Matumizi Kadi NYEUPE katika mchezo wa mpira wa miguu

DATAZ

JF-Expert Member
May 25, 2012
2,449
5,974
kadi nyeupe.png

Katika mechi ya Sporting vs Benfica Jana, Mwamuzi alitoa kadi nyeupe Mchezoni. Kwa wengi waliozoea kadi ya Njano na Nyekundu tu Mchezoni, tukio Hilo liliacha maswali.

Wataalam wa soka wanafafanua kuwa kadi nyeupe hutumika kama kuonesha Appreciation kwa jambo jema lililofanyika Mchezoni (fair play).


---
A white card has been issued for the first time in a football match in Portugal.

The card was shown during a women's cup match between Sporting Lisbon and Benfica on Saturday after medical staff from both clubs rushed to help a fan who had fainted in the stands as Benfica led 3-0 during the first half.

Referee Catarina Campos then showed the card to both teams.

The gesture recognises and praises acts of fair play.

Fans at the Estadio da Luz in Lisbon were heard cheering and applauding the decision.

The cards were introduced as part of an initiative of Portugal's National Plan for Ethics in Sport to encourage fair play and have been adopted by the Portuguese Football Federation.

So far only Portugal has adopted the white card.

They contrast yellow and red cards which are used to discipline players for misconduct.

Benfica won 5-0 to progress to the semi-finals.

The match also set a new attendance record for women's football in Portugal, with 15,032 fans showing up, beating the previous record of 14,221 seen in May last year.

While the use of the white card in the match on Saturday was celebrated, it remains to be seen how fans will react to their implementation if they are used more widely.

It comes after a FIFA directive saw stoppage time added at the end of each half for "unnatural lost time" during the Qatar World Cup.

Stoppages were added for time-wasting by players, treatment for injuries, lengthy goal celebrations, substitutions, VAR interventions and yellow or red cards.

Source: White card issued for first time in Portuguese football match
 
Nmeikuta mahali

Ni mpango wa Rais wa UEFA Michel Platini alisema hayo kwenye mkutano wa michezo uliofanyika Dubai, Bwana Platini alitoa ufafanuzi wa jinsi kadi hiyo itakavyo tumika mcheza akifanya kosa na kupewa kadi nyeupe atatakiwa kutoka nje kwa dk 10 na kurudi tena uwanjani. Kadi ya njano na nyekundu zitabakia vile vile na makosa yake kama mwanzo kabla ya kadi nyeupe.
 
View attachment 2492700
Katika mechi ya Sporting vs Benfica Jana, Muamuzi alitoa kadi nyeupe Mchezoni. Kwa wengi waliozoea kadi ya Njano na Nyekundu tu Mchezoni, tukio Hilo liliacha maswali.

Wataalam wa soka wanafafanua kuwa kadi nyeupe hutumika kama kuonesha Appreciation kwa jambo jema lililofnyika Mchezoni (fair play).
kwa hiyo mchezo unasimama ili refa aweze ku-appreciate?
 
Hakuna asiyejua kuhusu kadi nyekundu ama kadi ya njano katika mchezo wa soka. Kwa wengi wanaofuatilia soka, kadi nyekundu inafahamika zaidi kwa kuwa hupewa mchezaji ambaye aameonyesha mchezo usio wa kiungwana kama kucheza rafu mbaya, kushika mpira kwa makusudi, kutukana na mengine. Inawahusu pia hata benchi la ufundi.

Kadi ya njano yenyewe inatumika kuonya mchezaji ama bechi la ufundi ama yeyote anayehusishwa na mchezo kwa makosa madogo madogo ya uwanjani ama nje ya uwanja.

Kadi hizi zilianza kutumika miaka zaidi ya 50 iliyopita ikitambulishwa kwa mara ya kwanza kwenye kombe la dunia la mwaka 1970 lililofanyika nchini Mexico ili kupunguza rafu uwanjani zilizoanza kuongezeka katika mechi nyingi za soka wakati huo.

Lakini Januari 21, 2023 imekuwa siku ya kihistoria kwa kadi nyingine ya tatu kuanza kutumika, ni kadi nyeupe.

Imeanza kutumika rasmi kwa mara ya kwanza katika historia ya soka duniani kwenye mchezo wa kombe la ligi huko Ureno kwa timu za wanawake kati ya Sporting Lisbon na Benfica.

N kitu kikubwa kilichofikiriwa kwa muda sasa, lakini inamaanisha nini hasa?

Kadi nyeupe na tafsiri yake
Rangi nyeupe ina maana na uhusiano kadhaa wa kadhaa, ingawa maana zinaweza kutofautiana kulingana na mtu binafsi na tamaduni wanazoishi nazo.

Lakini tafsiri isiyo rasmi kuhusu rangi nyeupe iliyozoeleka mara nyingi rangi nyeupe inawakilisha usafi, kutokuwa na hatia na unyenyekevu.

Hili la unyenyekevu ndilo hasa linalohusisha kwa namna yake kadi nyeupe iliyoanza kutumika katika mchezo wa soka duniani.

Kadi nyeupe inaonyeshwa kutambua na kuhamasisha 'fair play' au uungwana, mchezo mzuri ama jambo zuri katika mchezo wa soka na "imewekwa maalumu kuboresha na kuimarisha nidhamu katika mchezo wa soka", anasema Shaban Shomvi, mmoja wa wacheza soka wa zamani wa Tanzania.

Huko nyuma mchezo mzuri ama jambo zuri la kiungwana katika mchezo huo lilitambuliwa baadaye kwa tuzo kutolewa kwa timu fulani ama mchezaji ama mdau yeyote wa soka, lakini sasa kadi hii itaanza kutambua hilo hapo hapo uwanjani wakati mchezo ukiendelea.

Tukio gani lilisababisha kadi nyeupe kutolewa kwa mara ya kwanza?
Sporting Lisbon na Benfica ni timu hasimu nchini Ureno, ziwe zinakutana timu za wanaume ama wanawake, mechi baina ya timu hizi huwa na upinzani mkali na wakati mwingine uleta vurugu ndani na nje ya uwanja.

Pengine muamuzi Catarina Camposwa aliyechezesha mchezo huo uliozikutanisha timu hizi katika mchezo wa robo fainali ya Taca de Portugal cup kwa wanawake uliopigwa Januari 21, 2023 mjini Lisbon aliona umuhimu wa kuwa nayo na kuitoa kwa sababu ya asili ya upinzani uliopo. Lakini kwa aina ya mchezo huo kuyapata matukio ya 'kiutu' yanayostahili kadi nyeupe iliwezekana.

Ruka Twitter ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Bonyeza kisha endelea
Maelezo ya video,Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa Twitter ujumbe, 1
Mchezo ukiwa unaendelea mmoja wa mashabiki alijisikia vibaya' kuumwa', ikalazimu madaktari wa timu zote mbili kukimbilia jukwaani kumsaidia kuokoa maisha ya mgonjwa huyo, kitendo hicho kilionekana ni cha kiungwana, kimichezo na cha kiutu, kilichomfanya refa au muamuzi Camposwa kuwapa kadi hiyo nyeupe madaktari wa pande zote mbili. Historia ikaandikwa.

Benfica ilishinda mchezo huo kwa mabao 5-0 mjini Lisbon. Lakini ushindi huo wala sio jambo linalozungumzwa, kinachozungumzwa ni kadi nyeupe na uungwana wa madaktari hao wa timu hizo.

Wadau wamepokeaje kadi hii?
Kama ilivyokuwa kwenye michuano ya kombe la dunia lililofanyika Qatar mwezi uliopita, ambapo Shirikisho la soka duniani (FIFA), lilikuwa linaongeza muda wa nyongeza mpaka dakika 10 ili kufidia muda unaopotezwa kwa makusudi na wachezaji, kadi nyekundu pia imepokelewa kwa hisia tofauti lakini kwa ujumla inaonekana kuungwa mkono zaidi.

Wengine kwenye mitandao wamekuwa na mitazamo ya namna hii lakini wapo pia wanaoipinga, mmoja wao ni Neil Fissler, mwandishi wa habari za michezo mahiri Uingereza akisema ni wazo lisilo na maana kwenye historia ya soka.

Ruka Twitter ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Bonyeza kisha endelea
Maelezo ya video,Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa Twitter ujumbe, 2
Lakini wanaounga mkono wanasema ni jambo la kubebwa. 'Nidhamu popote pale iwe uwanjani nje ya uwanja, nyumbani, shuleni hata makazini ni jambo la msingi sana, kadi nyeupe kutumika kila mahali ni msingi wa kuimarisha nidhani', anasema Seif Shangali, mdau wa soka Tanzania na kuongeza' ni muda wa FIFA na nchi wanachama kuifikiria na kuitengenezea sheria na kanuni'.

Nani kaileta na lini itaanza kutumika kwenye ligi kubwa duniani?


Kadi nyekundu na kadi ya njano zimeanza kutumiaka miaka zaidi ya 50 iliyopita

Mwaka 2014, aliyekuwa rais wa shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) Michel Platini aliwahi kutoa wito wa kuanzishwa kwa kadi nyeupe lakini yeye alitaka itumike kama adhabu kwa wachezaji ambao wanakuwa wakorofi uwanjani na kadi hiyo inampa nguvu muamuzi kumtoa mchezaji wa aina hiyo nje kwa dakika 10 kabla ya kumrejesha.

Hiyo ni mbali na kadi ya njano na nyekundu ambayo anaweza akapewa kadi hizo akirejea na kutenda madhambi yanayostahili kadi hiyo.

Hata hivyo wazo lake hilo halikufika popote. Kwa ujumla lilikutana na upinzani mkali na kwa wale waliopinga walionyesha kwamba ni kadi ambayo ingeuwa nguvu ya kadi ya njano, lakini pia ingempa muamuzi asiye muaminifu upenyo wa kuitumia kadi hiyo na kuacha nyingine kwa manufaa ya mahaba yake kwa timu ama mchezaji.

Waliopinga walikuwa na hoja kuwa ni bora kadi nyeupe itambulishe 'fair play' ili kuboresha nidhamu katika soka. Na sasa tunaanza kushuhudia hili likianzia Ureno, moja ya nchi wanachama wa UEFA.

Ni wazi haitaanza kutumika hivi karibuni katika ligi kubwa duniani kama za England, Ujerumani, Hispania, Ufaransa na Italia, lakini kuanzishwa kwake Ureno kutazishtua mamlaka za soka za kimataifa kama UEFA na FIFA, kufikiria upya suala hilo.

Kanuni za FIFA ni muongozo wa kanuni za mataifa wanachama. Hivyo kama FIFA italibeba hili na vyama vya mabara kama UEFA kwa Ulaya, CAF kwa Afrika na vyama vya mabara mengine, huenda siku moja tukashuhudia kadi nyeupe kwenye mifuko ya kila refa au muamuzi duniani.


Chanzo BBC
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom