha ina mapengo na kupokea maneno ya nje.
2) Ndiyo, angalau TZ hakika.
3) Ndiyo, kila lugha imeona ikienda nje ya kijiji chake kuna mambo ya dhana mpya zinazifika kwa umbo la lugha ya nje kwa hiyo ni rahisi zaidi kutaja kile kitu kipya kwa neno la kigeni moja kwa moja.
4) Inategemea nasi.

Usiwe nawasiwasi: lugha bora ya kupokea maneno ya nje ni Kiingereza. Msingi wa Kigermanik, maneno mengi kutoka Kifaransa cha kale, halafu maneno ya kitaalamu kutoka Kilatini na Kigiriki, halafu mengine kutoka lugha za koloni zao.
Tatizo wapi??
 
Ninakubaliana kabisa na sababu hizi kwa sababu lugha zote ulimwenguni zinapokea maneno kutoka lugha nyengine, na mara nyingi hili ndilo linalozidisha utajiri wa lugha. Lakini nilichokusudia hapa ni kuchanganya lugha mbili ndani ya andiko moja.

Nimechomoa mfano katika moja ya maandiko hayo humu ambalo ndilo lilikuwa chimbuko la hoja yangu:

Kilichonifanya nijiulize je what makes Zitto na JK kuwa marafiki? Je Zitto na JK walikuwa wanajuana kabla ya JK kuwa rais? Definitely Yes!
Je swali gumu na baya ambalo halina ushahidi ni je Zitto kuwa inclined kwa JK, Salim na kuwapenda baadhi ya viongozi wa kiislam je ni mdini?..........I mean chunguzeni hili. May be not! Kindly don't conclude! What Salim teaches Zito?? Salim is CCM, is Salim and JK close friends? Cause Ommy and Zitto are close friends, Ooh! Ommy ni personal assistant wa Salim, Nauliza Kama Ridh, Zitto, Ommy ni marafiki then Salim and JK ni maadui? Find out please. However, we all know JK ni mdini, maana alianza harakati za udini tangu akiwa UDSM miaka hiyo….na hili fuatilieni....

Ukiangalia andiko hili, huwezi kujuwa mara moja mwandishi alikusudia kuandika katika lugha gani. Kwa mawazo yangu, hali kama hii inauwa Kiswahili kuliko kukikuza, lakini kama mchangiaji mmoja alivyosema hapa, "Almradi tu huvunji sheria, kila mtu ana haki ya kuzungumza/kuandika anavyotaka.
 
Ukiona hivyo huyo mwandishi si mweledi wa lugha zote mbili!
 
Katika mfano wako ni wazi anachanganya lugha zote mbili. Hapa Kiingereza chake ni hafifu sana (kisarufi). Naona kwa kawaida ni nia ya mwandishi kuonyesha yeye ni mtu wa takaba ya juu anaweza Kiingereza. Ambayo katika staili hii inachekesha kidogo ukiona sarufi yake ya Kiingereza. Hapa tungeweza kuorodhesha wachangiaji wengi sana wa JF (sitaji majina).

Ila hata hii ni kawaida katika historia ya lugha nyingi. Ukisoma maandiko katika lugha za Ulaya karne ya 18 na 19 utakuta jinsi walivyochanganya lugha yao na Kilatini au baadaye pia Kifaransa na lugha yao. Sawa kama mfano wako. Haya yatapita, heri kuvumilia, kucheka kidogo, kutunza uwezo wa kuandika na kusema lugha safi na mara chache kuonyesha kiboko tukimpata mtu anayepiga makelele mno kwa kuonyesha Kiingereza chake kibaya.
 
Ugumu wa kusimamia lugha ya kiingereza kama lugha ya kufundishia ni kwamba viongozi wamekuwa na unafiki pamoja na wanasiasa.
Viongozi na wanasiasa wao wanaigiza kama vile wanapenda lugha ya kiswahili itumike hadi chuo kikuu,huku wao wakiwapeleka watoto wao shule zenye kufudisha masomo yote kwa kiingereza.
Sasa athari za unafiki wa wasimamizi wa mfumo wa elimu tunaendeleo kuona.
Kada za kitaaluma mfano sheria,udaktari na viongozi kuwa na kiingereza dhaifu.
Yaani,ukitafakari sana mbele ya safari tunatengeneza Taifa la wajinga wengi(division zero zinazidi kuongezeka miongoni mwa wahitimu wa shule zetu).
Dalili za kutawaliwa na wajanja wa dunia hii ni dhahiri.
 
Lugha rasmi za tanzania ni Kiswahili na Kiingeleza.
Kama mambo yangekuwa mazuri na elimu bora kabisa basi kila mtanzania angekuwa na uwezo wa kuongea KIINGELEZA bila kuchanganya 100% na Kiswahili 100% bila kuchanganya.

Kiukweli hatujui kuongea kiswahili 100% na kiingeleza 100%. Jitihada za kufikisha ujumbe kwa Lugha hizi halali kabisa kwa mtanzania hupelekea muandishi au mzungumzaji kuzichanganya.

Hakuna tatizo kabisa kwa sababu zote ni lugha nzuri za kutumia na halali kwa mtanzania japo KISWAHILI kinaupungufu wa maneno na misisitizo.

nini maoni yako...
 
Nikisoma baadhi ya maandishi katika jengo hili ninaona tunachanganya Kiswahili na Kiingereza.
Bila ya nia ya kukebehi bali kwa heshima zote, naomba tujadili ni zipi katika sababu hizi zinazotufanya kutumia lugha zote mbili:
1. Hatujui Kiswahili hivyo tunaziba pengo kwa kutuma Kiingereza?
2. Hatujui Kiingereza hivyo tunaziba pengo kwa kutumia Kiswahili?
3. Kiswahili hakijitoshelezi hivyo tunaposhindwa kupata neno sahihi tunakimbilia Kiingereza?
4. Hatuzifahamu lugha zote mbili?

Naomba kuwasilisha.
Hapo hakuna hata sababu moja ya msingi inayosababisha Code swift au Code mixing (kuchanganya Kiswahili na Kiingereza).
 
Back
Top Bottom