Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,377
- 217,438
Tulifahamu tangu awali kwamba ccm ni ile ile , ila kuna tofauti kidogo kati ya viongozi wanaopewa Mamlaka na Chama hicho , kiongozi mwenye exposure hutofautiana kidogo uungwana na kiongozi wa kutoka porini , tofauti ipo ya namna ya kuhandle issues , kujua wapi aongee nini na wapi atishie watu, badala labda ya kukamata mwingine aweza kuonya tu na mambo yakasonga.
Lakini kwa kiasi kikubwa kwenye masuala ya haki za kikatiba ccm bado ni moja , hawataki usawa hata chembe , viongozi wote wa ccm hawataki katiba itakayoleta usawa ndani ya nchi wala hawataki Tume huru ya uchaguzi , pamoja na mama kuondoa baadhi ya uchafu uliofanywa na awamu iliyopita , ambao kwa kiasi kikubwa uliidhalilisha nchi na kuitia aibu duniani , lakini kimsingi hana tofauti kubwa na viongozi wengine wa ccm waliomtangulia.
Labda kwa kuwakumbusha tu ni kwamba Mama ni miongoni mwa watu wasiopenda kusikia habari ya serikali 3 , huyu alikuwa makamu Mwenyekiti wa bunge la Katiba , aliyesaidia sana kuinyofoa katiba yote ya Warioba na kupachika madudu waliyoyataka , Mwenyekiti alikuwa Samuel Sitta , kwahiyo huyu hakuwahi kuwa mwema kwa Taifa , bali ni mtu anayeuma na kupuliza , inawezekana katika uongozi wake akawa ana nafuu kuliko yule mkomoa watu , lakini kuhusu Katiba mpya tuendelee tu kupambana naye kama tulivyopambana na wengine.
Huwezi kushawishi wawekezaji wakubwa ikiwa hauna mifumo imara ya kisheria , mifumo hii inawekwa ndani ya Katiba , Katiba ya sasa ya Tanzania inamwezesha rais wake kufanya chochote bila kuhojiwa , ni mwekezaji gani mwenye akili timamu awezaye kuja kwenye nchi ya hivyo?
Inasikitisha tu kwamba imani ndogo aliyowapa Watanzania kwa siku 100 za mwanzo ameiteketeza kwa kauli ya dakika 1 tu ya KUENDELEA KUVUNJA KATIBA ALIYOAPA KUILINDA , huku akiwa kashika quran Tukufu mkono wa kulia .