SoC02 Matumizi holela ya dawa za binadamu yanaathari kubwa Sana kwa mtumiaji

Stories of Change - 2022 Competition

Adqcos

New Member
Jul 20, 2022
2
0
Nikianza kwa kutaka kujua kama ni sheria ambayo siyo thabiti juu ya matumizi ya dawa za binadamu au wasimamizi wa sheria ya matumizi ya dawa za binadamu ndiyo hawazisimamii inavyotakiwa au tatizo lipo kwa wadau wanaotumia sheria ya matumizi ya dawa za binadamu?

Matumizi holela ya dawa za binadamu yanatokana na watu wengi kutokuwa na uelewa juu ya athari zitokanazo na matumizi holela ya dawa za binadamu, Lakini mbaya zaidi kuna wakati mwingine kitendo hiki kiovu hufanywa na wataalamu wa afya kwa makusudi na kusababisha madhara kwa mtumiaji.

Wakati mwingine waajiri hususani wa taasisi binafsi huwalazimisha waajiriwa wao kutoa dawa kwa wagonjwa nje ya utaratibu wa matibabu ili tu kituo kipate kuuza dawa na kupata faida ya kutosha pia waajiliwa utii amri au maelekezo hayo maana hutishiwa kwa kutoingiza mapato inaweza pelekea kutokupata ujira au mshahara wake.

Wakati mwingine changamoto huja kutoka kwa baadhi ya wagonjwa kulazimisha kupatiwa matibabu ya aina fulani hali ya kuwa vipimo havioneshi ya kuwa anatatizo hilo. Mfano kipimo cha haraka cha Malaria ni chepesi kukifanya na kinapunguza makosa mengi yaliyokuwa yanatokana na binadamu na kupelekea kupatia wagonjwa majibu ambayo siyo sahihi, watu wengi hawakiamini kipimo hiki na majibu yatakapotoka hawana maambukizi ya vimelea vya wadudu wa malaria hulazimmisha kupatiwa dawa za malaria.

Changamoto nyingine utokana na baadhi ya wataalamu wa maabara haswa za binafsi kutoa majibu ambayo si sahihi kwa wagonjwa na watakapoyarudisha kwa daktari au kwa wataalamu.

wanaohudumu katika maduka ya madawa muhimu husababisha wapatiwe dawa ambazo siyo sahihi na zisizo na faida yeyote kwenye miili yao na kuwaletea athari bila ya kupona kwa matatizo yaliyokuwa yanamsumbua mgonjwa.

Kwa baadhi ya taasisi kutokufuata miongozo ya kimatibabu iliyoainishwa na wizara ya Afya nchini kwa kutoiamini na kuamini ya kuwa miongozo ya nchi za kigeni ni sahihi zaidi bila ya kujali ya kuwa ili dawa hizi ziweze kutolewa na miongozo hutolewa baada ya kufanya tafiti za kutosha Mf: kuna taasisi moja mkoani shinyanga madaktari waliopo pale hawafuati kabisa miongozo ya Nchini kwetu kitu ambacho kinatengeneza usugu wa maradhi kwa wagonjwa wetu.

MADHARA YATOKANAYO NA MATUMIZI HOLELA YA DAWA ZA BINADAMU
Kutengeneza usugu wa ugonjwa
Kuharibu ini kwakuwa dawa nyingi huchakatwa na Ini zinapoingia mwilini
Kutengeneza sumu mwilini
Kuharibu mzunguko wa hedhi kwa wasichana na wanawake wanaotumia dawa za kujikinga na ujauzito bila kufuata utaratibu.

Huweza kusababisha kifo kwa mtumiaji hii inaweza kutokana na aina ya dawa uliyoitumia inaweza kuwa umetumia nyingi kuliko kiwango cha mahitaji ya mwili wako au umetumia dawa ambayo haukutakiwa kuitumia kabisa kama vile dawa zinazotumika kuongeza nguvu za kiume
Huchangia kuharibu ujauzito au kusababisha/kuchangia kujifungua mtoto au watoto wenye ulemavu kama vile ukiziwi

Hayo ni madhara machache tu kati ya mengi yanayoweza kusababishwa na matumizi holela ya dawa za binadamu.

NINI KIFANYIKE ILI KUNUSURU AFYA ZA WATANZANIA WENZETU WANAOTUMIA MADAWA KIHOLELA BILA YA KUJUA MADHARA YAKE;
Elimu ya kutosha itolewe kwa wananchi ili wajue madhara yatokanayo na matumizi holela ya dawa za binadamu.

Kuweka sheria na msisitizo wa kufuata miongozo ya nchini kwetu kwa madaktari wa kigeni wanaokuja kufanya kazi hapa nchini kwetu.

Kutengeneza na kuzisimamia kikamilifu sheria za utoaji dawa kwa kuzingatia miongozo na atakaekiuka apewe adhabu hata ya kufungiwa leseni yake ya kazi kwa muda au moja kwa moja.

Wamiliki wa vituo vya binafsi wapatiwe hisani hata ya kusaidiwa kulipa mishahara ya wafanyakazi walahu gawio la nusu kutoka serikalini au kwa mashirika mbalimbali ya kibinadamu ili waweze kutoa huduma za afya na malipo kwa wafanyakazi pasipo kuteteleka kiuchumi.

PIA KUNA CHANGAMOTO ZINAZOTOKANA NA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA
Hii kwa tafsiri ya haraka haraka changamoto yake inaweza isionekane lakini ukweli ni kwamba moja kati ya watu wanaofanya matumizi holela ya dawa za binadamu ni wanachana wa mfuko wa taifa wa bima ya hasa wale walioko mazingira ambayo kuna vituo vya awali vya kutolea huduma za afya kama vile Zahanati kwasababu ya makatazo ya baadhi ya huduma kwa wanachama kulingana na hadhi ya kituo hicho.

Pia Mfuko wa taifa wa bima ya Afya unapitia changamoto ya kiuchumi. Changamoto hii inatokana na ubadhilifu wa fedha unaotokana na baadhi ya wateja wake kutokuwa waaminifu kwa maana ya vituo vya kutolea huduma za Afya Zahanati, vituo vya Afya, Hospitali na kliniki za kibingwa na hata wanachama wa mfuko huo.

Kitendo hicho cha ubadhilifu kinapelekea mfuko kushindwa kumudu kulipa madeni ya wateja wake hivyo na kusababisha wateja wanaostahiki kupata huduma kutoka katika vituo ivyo kukosa huduma stahiki kwa wakati na wakati mwingine kutothaminiwa na vituo vya kutolea huduma tofauti na wagonjwa wa malipo ya papo kwa hapo, sababu wakati mwingine wateja hawa wanakuwa wamehudumiwa na kituo husika cha kutolea huduma za afya lakini baadae fomu iyo inapowasilishwa kwa ajili ya madai huwa inakatwa bila kulipwa chochote au inalipwa baadhi tu ya huduma, lakini pia mfuko wa taifa wa bima ya afya unatoa malipo finyu kulinganisha na gharama za dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya vipimo zilizopo sokoni wakati huu na malipo kutokutoka kwa wakati.

USHAURI WANGU KWA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA
Mfuko wa taifa wa bima ya Afya hauna budi kuajiri wafanyakazi ambao watakaokuwa wanahusika na kuingiza madai ya kituo husika kwa muda husika na kwa kufanya hivyo itausaidia mfuko kupunguza ubadhilifu unaofanywa na baadhi ya vituo vya kutolea huduma za afya na hivyo kupunguza kadhia kwa mteja au mwanachama wa Mfuko huu.

Gharama ya kumuajili mfanyakazi katika taasisi hizi za kutolea huduma binafsi zinaweza kuonekana zipo juu lakini hii itasaidia kuokoa fedha nyingi iwapo wataandaa mazingira mazuri kwa waajiriwa hao kuwa waaminifu na wazalendo kwa mfuko na Taifa wa bima ya Afya.

Waongeze gharama za malipo ya huduma za matibabu na kulipwa madai hayo yanayowasilishwa kwenye ofisi zao kwa wakati.

Kupunguza au kuondoa kabisa baadhi ya makatazo ya huduma kulingana na hadhi ya kituo, kitu cha msingi ni kwamba wataalamu wanakuwa wanajua huduma ya mgonjwa huyu inahitaji rufaa na huyu anaweza kutibiwa hapa bila kujali hadhi ya kituo, mgonjwa aachwe ahudumiwe apo bila kujali hadhi ya kituo cha afya kama zifanyavyo bima nyingine za binafsi.
 
Back
Top Bottom