Matumizi ya Cruise Control kwenye gari

Hii button wengi wanaiona ila hawajui kazi yake au jinsi ya kuitumia.
Kazi yake ni kushikilia mwendo usibadilike.

Yaani ukiwa 60kph ukiibonyeza mwendo unasimamia 60kph bila wewe kukanyaga mafuta kwahio unapumzika kiaina. Ni nzuri Sana masafa marefu.

Inafanyake kazi?
Kwenye picha hapo chini kuna ON na OFF,kuna RESUME,SET. Unaweka ON unaendesha Hadi speed uitakayo halafu unabonyeza SET inakuwa active na mwendo haubadiliki.

Kukiwa na muinuko utasikia engine inaongeza nguvu ku maintain speed,kukiwa na mteremko utasikia engine inapunguza nguvu ku maintain speed as well.

Iwapo kitatokea kitu ukakanyaga brake CC inakuwa DEACTIVATED ili uendelee nayo unabonyeza RESUME na gari itajiongeza yenyewe Hadi speed uliotega awali.

Kuna alama +/- hizi unatumia kuongeza na kupunguza mwendo wakati CC iko ACTIVE. KAMA ulikuwa 60kph na unataka 70kph unabonyeza + kama unataka 50kph unabonyeza -

Tuendelee kujifunza.View attachment 1081511View attachment 1081512
Kaka R uyu mnyama wa 260 ni nani...
Mana gari tulizozoea hazina hio Cruise Control
 
97 MB mjomba.

Ungeweza kuicompress kwanza kabla ya uploading.

Simple trick next time. Mtumie mtu whatsapp hiyo video. App ya whatsapp itaicompress. Kisha nenda kwenye whatsapp videos, upload it to JF from there.

Hii hapa compressed by WhatsApp to 8MB

 
Tahadhari; usitumie cruise control kwenye barabara inayoteleza. Kwa mfano wakati wa mvua usitumie cruise control hata siku moja kusudi tusije tukakuokota wewe na gari lako kutoka mtaloni.
 
Mkuu maelezo mazuri,mimi swali langu lipo nje ya mada kidogo. Je umewahi kumaliza kisahani kwenye hiyo gari ? maana naona inapiga mpaka 260km/h/

Kwenye magari ya kimarekani spidi hiyo unaifikisha kirahisi tu ukiwa kwenye highway kwani ni kama 150mph ambazo zinafikika sana. Ila kwa vile sehemu nyingi kuna spidi limit za kuazia 60MPH hadi 85mph utabanwa usiifikie, ila ukitaka wewe nenda Montana ambako utapiga mpaka 150mph bila matatizo kabisa
 
Kaka R uyu mnyama wa 260 ni nani...
Mana gari tulizozoea hazina hio Cruise Control

Haya Ndio matatizo ya kuzoea magari ya toyota/nissan/mazda(japan specifications) ndio maana tunaishia tu kuona 180km/h.

Na tunaendesha magari ya mjapan ya kizamani sana na ndio maana cruise control ni changamoto.

Bmw/audi/mercedes C/control ziko kitamboo tu kama standards wkt Mjapan alipointroduce Cruise control akafanya kwny gari zake(full options)/flagship cars.

Tutafuteni hela tu wakuu.
 
Haya Ndio matatizo ya kuzoea magari ya toyota/nissan/mazda(japan specifications) ndio maana tunaishia tu kuona 180km/h.

Na tunaendesha magari ya mjapan ya kizamani sana na ndio maana cruise control ni changamoto.

Bmw/audi/mercedes C/control ziko kitamboo tu kama standards wkt Mjapan alipointroduce Cruise control akafanya kwny gari zake(full options)/flagship cars.

Tutafuteni hela tu wakuu.
Ss mda wote tuko kwenye foleni
Kusafiri nje ya mkoa mara chache
Hio 260 naihitaji ili niitumie wapi?.
 
Kwenye Lexus GS toka wayback hio kitu ipo! Kwa Toyota labda zile highend models
nina lexus gs300 inafanya vzuri lakin kama ni speed kubwa unaitesa injini inalia had bas mliman. traction iwe nzuri la tairi kama vile zinataka kuzungukiana.
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom