JamiiForums
JF Official Account
- Nov 9, 2006
- 6,202
- 5,012
Hoja hii ilianzishwa wakati JF ikiwa katika matengenezo hivyo tunairejesha kwakuwa haikurejea kikamilifu:
mukama talemwa said:Jana nilikuwa Shinyanga nikaona VX v8 yenye usajili NW NM (M) kuangakia kwenye gari kaka Stephen Masele ambaye ni juzi tu kaapishwa kuwa naibu Waziri wa madini.
Kitu ambacho sikubaliani nacho siku zote huyu bwana hapa Shinyanga ni Jimbo lake la uchaguzi kwahiyo kuna gari kakopeshwa kwa ajili ya jimbo lake, mafuta anapewa, dereva analipiwa, kwahiyo kuchukua gari la Serikali kwa matumizi ya jimbo lake siyo sahihi hata kidogo. Mbaya zaidi yeye kapanda ndege dereva wake kaendesha hilo gari hadi Shinyanga, kilometer za kutoka Dar hadi Shy ni kama 1000 Dereva analipwa night allowance.
Je, tutegemee jipya gani kwa mabadiliko haya ya uongozi kuapishwa tu, matumizi mabaya ya mali za umma yanaanza kwa kasi mpya. Au ni kuwakoga wananchi wa SHY maana hakuwa chaguo lao.