Matumizi ya Dawa za Kuzuia mimba kwa watoto kuanzia umri wa miaka 10 na kuendelea iwe ni sheria.

Poise

JF-Expert Member
May 31, 2016
7,633
7,907
Wana JF, naamini hapo Tanzania mpo salama poleni kwa majukumu na siasa zinazokang'anya kidogo ila ndiyo kukua kwa utashi wa wananchi ili kufanya maamuzi sahihi kila itokeapo nafasi kama hiyo.

Kama, kichwa kinavyosomeka, Matumizi ya Dawa za Kuzuia mimba kwa watoto kuanzia umri wa miaka 10 na kuendelea iwe ni sheria.

Na hata pia kutoa mimba iwe ni poa tu. Na hilo linaenda kupitishwa na Bunge la EAC.

Swali: Je, wana JF mnasemaje juu ya hali hiyo na sheria hiyo?

Je, tukubaliane na sheria hiyo?

Samahani, hii thread nilipaswa kuiweka katika doctor forum ila ina mambo ambayo ni mtambuka yaani mambo ya sheria, dini (imani) afya na jamii kwa ujumla.

Chanzo: BBC Swahili
 
Watunge na sheria ya kufanya mapenzi na watoto Wa umri huo Wa miaka 10.
 
Kwa kweli mimi naona wazungu wametufanya soko la bidhaa za hospital sasa kila kukicha wanajiuliza ni aina ipi ya dawa au kifaa cha hospital cha kutuletea aisee
 
Duh! Yaani mtoto wa Darasa la 3 anazunguka na vidonge vya kuzuia mimba?
No.

Ndiyo hivyo .

Kwa hiyo huko Tanzania , angalieni namna ya kukataa hilo jambo badala ya kukalia siasa za simba kumkaribisha swala pangoni kwake.
 
Sio nzuri itawafanya wengine baade kushindwa kupata mimba

Kabisa na kusababisha nchi kuwa na wazee pekee au kuwa na jamaii yenye matatizo ya akili.

Kwa.sababu nimesikia dawa hizo zina.matatizo mengi sana kwa.watumiaji inaweza.ikawa.ya muda mfupi au muda mrefu na hata kwa watoto wanaozaliwa.
 
HAPANA.
ni dhambi mtakuwa mnaharalisha uhuaji.

Sasa , mkuu kama wananchi watachukua hatua gani?

Kwa.sababu, namna ya kutekelezwa labda watoto watapewa wakiwa shuleni kama zilivyo chanjo zingine na dawa za kuzuia baadhi ya mgonjwa!?
 
Watoto wafundishwe ngono kabla ya ndoa marufuku, kiafya na kidini sio jambo zuri. Wasubiri tuu muda utafika. Wazazi washiriki kikamilifu kutoa elimu hiyo, waache kuwa busy na mambo yao.
 
Baadae watoto wenu wakishindwa kuzaa muanze kuhangaika kwa waganga muambiwe mmerigwa na jirani...pumbavu zenu
 
Athali za Vidonge vya kuzuia mimba zinafichwa sana na haziwekwi wazi.

Haya madude sio mazuri kwa wake zetu halafu wewe unasema waanze kutumia wakiwa na miaka 10?
 
Ndiyo hivyo .

Kwa hiyo huko Tanzania , angalieni namna ya kukataa hilo jambo badala ya kukalia siasa za simba kumkaribisha swala pangoni kwake.
Tutashtuka baadaye.. Sasa hizi Watanzania 50M wanamjadili mtu 1 kwanza. Smh.
Ahsante kwa ushauri though.
 
Maana yake ni kuhalalisha ngono kwa umri mdogo.
Tuizuie kulinda vijana wetu maana hatuna wataalamu was kupima madhara ya hayo madawa. Itafikia watoto wetu wasiweze kuzaa tena. Don't play with west
 
Athali za Vidonge vya kuzuia mimba zinafichwa sana na haziwekwi wazi.

Haya madude sio mazuri kwa wake zetu halafu wewe unasema waanze kutumia wakiwa na miaka 10?

Mkuu, siyo Mimi niliyesema.

Ni sheria inatakiwa kupitishwa na bunge letu la nchi za jumuiya ya afrika ya mashariki ( EAC) ili mabinti wa miaka 10 na kuendelea watumie .

Saa.mimi nilipopata hizo habari nikaweka hapa ili watu mjue na pia mchukue hatua kuponya watoto wa kike huko Tanzania
 
Sasa , mkuu kama wananchi watachukua hatua gani?
Kwa.sababu, namna ya kutekelezwa labda watoto watapewa wakiwa shuleni kama zilivyo chanjo zingine na dawa za kuzuia baadhi ya mgonjwa!?
JIBU LAKO HILI HAPA:
Watoto wafundishwe ngono kabla ya ndoa marufuku, kiafya na kidini sio jambo zuri. Wasubiri tuu muda utafika. Wazazi washiriki kikamilifu kutoa elimu hiyo, waache kuwa busy na mambo yao.
 
Back
Top Bottom