Matumbo Sumbufu au Irritable Bowel Syndrome (IBS) Ni nani anayeweza upata? IBS ni

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
Ni nani anayeweza upata?

IBS ni shida ya kawaida. Huwashika mtu mmoja kati ya watano. Huanza wakati wa ujana au kijana anapoingia utu uzima. Hata hivyo huweza kushika watu wa umri wowote ule.

Ni nini baadhi ya dalili za ugonjwa huu?

  • Kusokotwa na tumbo - Cramps
  • Kufunga choo
  • Kuendesha
  • Kushikia kuwa hujakamaliza kabisa kusukuma haja kubwa
  • Hewa nyingi tumboni
  • Kufura
  • Makamasi kutokea kwenye haja kubwa
Kinachosababisha huu ni nini?

Utumbo wako mkubwa (large Intestines) hunywa maji na chumvi yapatikanayo katika chakula ambacho ushakula wakati ambapo hicho chakula kimesafiri kutoka tumboni hadi utumbo wako mdogo. Iwapo utumbo wako mkubwa ni sawa na hauna shida yoyote, utapata haja yako kubwa bila shida yoyote. Kwa sababu zisizojulikana utumbo mkubwa wa watu wengine huwa unashindwa na vyakula vingine, jambo ambalo halisumbui watu wengine. Hii ni pamoja na mtu kushikwa na kunguruma kwa tumbo na kuendesha wakati wa au baada ya kula chakula.

Namna ya lishe na kuwa na mawazo vinaweza kusababisha hali hii au hata kulifanya iwe mbaya zaidi. Kwa wanawake IBS ni hali ambayo inaweza kuwa mbaya sana wakati wa hedhi sababu ya mabadiliko ya homoni za mwili. Wakati mwingine dalili za IBS zinaweza kujidhihirisha kutokana na maradhi mengine.

Namna ya kutibu

Unapomtembelea daktari au mhudumu wako wa kiafya, ataangalia historia yako ya kiafya. Atakagua mwili wako, damu na haja, akuchukue uyoka (x-ray) na kuchungulia sehemu ya utupu wa nyuma kwa kutumia mrija unaingizwa huko nyuma. Utapewa matibabu na dawa ambazo zitakusaidia.
 
Ni kweli hii kitu huwa inawakumba watu wengi ila ni ngumu kusema sababu inainvolve maeneo ya sirini.

Vitunguu swaumu na papai vinasaidia sana kutibu matatizo haya, pia juice ya ukwaju inasaidia kuondoa haya matatizo.
 
Inflamatory bowel disease(IBS) is a chronic inflamatory large intestine disease,whose aetiology is not known but sometimes the disease can progress to cancellous(malignant)
Symptoms(major)-maleina,chronic abdomen pain especially RLQ+LLQ,Dyspepsia etc
Diagnosis
-Barium enema
-colonoscopy
-Biopsy(FNAC)-histopathology r/o whether cancer or not
Cure....Broad spectrum antibiotics,can help to cure and Special diet

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom