Matumizi saba ya baking Soda ( Magadi Soda)

CharmingLady

JF-Expert Member
Apr 16, 2012
18,250
12,868
Habari wana JF Chef....
Kuna hii mada nimekutana nayo nikaona ni vyema nikashare nanyi... Ni ndefu ila ina ujumbe mzuri sana!!! Karibuni

Najua wengi mnaifaham Baking soda au Bicarbonate of soda kwa lugha ya Kiswahili huitwa magadi soda ,kwa wale msioifahamu, Baking soda au bicarbonate of soda ni hitaji la kawaida kabisa jikoni,

Hutumika sana katika vyakula vya kuoka kama keki na mikate pia hutumika katika maandazi, pan cakes, chapati na vyakula vingine vingi. Hata ivyo Baking soda wakati mwingine hutumika kulainisha vyakula ambavyo ni vigumu kuiva au visivyolainika haraka vinapopikwa kama mahindi yasiokobolewa, mboga za majani za kienyeji kama mgagani, msusa, majani ya kunde yaliyo komaa na kadhalika.

Hapa nchini Baking soda ya jina kubwa na kufaamika kwa wengi inaitwa SIMBA.
Baking soda hupatikana kwa wingi madukani na hata sokoni. kuna ile ambayo imepita kiwandani na kusindikwa kitaalam na kuna ile ya kienyeji ambayo iko kiasili zaidi.

Siri kubwa ambayo wengi hawajui kuhusu baking soda, Ni ambavyo huweza kutumika kufanya shughuli nyingi za usafi. Uwepo wa alkalini ndani ya baking soda huipa uwezo wa kuondoa uchafu wenye asili ya asidi.

1. Kusafisha kibao cha kukatia nyama au mboga.

Kwa wale mnaotumia kibao cha plastiki au mbao kukata nyama mnajua ambavyo kibao hushika uchafu na hata kubadilika rangi, hata baada ya kukiosha. Kutatua tatizo hilo na kufanya kibao chako kiwe safi na cheupe tena, Nyunyuzi baking soda ya kutosha kisha sugua na dodoki hadi kibao kiwe safi, kama ni uchafu wa muda mrefu loanisha kibao na maji kisha nyunyuzi baking soda na uache kwa dakika 15 ndipo usugue na dodoki

2. Kuzibua sinki la jikoni.
Sinki la jikoni mara nyingi huziba na kugoma kupitisha maji machafu kwasababu ya mafuta na uchafu wa chakula. Mwaga kikombe kimoja cha baking soda kwenye tundu la sinki, kisha mwaga vikombe vitatu vya maji ya moto sana. Acha kwa angalao masaa manne kabla hujatumia sinki. Ni vyema ukafany ivyo usiku unapoenda kulala kwani sinki halitatumika adi asubuhi.

3. Kukata harufu ya mkojo chooni.

Kama unasafisha choo lakini bado kuna harufu mbaya ya mkojo.Chukua nusu kikombe cha baking soda changanya na nusu kikombe cha vinegar nyeupe kisha mwaga ndani ya choo na unyunyuze kwenye sakafu ,na baada ya nusu saa unaweza kudeki sakafu ili pabaki safi.

4. Kusafisha na kung’arisha sinki,bathtab na tiles.

Ingawa wengi hupenda kuweka tiles,masinki na Bathtubs kwenye nyumba zao,utakubaliana na mimi nikisema wengi hawajui namna ya kuzifanyia usafi,unakuta sinki au tiles nyeupe zimegeuka na kua za rangi ya njano kwa uchafu.

Chukua nusu kikombe cha baking soda changanya na nusu kikombe cha sabuni ya majichanganya vizuri ili kupata kama uji mzito.Kisha tumia kusugua sinki,tiles au bathtub.

5. Kusafisha Oven
Kawaida unapohoka vyakula kama nyama,samaki,mboga za majani na matunda kama nanasi,mchuzi au umajimaji kutoka kwenye vyakula hivi humwagika ndani ya oven.Wakati mwingine unapo rost vyakula ndani ya mafuta kwenye grill,mafuta huruka na kuchafua oven.Kwa kawaida uchafu wa aina hii Uganda haraka sana ndani ya oven.

Ili kusafisha .weka baking soda yakutosha kwenye sehem ya chini kabisa ya oven,kisha iloanishe na maji,usiweke maji mengi,kiasi tu cha kutosha kuloanisha baking soda.Fanya hivi usiku kabla ya kulala na ifikapo asubui uchafu wote ulioganda utakua umelainika,tumia dodoki kusafisha.

6.Kukata /Kuondoa harufu mbaya ndani ya friji.

Kutokana na uwekaji wa vyakula iana mbalimbali vyenye harufu tofauti tofauti mara nyingi friji huwa na harufu isioeleweka.Kwa sisi yunaoishi Tanzania na kukabiliwa na tatizo la umeme,umeme unapokatika kwa muda mrefu friji hutoa harufu.

Chukua boksi la baking soda,lifungue na kisha fungua mfuko wa plastiki uliobeba baking soda ili ukae wazi,kisha weka baking soda hiyo kwenye sehem ya chini ya friji yako,itanyonya harufu yote ndani ya friji na kuiacha ikiwa fresh.Ukiweka boksi lenye baking soda kidogo utendaji wake huwa wataratibu sana,hivyo ni vyema ukaweka boksi jipya.

7.Kukata harufu kwenye nguo mpya
Mara nyingi unaponunua nguo mpya inakua na harufu ya upya na ndio maana watu wengi hufua nguo mpya kabla hawajavaa.Nguo za mtumba nazo hua na harufu kali inayolazimu kufua kabla hujavaa,hizi zote ni harufu za kemikali zilizotumika katika utengenezaji wa nguo,na kwa nguo za mitumba ni harufu ya madawa yenye kemikali zinazotumika kuhifadhi nguo.

Ili kuondoa harufu hizo,pima kikombe kimoja cha baking soda changanya kwenye maji lita tano ,kisha loweka nguo kwenye maji hayo kwa masaa matatu au zaidi,suuza na uanike.

Kwakua baking soda inaweza fanya yote haya,unakila sababu ya kua nayo jikoni kwako,hasa kwa ajili ya kusafishia kibao cha kukatia Nyama na mboga,pamoja na kuzibua sinki lako la jikoni.Ukweli ni kwamba,kibao cha kukatia nyama kikiwa kichafu,au kimebadilika rangi na mabaki ya nyama yamenata au kuganda kwenye kibao hicho,inatia kinyaa na pia ni hatari kwa afya ya familia yako.

Sinki la jikoni nalo likiziba na kuacha kupitisha maji machafu ndio mwanzo wa kurundika viombo vichafu na kua na maji machafu kwenye beseni kila wakati, chanzo kikubwa cha inzi jikoni na magonjwa ya tumbo.

Kama kawaida,naboresha maisha ya familia yako, Kazi yangu ni kukuelimisha tu, utendaji ni juu yako.
Jali afya ya familia yako.

Source: tollyzkitchen
 
Ninatumaini akina mama/dada wa JF wataitumia hii mada effectively make wengi wengi tu wahanga kwa namna moja ama nyingine...

Hebu njooni huku haraka ninyi akina gfsonwin, snowhite, Preta, Pretty, Madame B, Elizabeth Dominick, Fixed Point, ladyfurahia, sweetlady, miss strong, Farkina, kashesho, Blue G, Nivea, lara 1, Evelyn Salt, ram, TrueLove, Munkari, Heaven on earth, measkron, King'asti, mimi49, madameA, Ablessed, christine ibrahim, Passion Lady, Kongosho, Kaunga, Asnam, KOKUTONA, Smile, Mkunde Original na wadada/ wamama wooooote wa JF....

Pia wakaka / wababa mnaweza kuchukua maujuzi na kuwapelekea wenzi wenu. Ila kuna wale ambao ni mabachelor pia wanakaribishwa!!!!!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Dah hii kitu kumbe muhim sana, kuliko nnavyoichukulia. Nakuhakikishia huitumia kwenye upishi tu, tena vitu vya kukanda , so hukaa mda mrefu kweli. Nashukuru sana kwa hilo, ntaipa hadhi yake
 
8.Kusafisha meno kuwa meupe na kuondoa yanga oyeee.

=========================
Ukipa Ujumbe wa chuki matusi futa delete kabisa.
=========================
 
Pia unaweza itumia kusafisha terminal za betri ya gari iliyo develop caborn.
 
Habari wana JF Chef....

Kuna hii mada nimekutana nayo nikaona ni vyema nikashare nanyi... Ni ndefu ila ina ujumbe mzuri sana!!! Karibuni

Najua wengi mnaifaham Baking soda au Bicarbonate of soda kwa lugha ya Kiswahili huitwa magadi soda ,kwa wale msioifahamu,Baking soda au bicarbonate of soda ni hitaji la kawaida kabisa jikoni,hutumika sana katika vyakula vya kuhoka kama keki na mikatepia hutumika katika maandazi,pan cakes,chapatti na vyakula vingine vingi.Hata ivyo Baking soda wakati mwingine hutumika kulainisha vyakula ambavyo ni vigumu kuiva au visivyolainika haraka vinapopikwa kama mahindi yasiokobolewa,mboga za majani za kienyeji kama mgagani, msusa,majani ya kunde yaliyo komaa na kadhalika.Hapa nchini Baking soda ya jina kubwa na kufaamika kwa wengi inaitwa SIMBA.

Baking soda hupatikana kwa wingi madukani na hata sokoni.kuna ile ambayo imepita kiwandani na kusindikwa kitaalam na kuna ile ya kienyeji ambayo iko kiasili zaidi.

Siri kubwa ambayo wengi hawajui kuhusu baking soda,Ni ambavyo huweza kutumika kufanya shughuli nyingi za usafi.Uwepo wa alkalini ndani ya baking soda huipa uwezo wa kuondoa uchafu wenye asili ya asidi.

1.Kusafisha kibao cha kukatia nyama au mboga.

Kwa wale mnaotumia kibao cha plastiki au mbao kukata nyama mnajua ambavyo kibao hushika uchafu na hata kubadilika rangi,hata baada ya kukiosha.Kutatua tatizo hilo na kufanya kibao chako kiwe safi na cheupe tena,Nyunyuzi baking soda ya kutosha kisha sugua na dodoki adi kibao kiwe safi,kama ni uchafu wa muda mrefu loanisha kibao na maji kisha nyunyuzi baking soda na uache kwa dakika 15 ndipo usugue na dodoki

2.Kuzibua sinki la jikoni.

Sinki la jikoni mara nyingi huziba na kugoma kupitisha maji machafu kwasababu ya mafuta na uchafu wa chakula.Mwaga kikombe kimoja cha baking soda kwenye tundu la sinki,kisha mwaga vikombe vitatu vya maji ya moto sana.Acha kwa angalao masaa manne kabla hujatumia sinki.Ni vyema ukafany ivyo usiku unapoenda kulala kwani sinki halitatumika adi asubuhi.

3.Kukata harufu ya mkojo chooni.

Kama unasafisha choo lakini bado kuna harufu mbaya ya mkojo.Chukua nusu kikombe cha baking soda changanya na nusu kikombe cha vinegar nyeupe kisha mwaga ndani ya choo na unyunyuze kwenye sakafu ,na baada ya nusu saa unaweza kudeki sakafu ili pabaki safi.

4.Kusafisha na kung'arisha sinki,bathtab na tiles.

Ingawa wengi hupenda kuweka tiles,masinki na Bathtubs kwenye nyumba zao,utakubaliana na mimi nikisema wengi hawajui namna ya kuzifanyia usafi,unakuta sinki au tiles nyeupe zimegeuka na kua za rangi ya njano kwa uchafu.

Chukua nusu kikombe cha baking soda changanya na nusu kikombe cha sabuni ya majichanganya vizuri ili kupata kama uji mzito.Kisha tumia kusugua sinki,tiles au bathtub.

5.Kusafisha Oven

Kawaida unapohoka vyakula kama nyama,samaki,mboga za majani na matunda kama nanasi,mchuzi au umajimaji kutoka kwenye vyakula hivi humwagika ndani ya oven.Wakati mwingine unapo rost vyakula ndani ya mafuta kwenye grill,mafuta huruka na kuchafua oven.Kwa kawaida uchafu wa aina hii Uganda haraka sana ndani ya oven.

Ili kusafisha .weka baking soda yakutosha kwenye sehem ya chini kabisa ya oven,kisha iloanishe na maji,usiweke maji mengi,kiasi tu cha kutosha kuloanisha baking soda.Fanya hivi usiku kabla ya kulala na ifikapo asubui uchafu wote ulioganda utakua umelainika,tumia dodoki kusafisha.

6.Kukata /Kuondoa harufu mbaya ndani ya friji.

Kutokana na uwekaji wa vyakula iana mbalimbali vyenye harufu tofauti tofauti mara nyingi friji huwa na harufu isioeleweka.Kwa sisi yunaoishi Tanzania na kukabiliwa na tatizo la umeme,umeme unapokatika kwa muda mrefu friji hutoa harufu.

Chukua boksi la baking soda,lifungue na kisha fungua mfuko wa plastiki uliobeba baking soda ili ukae wazi,kisha weka baking soda hiyo kwenye sehem ya chini ya friji yako,itanyonya harufu yote ndani ya friji na kuiacha ikiwa fresh.Ukiweka boksi lenye baking soda kidogo utendaji wake huwa wataratibu sana,hivyo ni vyema ukaweka boksi jipya.

7.Kukata harufu kwenye nguo mpya

Mara nyingi unaponunua nguo mpya inakua na harufu ya upya na ndio maana watu wengi hufua nguo mpya kabla hawajavaa.Nguo za mtumba nazo hua na harufu kali inayolazimu kufua kabla hujavaa,hizi zote ni harufu za kemikali zilizotumika katika utengenezaji wa nguo,na kwa nguo za mitumba ni harufu ya madawa yenye kemikali zinazotumika kuhifadhi nguo.

Ili kuondoa harufu hizo,pima kikombe kimoja cha baking soda changanya kwenye maji lita tano ,kisha loweka nguo kwenye maji hayo kwa masaa matatu au zaidi,suuza na uanike.

Kwakua baking soda inaweza fanya yote haya,unakila sababu ya kua nayo jikoni kwako,hasa kwa ajili ya kusafishia kibao cha kukatia Nyama na mboga,pamoja na kuzibua sinki lako la jikoni.Ukweli ni kwamba,kibao cha kukatia nyama kikiwa kichafu,au kimebadilika rangi na mabaki ya nyama yamenata au kuganda kwenye kibao hicho,inatia kinyaa na pia ni hatari kwa afya ya familia yako.Sinki la jikoni nalo likiziba na kuacha kupitisha maji machafu ndio mwanzo wa kurundika viombo vichafu na kua na maji machafu kwenye beseni kila wakati,chanzo kikubwa cha inzi jikoni na magonjwa ya tumbo.

Kama kawaida,naboresha maisha ya familia yako,Kazi yangu ni kukuelimisha tu,utendaji ni juu yako.

Jali afya ya familia yako.

Source: tollyzkitchen

Ahsante sana mdogo wangu...mi nilikuwa naitumia kwenye mapishi tu.

Got you babby
 
Ninatumaini akina mama/dada wa JF wataitumia hii mada effectively make wengi wengi tu wahanga kwa namna moja ama nyingine...

Hebu njooni huku haraka ninyi akina gfsonwin, snowhite, Preta, Pretty, Madame B, Elizabeth Dominick, Fixed Point, ladyfurahia, sweetlady, miss strong, Farkina, kashesho, Blue G, Nivea, lara 1, Evelyn Salt, ram, TrueLove, Munkari, Heaven on earth, measkron, King'asti, mimi49, madameA, Ablessed, christine ibrahim, Passion Lady, Kongosho, Kaunga, Asnam, KOKUTONA, Smile, Mkunde Original na wadada/ wamama wooooote wa JF....

Pia wakaka / wababa mnaweza kuchukua maujuzi na kuwapelekea wenzi wenu. Ila kuna wale ambao ni mabachelor pia wanakaribishwa!!!!!!!!!!
Asante sana nimejifunza mengi lol kumbe ina matumizi mengi kiasi hiki.
 
Du ngojea nikanunue sasa hiv niiweke kwenye flig maana niliondoka kama siku 5 nikazima Flige ubachelol huu.kumbe kwenye Fliza nilisahau kuwa kulikuwa na kuku sasa hiyo harufu nimeosha leo lakin badoo.Ndo raha ya jf unapata solution ya matatizo yako.Ubarikiwe mleta mada

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Nashukuru sana mkuu .... Unajua kupitia JF nimejifunza mambo mengi. Hivyo nami nikiona kuna kitu kizuri mahali sisiti kushare na member wenzangu!!!
 
34 Reactions
Reply
Back
Top Bottom