Matumizi ya Dola ya Marekani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matumizi ya Dola ya Marekani

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mwalimu, Jan 16, 2009.

 1. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #1
  Jan 16, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Ndugu zangu naomba kuuliza kuhusu noti za dola ya marekani za miaka chini ya 2000;

  1)Serikali/BOT wamewahi kutoa tamko lolote kuhusu matumizi ya noti za dola ya marekani zenye miaka chini ya 2000 kwamba haziruhusiwi kutumika nchini?

  2)Huko jikoni kwenyewe (USA) noti hizi za miaka chini ya 2000 zimepigwwa marufuku kutumika?
   
 2. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #2
  Jan 16, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,288
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Kwa uelewa wangu, nitajibu swali la pili. Noti zilizochapwa chini ya mwaka 2000 bado zinaendelea kutumika USA na sehemu mbalimbali duniani. Ila tatizo la noti hizi ni kwamba security feature zake ni dhaifu na zinaweza kugushika kiurahisi. Benki mbali mbali za Africa ambazo bado hazina mitambo ya kisasa ya kutofautisha noti bandia na halali zimekuwa zikikwepa kupokea noti hizi, lakini noti hizi ukizipeleka nchi kama USA na Canada zinapokelewa bila chembe ya kikwazo. Benki nyingi za USA na Canada zinatambua ugumu wa matumizi ya noti za chini ya mwaka 2000 katika nchi za Africa.
   
Loading...