Matumaini ya Wananchi waliowengi ni CHADEMA; CCM haiwezi kuruhusu uchaguzi huru na haki

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
CCM Ina watu wanamiliki kadi za chama Kwa usalama wao, Mali zao na jamaa zao lakini hakuna wanachama. Sirini hata wale waliopo karibu na Mwenyekiti wa chama Wana maamuzi Yao binafsi ambayo ni kinyume kabisa kile mwenyekiti anachodhani. Magufuli amegeukwa; hata walewachache waliojitumumua kumtetea akiwa hayupo na wao wamenyamazishwa Sasa wimbo unaosikika ni mmoja tu. Je wanavyoimba ndivyo wanavyotafakari na kufikiri?Vinyonga

Kwa upande Mwingine CHADEMA Ina watu wachache wanaomiliki kadi za chama lakini Ina watu wengi wanaoamini katika itikadi ya Chadema. Wale wote wanaoamini Kwamba Taofa limekuwa Mali ya familia flani wanaamini wao Wana haki pia yakutumia muda waliopewa na Mwenyenzi Mungu kulitumikia Taifa.. wanatamani mfumo rasmi utakaruhusu competition Ili wanapozaa watoto wenye akili na uwezo wa kuongoza basi waruhusiwe kuongoza. Wanatambua walizaliwa kuendeleza Tanzania na siyo kusomamiwa na watu wenye maslahi na familia zao.

Wanaamini Mali za Dunia zinapita hivyo wanapaswa kuweka hazina kwenye miyoyo ya vizazi vijavyo kama alivyofanya Nyerere.

Wanakerwa Sana kusikia Watanzania wanaoiba pesa nchini na kuzipeleka kuzihifafhi kwenye mabenki huko Ulaya ndio wanaoongoza sekta nyeti. Watu Hawa ni wengi wanahitaji mfumo tu waweze kuivusha Nchi.

Unapokuwa na KUNDI linalowaza familia against KUNDI linalowaza maslahi mapana ya Nchi basi tambua kura ni Siri na endapo kiongozi atataka kubeti basi abeti kwenye uchaguzi huru na haki.

Watanzania Sasa wanaelewa wanavyoibiwa na wanatamani kuhitimisha maisha haya yakuelekezwa Nani aongoze.
 
Back
Top Bottom