Anko Drew
Member
- Jun 9, 2021
- 15
- 41
MATUMIZI SAHIHI YA JIKO LA GESI
No. 1
Gesi ya kupikia yaweza kuwa ya asili (natural gas), mitungi ya gesi (liquified petroleum gas) na gesi inayotokana na kinyesi (biogas)
No. 2
Gesi hizo ni zile ambazo zina tabia ya kuwaka kama vile butane, propane na methane.
No. 3
Gesi ni nishati nzuri na rahisi kuitumia ila ni hatari kama hautozingatia usalama
No. 4
Unapopika kwa kutumia jiko la gesi hakikisha kuna hewa ya kutosha ili endapo kutakuwa na uvujaji wa gesi yasitokee madhara.
No. 5
Hakikisha mtungi wa gesi haukai Karibu na jiko (cooking place) ikiwezekana mtungi wa gesi ya kupikia uwe nje ya jiko na mpira wa gesi utoke nje kuingia ndani
No. 6
Hakikisha unaweka mtungi wa kupikia ukiwa umesimama (upright) na hakikisha hauwezi kupata misukosuko yeyote ambayo inaweza kuuharibu mtungi huo.
No. 7
Hakikisha unaangalia valve, regulator na pipe kama viko sawa kabla haujaanza kutumia gesi ya kupikia.
No. 8
Unapotumia jiko la gesi usiache kitu Jikoni na wewe ukaondoka vinaweza kuungua na kusababisha moto au tatizo likatokea bila wewe kuona.
No. 9
Hakikisha unakagua mpira unaopitisha gesi mara kwa mara kwa kupaka povu la sabuni ili kuona kama kuna sehemu inavuja. Pia hakikisha unabadilisha mpira kila baada ya miaka miwili na valve baada ya miaka 3-5
No. 10
Ukitaka kujua mtungi wa gesi upo kiasi gani usiutingishe. Chukua kitambaa weka maji kisha paka kwenye huo mtungi kuzungushia kwa pembeni na utaona kiasi kilichobaki, Ni hatari kutingisha mtungi wa gesi ya kupikia.
No. 11
Mambo ya kuzingatia endapo utahisi harufu ya gesi ya kupikia jikoni;
-Hakikisha unafungua milango na madirisha hewa iingie na kutoka.
-hauwashi moto wa aina yeyote.
-hakikisha kama taa zimezimwa usiwashe na kama zimewashwa usizizime. -hakikisha hauwashi tochi au simu.
-Usipige picha kwa simu au camera.
-Toa mtungi nje ya jiko na ukague wapi unavuja.