LE GAGNANT
JF-Expert Member
- Jan 20, 2011
- 1,241
- 251
Serikali ya TZ ina matumizi mengi ambayo hayana faida yoyote kwa mwananchi wa kawaida. Mfano: Kuna viongozi lukuki wastaafu wa kisiasa na kijeshi wanaoendelea kulipwa mishahara hadi wafe. Marais na mawaziri wakuu wastaafu bado wanapata marupurupu yote maishani. Jeshini kuanzia cheo cha major general, lieutenant general na general wakistaafu wanaendelea kulipwa mishahara hadi wafe na mashangingi wanabadilishiwa yakichoka, service zote serikalini na marupurupu kibao. Ukichanganya na wabunge wa kuteuliwa, waku wa mikoa na wilaya ambao kazi zao zinafanywa na wakurugenzi, wao ni kutoa matamko tu. Mkulo, ndio maana pesa inaishia kuwalipa wao kwa kuwa wao wana 'lion share'.