Matumizi ya Cruise Control kwenye gari

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
51,719
107,771
Hii button wengi wanaiona ila hawajui kazi yake au jinsi ya kuitumia.
Kazi yake ni kushikilia mwendo usibadilike.

Yaani ukiwa 60kph ukiibonyeza mwendo unasimamia 60kph bila wewe kukanyaga mafuta kwahio unapumzika kiaina. Ni nzuri Sana masafa marefu.

Inafanyake kazi?
Kwenye picha hapo chini kuna ON na OFF,kuna RESUME,SET. Unaweka ON unaendesha Hadi speed uitakayo halafu unabonyeza SET inakuwa active na mwendo haubadiliki.

Kukiwa na muinuko utasikia engine inaongeza nguvu ku maintain speed,kukiwa na mteremko utasikia engine inapunguza nguvu ku maintain speed as well.

Iwapo kitatokea kitu ukakanyaga brake CC inakuwa DEACTIVATED ili uendelee nayo unabonyeza RESUME na gari itajiongeza yenyewe Hadi speed uliotega awali.

Kuna alama +/- hizi unatumia kuongeza na kupunguza mwendo wakati CC iko ACTIVE. KAMA ulikuwa 60kph na unataka 70kph unabonyeza + kama unataka 50kph unabonyeza -

Tuendelee kujifunza.
IMG_20190426_085800.jpg
IMG_20190426_085818.jpg
 
Ndio maana nimeshangaa kuona hiyo kitu aisee kwa haya magari yetu ya kijapan tunakosa vitu vingi kumbe

Gari za kijapani zipo nying tu, crown models, rav 4 miss Tanzania model, vanguard, corolla new model fortuner second and third models etc, kiufupi kama unatumia gari ya toyota au mjapani yeyote aliyekuzidi umri hiyo kitu sahau
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom