Matumizi fasaha ya maneno ya kiswahili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matumizi fasaha ya maneno ya kiswahili

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Babu Swahili, Jan 9, 2009.

 1. B

  Babu Swahili Member

  #1
  Jan 9, 2009
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimepewa taarifa na mjukuu'angu mmoja ya kwamba kuna uharibifu mkubwa sana wa lugha yetu ya kiswahili humu jamvini. Kwa hiyo nimekuja hapa kuwa adhibu wale wote wanaoharibu lugha yetu takatifu.

  Nikianzia na hawa hapa:

  Sio Mwulize, ni Muulize

  Sio Najuwa, ni Najua

  Endeleeni kuchambua mambo mbalimbali, lakini mjue ya kuwa nina macho makali sana ya kunasa kila uchafuzi wa lugha yetu.

  Ndimi Babu Mswahili
   
  Last edited by a moderator: Jan 13, 2009
 2. B

  Babu Swahili Member

  #2
  Jan 9, 2009
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni vizuri kuona kuwa umejirekebisha mwenyewe ulipotumia neno la ndio kwenye sentensi nyingine.
   
 3. B

  Babu Swahili Member

  #3
  Jan 9, 2009
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sio Kimejili, ni Kimejiri

  Ni Hicho
   
 4. B

  Babu Swahili Member

  #4
  Jan 9, 2009
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mjukuu wangu JMushi1, ni Nimetoa, na sio Nimetowa
   
  Last edited: Jan 10, 2009
 5. Suki

  Suki JF-Expert Member

  #5
  Jan 10, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 373
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mzee mwenzangu,
  Kwanza,ninafurahi sana kuona kitu hiki kinatendeka hapa jamvini.
  Sababu kuu ni kwamba,wengi wetu hujisahau na muda unapozidi kwenda,makosa haya huota mizizi na inakuwa vigumu kujirekebisha.

  Pili,naomba msaada kwenye sehemu hizi (kutoka kwenye bandiko lako hapo juu)

  Katika sentensi hiyo ya kwanza,ninaweza pia kutumia neno 'kwamba' bila kuweka 'ya' na ikaleta maana sahihi,si ndio?Sasa basi,kuna umuhimu gani kuwepo kwa 'ya'?Je?Kuna makosa yoyote iwapo ikitumika (kama ulivyofanya wewe)?

  Kuwaadhibu,labda?
   
 6. B

  Babu Swahili Member

  #6
  Jan 10, 2009
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shukrani mzee Suki,

  Utumiaji wa ya kwamba au kwamba unaleta maana ile ile. Kwa hiyo, utangulizi wa "ya" kabla ya "kwamba" ni uongezaji wa ladha kwenye sentensi tu.

  Mara nyingi tuna unganisha (tunaunganisha) maneno mawili na kuunda neno moja, kwa sababu uandishi wetu umejengwa na jinsi tunavyo ongea (tunavyoongea). Angalia mifano kwenye mabano. Sasa je sahihi ni "kuwa adhibu" au "kuwaadhibu," nafikiri hapo nitaomba msaada wa kuelimishwa hata mimi.
   
 7. Suki

  Suki JF-Expert Member

  #7
  Jan 10, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 373
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwa mtazamo wangu,kuunganisha au kutenganisha neno kunategemea sheria za lugha.Kwa mfano,neno ulilolitumia ''tunaunganisha'' hatuwezi kusema ''tuna unganisha'' kwani sheria za mnyambulisho wa neno hili haziruhusu.''Tuna'' ikitumika peke yake lazima ifuatiliwe na nomino.Kwa mfano;tuna watoto au tuna majukumu.
  Vinginevyo matumizi mengine ya ''tuna'' yanafuatana na sehemu nyingine za maneno bila kuachanishwa na maneno hayo.Vivyo hivyo katika neno kuwaadhibu na mengineyo mengi.

  Pia umegusia uandishi unaotegemea uongeaji wa mwandishi na sijaona kama hili ni tatizo katika muunganisho au mgawanyiko wa neno ingawa ni tatizo kubwa katika maeneo mengine mfano; ''kurikuwa'' badala ya ''kulikuwa'' na haya hujulikana kama makosa ya kimatamshi.
   
  Last edited: Jan 10, 2009
 8. M

  Mahmoud Qaasim JF-Expert Member

  #8
  Jan 10, 2009
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 922
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 60

  Hii ya kuakata maneno ni makosa makubwa.
  usahihi wake ni kuunganisha kama ulivyoweka sio ulivyo weka kwenye mabano.
  hebu niambie kama unaweza kutumia kama hivi: - mfano tunakwenda kazini haiwi sawa na kusema tuna kwenda kazini. tunakwenda ni neno moja kulikata ni makosa sawa na tunaunganisha ukasema tuna unganisha. neno tuna humaanisha kwamba msemaji akiwa yeye na wenzie kwa pamoja wanacho kitu cha pamoja, na kwa kawaida hufuatiwa na nomino mfano tutumie maneno yaleyale tunaunganisha ukilikata itatakiwa useme tuna unganisho( hapo tuna linamaanisha msemaji pamoja na wenzie wanalo unganisho yaani wanalojambo linalowafanya kuungana pamoja.unganisho limekuwa ni nomino).
   
  Last edited: Jan 10, 2009
 9. B

  Babu Swahili Member

  #9
  Jan 10, 2009
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana nanyi kabisa wajukuu zangu.

  Naombeni muungane nami katika harakati hizi za kunyoosha lugha yetu humu jamvini.

  Tuendelee....

  Sio Ikionesha, ni Ikionyesha
   
  Last edited: Jan 10, 2009
 10. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #10
  Jan 10, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,932
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Nadhani neno 'ikionesha' ni sahihi katika muktadha anaokusudia Mfumwa. Linatokana na neno 'ona'. Neno 'ikionyesha' kimantiki linatokana na neno 'onya'. Neno 'onya' lina maana ya kukanya. Katika muktadha wa Mfumwa, akitumia neno 'ikionyesha' haitaleta maana anayokusudia.

  Angalia maneno haya pia:
  'Maonesho' na si 'Maonyesho'
  'Onesha' na si 'Onyesha'
   
  Last edited: Jan 10, 2009
 11. Suki

  Suki JF-Expert Member

  #11
  Jan 10, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 373
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Babu ulivyokazania huo ujukuu!
  Ila ''kazana'' hii usiichukulie 'kimwinyimwinyi' maana watu wa lugha mh!
   
 12. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #12
  Jan 11, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Babu Mwanakijiji ni mwalimu wangu wa Kiswahili, na hayo uliyosema ni sawia na yale aliyonifundisha!

  Ni 'maonesho' na si 'maonyesho'
   
 13. B

  Babu Swahili Member

  #13
  Jan 11, 2009
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyie wajukuu mbona mwataka niadhiri babu yenu?

  Haya sasa, kwenye magazeti ya mzalendo huwa wanaandika "maonesho ya sabasaba" au "maonyesho ya sabasaba?"
   
 14. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #14
  Jan 11, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Babu, wanatakiwa waandike 'maonesho' na siyo 'maonyesho', ni makosa yaliyo ya kawaida na kuzoeleka, ndiyo maana wengi hatuoni kama kufanya hivyo ni makosa.
   
 15. B

  Babu Swahili Member

  #15
  Jan 11, 2009
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ha si wajua tena ukishakula chumvi nyingi, kila mtu wamwita mjukuu. Weye ulishasema ni mzee mwenzangu. Kwa hiyo heshima yako nakutumia.
   
 16. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #16
  Jan 11, 2009
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Babu,

  Kwa niaba yangu binafsi nakushukuru kwa ujio wako hapa jamvini,nadhani utasiadia sana katika kuboresha hii lugha yetu nzuri ya kiswahili na kwa kufanya hivyo sisi watumiaji tutarekebika katika maandishi yetu sawia na matamshi.

  Lakini Babu tatizo langu liko hapo juu,kwenye bandiko lako ulipodai kwamba ''hii lugha yetu takatifu''
  Tafadhali rekebisha au ni juze kuhusu hili la utakatifu wa kiswahili.

  Ni mimi Mjukuu wako kama sio Kikongwe mwenzio.

  SANDA
   
 17. M

  Maamuma JF-Expert Member

  #17
  Jan 12, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Hapa neno "tukufu" lingefaa zaidi. Labda kama Babu Swahili alikuwa na maana nyingine zaidi ya kuitukuza lugha yetu adhimu ya Kiswahili.
   
 18. M

  Maamuma JF-Expert Member

  #18
  Jan 12, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Sanda Matuta,
  Wewe binafsi unashukuru na si kwa niaba yako binafsi. Unaposema "kwa niaba" una maana ya kuwakilisha mtu mwingine lakini sio wewe mwenyewe. Huwezi kujiwakilisha kwa sababu ndiwe unayesema au kutenda - bila kuwakilishwa.

  ....ni juze... - ulikuwa na maana "nijuze", au?
  Naomba kuwasilisha.
   
  Last edited: Jan 12, 2009
 19. Mr Kiroboto

  Mr Kiroboto JF-Expert Member

  #19
  Jan 12, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 321
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  naona sasa wakati umefika kwa kila mmoja wetu kuhakikisha anatumia kiswahili fasaha.tupo pamoja katika hili
   
 20. B

  Babu Swahili Member

  #20
  Jan 12, 2009
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kutokana na utaalam wa mzee mwenzangu Suki, haya maneno yanapaswa kuunganisha na kuwa neno moja. Yaani Tunaamini.

  Swali hili halijakaa sawa...

  Kianzio cha Hivi hili kinalenga kwa Mzee Jasusi, Kongamano au Mzee Jasusi Kongamano?

  Swali hili lingepaswa kuwekwa hivi:

  Mzee Jasusi, hivi hili kongamano lilikuwa kwa ajili........?
   
  Last edited: Jan 12, 2009
Loading...