matumizi ya hovyo ya neno pendwa 'mjanja' yanavyotutafakarisha waungwana!

NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
3,824
5,604
neno 'mjanja' ni zuri sana na wengi huwa wanatabasamu wakihusishwa nalo.

mtu akiambiwa, 'we mjanja sana' basi huwa anafurahi na kuridhika sana......na hali hiyo ipo karibu kwa binadamu wote.

hata tafsiri ya kiingereza ya neno hili ni nzuri sana, baadhi ya maneno, kama sikosei, ya kiingereza yanayomaanisha 'mjanja' ni kama yafuatayo;
clever,
smart,
artful,
wise,
bright n.k. ni nani hataki kusikia akiambiwa maneno hayo?!!!!! hakuna, bila shaka

sasa kuna hii tabia ya kuwarefer wahalifu/wezi/wahujumu uchumi/vibaka n.k kwa kutumia neno hilo pendwa. utamsikia kiongozi mkubwa tu aliyeenda kwenye mradi fulani uliohujumiwa akisema, 'fedha tulitoa ya kutosha kabisa hapa, ilikuwa milioni 800, lakini mradi haujakamilika na fedha zote zimeisha; kuna wajanja wachache wamezitafuna'! dah, huwa nasaga meno kwa maumivu nikisikia kauli kama hiyo. najiuliza , ina maana wale waaminifu na watiifu ni malofa? kwani si ndiyo kinyume cha neno mjanja au?

wadau, matumizi kama hayo ya neno hili hayahamasishi uhalifu kweli? yaani mi nikae tu ofisini nikishuhudia wenzangu wakiwa described kama wajanja kila siku........the surest indirect way ya kuniambia 'wewe lofa/bwege sana'. nahisi umefika wakati wa kuchunguza vitu vidogo pia kama hivi huenda vinachangia kutokuisha kwa uhalifu kila leo!
 
Ni kama vile kuitana boss au mkuu ilhali hamna uboss wala ukuu wowote, so hapo sion kama kuna tatizo
 
ujanja sio kwenye mema tu. hata ukipiga dili yako nyeusi, magendo na ulitumia akili nyingi bado unabaki kuwa mjanja
wajanja wote town ndio wanaongoza kupiga dili za nyeusi (wizi wizi)
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom