Matumizi ya dawa za kuzuia mimba kwenye vipodozi

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
26,574
48,725
wanawake sisi sometimes tunajipenda utadhani hatutakufa.jana nilikuwa na shosti wangu mmoja hivi sehemu .huyu shosti tumetoka kijiji kimoja kwa hyo gene zake nazijua kabisa .

Ila mwenzangu ana nywele siku hizi balaa kama mzungu vile mimi mwenzake baado nahangaika na kipilipili changu kama mavi ya mbuzi vile. shukrani kwa mchina na mawigi yake hata tunaonekana mjini sometimes.

Basi bwana nikamuuliza shosti mi nimeshatumia madawa yote anzia sazuu ,revlon,beautiful beggining ya box ya chupa ,mega ,olive ,black jamaika ila kipilipili hakiongezeki kinapukutika tu naishia kila siku kunyoa na kuanza upya .

Natunza nywele weee nikipiga hesabu ambayo ishaenda kichwani ningejenga hata barabara moja ya mwendokasi .Akaniambia miss natafuta mama nikupe siri mimi kichwani napaka dawa za majira ndo unaniona nywele zipo hivi .

So nikamuuliza unapakaje akanipa formula jinsi wanavochanganya madawa hayo kwenye mafuta au dawa za nywele .
kwa hiyo wanawake kuweki makini hayo madawa mnayouziwa huko instagram ya kukuza nywele hayana manufacture name wala adress watu wanachanganya tu mavidonge ya uzazi .na ndo maana matatizo ya uzazi ni mengi
 
Miss bado unatafuta au ushampata?tuanzie hapo kwanza.then tuambie huyo ni wewe kwenye avatar
 
Niliwasikia wanabadilishana notes kuwa dawa za eczema ni nzuri sana kwa kulainisha ngozi, mmoja akasema yeye ameambiwa anayo na daktari anamwandikia dawa, mwenzake akamwambia basi ukipewa prescription yako niletee umwambie daktari imepotea. Dawa zenyewe ni steroids ambazo hutakiwi kutumia muda mrefu.
 
Niliwasikia wanabadilishana notes kuwa dawa za eczema ni nzuri sana kwa kulainisha ngozi, mmoja akasema yeye ameambiwa anayo na daktari anamwandikia, mwenzake akamwambia basi ukipewa prescription yako niletee umwambie daktari imepotea. Dawa zenyewe ni steroids ambazo hutakiwi kutumia muda mrefu.
mmhmhmh wanawake mna mamboooo... urembo tu jaman ili kuvutia wanaume. duuuuuu!!!!!
 
Niliwasikia wanabadilishana notes kuwa dawa za eczema ni nzuri sana kwa kulainisha ngozi, mmoja akasema yeye ameambiwa anayo na daktari anamwandikia dawa, mwenzake akamwambia basi ukipewa prescription yako niletee umwambie daktari imepotea. Dawa zenyewe ni steroids ambazo hutakiwi kutumia muda mrefu.
eczema ni dawa ya nini mamy dr?
 
Back
Top Bottom