Matumizi ya Cruise Control kwenye gari

Gari za kijapani zipo nying tu, crown models, rav 4 miss Tanzania model, vanguard, corolla new model fortuner second and third models etc, kiufupi kama unatumia gari ya toyota au mjapani yeyote aliyekuzidi umri hiyo kitu sahau
Haina jinsi mkuu acha tuendeshe hizohizo za mwaka 47
 
hv vigari vyetu vingine sijui hicho kitu kiko wapi...niko huku nyuma kwenye boot natafuta maana ndani kwenye staring pale mi sioni kitu asee..

hii mishipa tunayouziwa engine hiiii ...Baba tusaidie waja wako maana gari zote nazonunua hata kama zina hiyo kitu huwa zinanifikiaga zikiwa zishang'olewa yani Gia tu ndo inafanya kazi..Dashboard enyewe haisomi kitu mshale umelala doloooooo ka teja muda wote yani.

Maombi yanahitajika.
 
Hii button wengi wanaiona ila hawajui kazi yake au jinsi ya kuitumia.
Kazi yake ni kushikilia mwendo usibadilike.

Yaani ukiwa 60kph ukiibonyeza mwendo unasimamia 60kph bila wewe kukanyaga mafuta kwahio unapumzika kiaina. Ni nzuri Sana masafa marefu.

Inafanyake kazi?
Kwenye picha hapo chini kuna ON na OFF,kuna RESUME,SET. Unaweka ON unaendesha Hadi speed uitakayo halafu unabonyeza SET inakuwa active na mwendo haubadiliki.

Kukiwa na muinuko utasikia engine inaongeza nguvu ku maintain speed,kukiwa na mteremko utasikia engine inapunguza nguvu ku maintain speed as well.

Iwapo kitatokea kitu ukakanyaga brake CC inakuwa DEACTIVATED ili uendelee nayo unabonyeza RESUME na gari itajiongeza yenyewe Hadi speed uliotega awali.

Kuna alama +/- hizi unatumia kuongeza na kupunguza mwendo wakati CC iko ACTIVE. KAMA ulikuwa 60kph na unataka 70kph unabonyeza + kama unataka 50kph unabonyeza -

Tuendelee kujifunza.View attachment 1081511View attachment 1081512
VW?? Swali! Jinsi gani unaweza kuchagua aina ya display ( zile nyekundu) unazotaka kuona kwani wakati mwingine inaonyesha speed, au kms za kwenda kwa mafuta yaliyopo, au average speed, au fuel consumption kwa km/litre, au muda ulioendesha gari etc. Nataka nichague mwenyewe information ninayotaka kuona badala ya zenyewe kujibadilisha.
 
Nitapost video. Nikumbushe.
 
Attachments

  • VID_20190811_172402.mp4
    97.6 MB
Back
Top Bottom