Matumizi ya Bible App Kanisani na mitazamo hasi

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
19,639
33,414
Wakuu,

Nimeona nilete hili hapa kwa mjadala mpana. Naona kuna wachungaji, mapadre na watumishi wa Mungu mbalimbali wakiponda waamini wanaotumia Bible App kwenye ibada badala ya bible yenyewe.

Je ni mchakato wa mabadiliko ambao pengine hawajauelewa lakini nguvu ya teknolojia inawaacha nyuma?

Kuna ubaya gani mtu kutumia Bible app kwenye ibada tofauti na kutumia Bible? Binafsi naona inarahisisha sana usomaji na kufatilia ibada vizuri.

Inawezekana kanisa linahofia kushuka kwa mauzo ya kitabu hicho ambacho ndicho kinachoongoza kwa kununuliwa zaidi duniani?

Kwa mtazamo wangu, Kanisa liwekeze kwenye kuweka version zao za Bible kwenye App ili kuepusha waamini kupakua matangopori ili kupotosha maana kila mtu anajiwekea tu. Kwa mfano kupata Catholic bible swahili version kwenye app ni tatizo hivyo Wakatoliki wengi wanapakua version ya vitabu 66.

Kama matumizi ya Bible App si sahihi ni vizuri tukapigwa shule badala ya makatazo yasiyojengewa hoja vizuri na sometimes inaweza kuwa ni kushindana na wakati tu.

Naamini nitapata shule hapa ili nibadili fikra zangu juu ya matumizi ya Bible App kwenye ibada. Wahenga walisema, wakati ni ukuta! Nani alijua siku moja tutakuwa na Pope Instagram? Teknolojia ni mbaya ikitumika vibaya lakini ni kitu chema sana kikitumika vizuri.
 
Nadhani haina shida hao wachungaji wanaopinga nina wasiwasi na imani zao kama hakuna neno lililobadirika shida ipo wapi? Kama ulivyosema wajipange mfano kama catholic bible mtandaoni ni shida na kingine kizuri kwenye bible app sasa hivi hata ukiwa kazini ,safarini na n.k ni rahisi kupitia neno la Mungu
 
Sometimes wanasema wenye biblia nyanyueni juu, ambao hawana lakini wanatumia za simu nyanyueni simu zenu! Alafu kichambo kinaanzia hapo sasa
 
Teknolojia isitufanye tujisahau kiasi hicho! Simu uko nayo wiki nzima na ina hiyo app na hujawahi isoma, hiyo ya kwenda na simu kanisani sababu tuu ya app sidhani kama ni sahihi!
Simu ina vishawishi vingi sana! Beba Bible yako kwani utapungukiwa nini!
Hata makanisani simu tukakuwa nazo ila tunaziweka off tu, lakini bado sijaona ubaya wa kutumia bible app kama ni italeta matumizi mengine mabaya kanisani hili linahitaji elimu tu.
 
Fafanua mkuu labda nahitaji kueleweshwa ili nibadilike. Ndio faida ya platform kama hizi.
Labda tu nikwambie kiufupi ...maswala ya roho usiyaweke kwenye teknolojia ... ROHO na teknolojia ni tofaut teknolojia inatumiwa na ibilis kwa asilimia nyingi hvo kitu chenye roho ya MUNGU mfano biblia hakitaweza kuwa na nguvu ikiwa kikiwekwa sehem ambayo ibilisi ametawala asilimia kubwa

SIMU Inaweza beba video za ngono
simu hio hio umetumia kusema uongo
af baadae uweke biblia my friend hautaielewa

KEY POINT
Ukitaka uone kama biblia ya kwenye simu haina maana ...katika ROHO
Fanya yafuatayo
Siku ukiona mtu amepandwa pepo chukua simu yako yenye biblia ndan kisha sogea karibu yake uanze kusema ushindwe kwa jina la yesu ..na mwingine ashike biblia kama kitabu uone nani atakaekabwa shati na kupasuliwa simu
 
Hata makanisani simu tukakuwa nazo ila tunaziweka off tu, lakini bado sijaona ubaya wa kutumia bible app kama ni italeta matumizi mengine mabaya kanisani hili linahitaji elimu tu.
Ni kwa nini Bible app na sio biblia?!
Mwanao akuone unaenda kanisani bila Bible yeye utaweza mshawishi abebe Bible?!
 
Labda tu nikwambie kiufupi ...maswala ya roho usiyaweke kwenye teknolojia ... ROHO na teknolojia ni tofaut teknolojia inatumiwa na ibilis kwa asilimia nyingi hvo kitu chenye roho ya MUNGU mfano biblia hakitaweza kuwa na nguvu ikiwa kikiwekwa sehem ambayo ibilisi ametawala asilimia kubwa

SIMU Inaweza beba video za ngono
simu hio hio umetumia kusema uongo
af baadae uweke biblia my friend hautaielewa

KEY POINT
Ukitaka uone kama biblia ya kwenye simu haina maana ...katika ROHO
Fanya yafuatayo
Siku ukiona mtu amepandwa pepo chukua simu yako yenye biblia ndan kisha sogea karibu yake uanze kusema ushindwe kwa jina la yesu ..na mwingine ashike biblia kama kitabu uone nani atakaekabwa shati na kupasuliwa simu
Another mistake brother. Tunampa bure shetani utukufu bila kujua. Maendeleo ya mwanadamu yanatokana na nguvu iliyo ndani yake ya uumbaji ambayo inatokana na Mungu mwenyewe ambaye sisi wanadamu ni sura na mfano wake!

Hata teknolojia ni sehemu ya kazi ya Mungu kupitia wanadamu! Leo unaweza kupima magonjwa, kutumia masaa machache kwenda sehemu yoyote duniani n.k uwepo wa ibilisi kupitia teknolojia si sababu ya teknolojia! Ibilisi yupo popote ikiwemo humo kwenye teknolojia! Tukiacha kutumia teknolojia sababu ya ibilisi basi ibilisi ameshinda!!
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom