Matumizi mabaya ya akili kuwaacha wananchi wafe/wakinamama wajifungue njiani wakienda kwa miguu hospitali then uwasombe kwa gari wakati wa kampeni

lukoma

JF-Expert Member
Jul 1, 2013
2,991
2,000
Siwezi sahau siku niliposimamishwa njiani na mama aliyevaa flana ya kijani akiwa na mwanae wakike aliyekaribia kujifungua. Kwanza nilimpita, lakini nilipofika mbele kidogo huruma ilinijia nikaamua kurudi kuwachukua na kawapeleka mpaka hospitalini. Baada ya kuwashusha yule mama alisema asante baba, nilimwangalia usoni sikumjibu nikaondoka.

Nauliza hii ni akili au matope?

Miaka mitano 5 iliyopita wako wagonjwa waliofia njiani wakiwa wanakwenda hospitali kwa miguu. Wako wakinamama waliojifungulia njiani wakiwa wanakwenda hospitali kwa miguu.

Wako wakinamama waliolazimika kupanda daladala wakiwa wametoka kujifungua wanalazimika kubanana kwa kuwa hawana hata buku ya bajaji na hakuna wa kuwasaidia.

Wako pia wakinamama wakitoka kujifungua na wagonjwa huomba wasamalia wema wawasaidie nauli ya tena buku au miatano tu. Ajabu na mshangao wakina mama hawa walojifungulia njiani kwa kukosa usafiri, na wengine ndugu zao walifia njiani kwa kukosa usafiri leo amekuwa wafalme na malkia wanafuatwa na bus na magari kupelekwa kwenye kampeni wakiwa wazima.

Swali, katika mazingira kama haya mjinga ni nani? Yule anaewasomba kwa magari wakati wa kampeni au wale wanaokubali kusombwa kwa magari wakati wa kampeni wakiwa wazima lakini wakiwa wagojwa wanatembea kwa miguu kwenda hospitali helplessly!!
 

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
8,254
2,000
Swali, katika mazingira kama haya mjinga ni nani? Yule anaewasomba kwa magari wakati wa kampeni au wale wanaokubali kusombwa kwa magari wakati wa kampeni wakiwa wazima lakini wakiwa wagojwa wanatembea kwa miguu kwenda hospitali helplessly!!
Pande zote mbili zinafaa kupata cheti Cha ujinga.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom