Vitalis Msungwite
JF-Expert Member
- May 11, 2014
- 3,268
- 7,779
Haya ni maneno matatu ambayo hufanya kazi moja. Kazi kuu ya maneno haya ni kuongeza maelezo ya ziada katika jambo. Hutoa taarifa ya ziada au kukazia taarifa ya awali.
Katika jamii kuna mazoea ya kutumia maneno hayo katika sentensi moja. Si mara moja kusikia watu wakitumia neno "lakini pia........." bila kujua kuwa hayo ni makosa makubwa katika lugha. Kwa kawaida neno moja likitumika mengine yasitumiwe.
Matumizi ya neno "Lakini......"
Neno hili hutumika pale ambapo maelezo ya ziada huwa kinyume na maelezo ya awali au mhusika wa awali kupewa mpinzani.
Mfano: -Juma utaimba lakini Musa utacheza.
TCRA wameongeza muda wa usajili kwa alama za vidole lakini zoezi la kuzima laini zisizosajiliwa lipo pale pale.
- Mama ataandaa chakula, Lakini sisi tutaoshwa vyombo.
-Utasalimiana na Mpenzi wangu lakini usimzoee.
-Nitakuunganisha kwenye kazi lakini utanipa 5% ya mshahara kwa miezi 6.
Matumizi ya neno "vile vile......"
Hili ni neno ambalo hutumika kutoa taarifa ya ziada kutokana na taarifa ya awali. Huwa ni taarifa ya maboresho au kukazia taarifa ya awali.
Mfano: - Mama amenunua nguo na viatu vya watoto, vile vile amewanunulia daftari, peni na vitabu.
-Polisi wamemkamata kiongozi wa ujambazi, vile vile wameanzisha msako mkali ili kubaini washirika wengine.
-Timu ya mpira imemfukuza kocha wake mkuu, vile vile imewaondoa wachezaji wakigeni walio letwa na kocha huyo.
Matumizi ya neno "pia.. ."
Hili neno matumizi yake hayatofautiani na neno "vile vile ...." tofauti yake na hilo neno ni kuwa taarifa inayotolewa inaweza kuwa inalingana na taarifa ya awali au kutofautiana kabisa lakini zenye mlengo mmoja.
Mfano: - Serikali inatoa elimu bure nchi zima, pia inaendelea kuboresha huduma nyingine za kijamii.
-Benard Membe ameitwa na kamati kuu ya chama, wengine walioitwa pia ni Kinana, Makamba na Kalamagi.
-Sikukuu hii tutapika pilau, pia tutanua soda na bia ili kufurahia zaidi.
HIVYO BASI. Matumizi ya neno lakini pia katika lugha hayatakiwi na kila neno litumike pweke pweke. Inaweza ikatokea katika sentensi maneno yote yakatakiwa kutumika, hivyo katika mazingira hayo yatumike pweke pweke lakini sio kwa kuyaunganisha.
mfano: Tunashukuru kukuona ndugu yetu lakini sisi hatuta fika nyumbani kwako, pia hatutapita kwa mjomba, vile vile hatutafika kwa bibi hivyo wewe uende ukawape salamu zetu.
Sent using Jamii Forums mobile app