Matumizi ya energy ni bomu kwa Vijana Afrika

Ni kawaida VIJANA wa kileo kushindana katika kufakamia Red Bull, Monster Energy, MO Energy na vinginevyo, huku Wengine wakioneshana ubobezi wa kuchanganya Vinywaji Hivyo na Pombe.

Chombo Cha UMOJA wa ULAYA chenye Mamlaka ya kusimamia Usalama wa Chakula (European Food Safety Authority, kimebainisha kuwa Asilimia 30 ya Watu wazima hutumia Energy Drinks, Asilimia 68 Ni Watoto wa Umri wa Miaka 16-18 na Asilimia 18 ni Watoto CHINI ya Miaka 10.

Pamoja na Ongezeko la Watoto na VIJANA Wanaotumia, Tafiti zinaonesha kuwa Matumizi ya Vinywaji vya kuchochea nguvu maarufu Kama Energy Drinks, Yana athari Kubwa kwa Afya ya Mwanadamu.

Utafiti uliofanywa na Jopo Wataalam toka Shirika la Afya Ulimwenguni 'WHO,' umethibitisha kuwa vivywaji vya Energy, ambavyo ni mchanganyiko wa kichocheo Cha Caffeine, sukari, Sodium na Taurine ni Chanzo kikuu cha MATATIZO ya MOYO, Akili ikiwemo kukosa usingizi, Shinikizo la Juu la DAMU, Shambulio la MOYO, Mpapatiko wa MOYO(Heart Palpitations), sonona, Kukosa utulivu(Restlessness) na kuishiwa maji mwilini(dehydration, na vifo vya ghafla, kutokana na Shambulio la MOYO(cardiac arrest).

Kwa mujibu wa Matokeo ya Utafiti wa Chuo Kikuu cha Toronto ya Mwaka 2015, Matumizi ya Energy Drinks yaweza kupelekea Athari ya kuharibika kwa UBONGO.Brain Damage.

Hatari ya Matumizi yya Energy Drinks huongezeka Mara dufu pale vinywaji hivyo vinapochanganywa na Pombe. Kuto

Athari ya vinywaji Hivyo kwa Watoto zimepelekea Ushirikiano wa Madaktari wa Marekani(American Medical Association) kuzuia Watoto CHINI ya Miaka 18 kutumia Energy Drinks.

Dokta Stephen Nguyan MD, Palo Alto wa Taasisi ya Afya wanadai kuwa Matumizi ya vinywaji hivi si SALAMA kabisa. Wakati chupa Moja ya SODA(COKE, PEPSI) kina KIWANGO cha Caffeine cha miligramu 35, vinywa vya kuchochea nguvu maarufu Kama Energy Drinks vina Caffeine miligramu kuanzia 150 Hadi 280. Kiwango Cha juu Cha caffeine kwa MTU Mwenye kilo 70 Ni miligramu 210.

Kuhusu vifo vinavyotokana na Energy Drinks, Dalili za MWANZO Ni kifua kubana, uchovu, miguu kuvimba, kizunguzungu kikali, kuona giza la ghafla, Kukosa usingizi. Unapohisi Dalili hizo ni king'ora Cha HATARI.

Nimeshuhudia VIJANA wawili, wabobevu wa Matumizi ya Energy Drinks Wakipoteza MAISHA kwa Shambulio la MOYO. VIJANA walioshaurika na kuacha Matumizi ya vinywaji Hivyo Hadi Sasa wako hai.

Je, tunapoteza nguvu KAZI kiasi gani kutokana na JINAMIZI HILI? Je, tutakwepaje HATIA ya kukitoa KAFARA kizazi chetu kwa kigezo feki Cha Kulinda UCHUMI?

VIJANA wa Bara la AFRIKA wapaswa kulitegua BOMU hili HATARI kwa kwa kupaaza SAUTI Ili Nchi zao ziwe na SERA za Kulinda USALAMA WA WATU WAO. Katika hili Tanzania yapaswa kuongoza usukani.
Asante sana Mkuu Mshana. Ubarikiwe kwa jitihada zako hizi za kuielimisha Jamii. Shida ninayoiona hapa ni Je, Vijana e.g waliomo humu Jf. wataisoma Habari hii njema? au watakimbilia kusoma nyuzi za kula tunda....n.k... 😟??
 
Asante sana Mkuu Mshana. Ubarikiwe kwa jitihada zako hizi za kuielimisha Jamii. Shida ninayoiona hapa ni Je, Vijana e.g waliomo humu Jf. wataisoma Habari hii njema? au watakimbilia kusoma nyuzi za kula tunda....n.k... ??
Asante mkuu Kirumberumbe uzuri wa maandishi ni kuwa hayafutiki mtu asiposoma leo basi kuna siku atasoma tuu.. Anaweza akapotezea mara moja au mbili lakini ya tatu atasoma na kutafakari.. Na kamwe hakuna neno jema linaloenda bure
 
Mshana wanasema hizi za mo extra haziko kwenye category ya energy drink. Hebu tuekee content zake hapa tuone caffeine ipo kwa kiasi gani.
Ati ni carbonated soft drink.
 
Mshana wanasema hizi za mo extra haziko kwenye category ya energy drink. Hebu tuekee content zake hapa tuone caffeine ipo kwa kiasi gani.
Ati ni carbonated soft drink.
Mmh nipe muda nisijibu kwa kubahatisha
 
Mi nilikuwa nakunywa kila siku asubuhi nilikonda mpaka kuna mtu aliniona nazinywa akaniambia zitaniua harafu nilikuwa siwezi kuzuia mkojo kwa muda mrefu energy sio kabisa
 
Mi nilikuwa nakunywa kila siku asubuhi nilikonda mpaka kuna mtu aliniona nazinywa akaniambia zitaniua harafu nilikuwa siwezi kuzuia mkojo kwa muda mrefu energy sio kabisa
Aisee la kuzuia mkojo Kwa mda mrefu namimi limekuwa likinitokea, lakini saizi naona limepungua baada ya kuacha kutumia energy, lakini sikujua kama zinasababisha tatizo hilo!!

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Ngoja nipoze koo kwanza ,kuhusu kufa kila mtu atakufa tu
20220616_184648.jpg
 
Mshana wanasema hizi za mo extra haziko kwenye category ya energy drink. Hebu tuekee content zake hapa tuone caffeine ipo kwa kiasi gani.
Ati ni carbonated soft drink.
Yah, ile ni Mo Extra sio energy. Pia haijaandikwa kuwa usinywe zaidi ya mbili kwa siku kama ilivyo kwa Azam energy. Na binafsi nikitumia usingizi napata tofauti na energy drinks nyingine. Ila still sio nzuri kwa afya haifai kunywa.
 
Back
Top Bottom