Matumizi mabaya ya ofisi na Mali ya umma!

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
251
1,000
Hakuna binadamu aliyekamilika, lakini pia binadamu wote niwabinafsi.

Kwa sifa hizo mbili kila binadamu amewekewa mipaka na katika uongozi zimewekwa sheria za kufuata na ambazo tunapoapa tunaahidi kuzilinda na kuziheshimu sheria zilizowekwa.

Wapo watu kila siku wanashangilia na kuelekeza binadamu wengine wakamatwe na kutiwa ndani kwa makosa ya ubadhirifu wa mali za umma au matumizi mabaya ya madaraka.Watuhumiwa uhukumiwa kwa kukiuka sheria na kanuni mbalimbali zilizowekwa,

Cha kushangaza wao ndio wabadhirifu namba moja wa mali za umma, ndio watumiaji vibaya wa ofisi za umma.

Haya matumizi mabaya ya ofisi yaliligharimu Taifa, yanaligharimu na yataligharimu Taifa hadi pale tutakapo kemea watu kwa nafasi zao kujipangia namna wanavyotaka fedha zetu za Kodi zitumike bila kufuata taratibu zilizowekwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom