Matumizi ya Dola ya Marekani kwenye Manunuzi yachanganya Wananchi

FikraPevu

JF-Expert Member
Jan 2, 2010
303
236
Dola-ya-Marekani-660x350.jpg

KILIO cha muda mrefu kutoka kwa wananchi kutaka Serikali iilinde shilingi ya Tanzania kwenye shughuli za kibiashara dhidi ya Dola ya Marekani ambayo imekuwa ikipendelewa zaidi kwa malipo ya biashara na huduma katika maeneo mbalimbali nchini, bado hakijatatuliwa na hivyo kusababisha shilingi kuporomoka mara kwa mara, FikraPevuimeelezwa.

Serikali kwa miaka kadhaa imekuwa ikiahidi kuwa itachukua hatua za kudhibiti matumizi ya dola ili kulinda hali hiyo, lakini hadi sasa haijatekeleza ahadi hiyo.

Katika kipindi cha miaka kumi na moja iliyopita nchini, shilingi ya Tanzania ilianza kupotea thamani yake kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kukithiri kwa matumizi ya fedha za kigeni hususani Dola ya Marekani.

Matumizi ya Dola yashamiri

Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wameeleza kuwa kumekuwepo na ongezeko kubwa la matumizi ya fedha za kigeni nchini hususani kwenye taasisi za watu binafsi zikiwemo shule za awali na sekondari.

Aidha, licha ya biashara ya fedha za kigeni kuendelea kukua katika miji mikubwa pamoja na miji iliyopo mipakani wananchi wengi wamelalamikia hatua ya kufika kupata huduma kwenye maeneo mbalimbali nchini na kudaiwa kuwa wanatakiwa kufanya malipo.....

Habari zaidi soma,=>Matumizi ya Dola ya Marekani kwenye Manunuzi yachanganya Wananchi

hii thread ina maana sana lakini tumuombe Dr. JPM atoe tamko kali juu ya hili kwa mfano huduma za usafiri wa anga zina umiza sana. Nauli zote zipo katika mfumo wa dola na kupelekea ongezeko kubwa katika sh. Hvyo kuwafanya watanzania kuwa watumwa katika nchi yao. Hivyo basi mh. Katika hili kweli tuna umia. Unakuta smart phone ulaya ni dola 200 bongo dola 600 hadi 800. Sasa uki turn into sh. Hatari sana hv ni kwa nin jaman
 
Mkuu,
Wahujumu Uchumi wanaiita hiyo "Soko Huria". Ila mwisho ndio umewadia.
 
Nilishuhudia mteja mmoja wa kigeni anataka kuingia hifadhi ya Taifa hapa kwetu Tanzania akwaambiwa wadau kuwa yeye alichenchi dola zake nyingi kwahiyo akimaanisha kuwa Tanzania watazipokea lakini chakushangaza wakamwambia hawahitaji Shilingi bali dola jamaa akawauliza iweje hela ni za kwenu halafu hamuzihitaji?:shock:
 
mengine yote uliyoandika sawa lakini hilo la smart phone acha kudanganya watu. ulichoandika ni uongo mtupu kwenye hilo na kama hujui ni bora ungeuliza ueleweshwe.

Back
Top Bottom