Matumaini ya wafanyakazi yazikwa: Serikali yagoma kurekebisha sheria ya fao la kujitoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matumaini ya wafanyakazi yazikwa: Serikali yagoma kurekebisha sheria ya fao la kujitoa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Conquerer, Oct 17, 2012.

 1. T

  The Conquerer Member

  #1
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ndugu wafanyakazi na watu wote wenye mapenzi mema mliojiunga na mifuko mbali mbali ya hifadhi za jamii kwa lengo la kujiwekea akiba ya siku zijazo; Serikali yenu imepuuzia maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ambayo yaliitaka Serikali kuleta mara moja muswada wa marekebisho ya sheria kandamizi iliyofuta kinyemela haki ya fao la kujitoa katika mifuko ya jamii. Serikali pia imepuuzia maagizo ya Spika wa Bunge ya kuitaka Serikali ilete muswada wa marekebisho ya sheria ya hifadhi za jamii hususan fao la kujito kwa hati ya dharura katika mkutano wa bunge wa Novemba 2012.

  SERIKALI IMEJIBU RASMI KWAMBA MUSWADA HUO HAUTALETWA KATIKA BUNGE LA NOVEMBA, 2012. HIVYO MATUMAINI YA WAFANYAKAZI YAMEZIKWA NA HATIMA YA MAFAO YA WAFANYAKAZI HAIJULIKANI. Napenda kuwahakikishia vilevile kwamba Mbunge wa CCM, Mh. Jafo hana nia ya dhati ya kuwatetea wafanyakazi kwa kuwa anatumika na Serikali yake ya CCM kuchelewesha mchakato wa kuleta muswada binafsi ili haki za wafanyakazi zilizopora zirudishwe.

  Hakuna Shaka kwamba hoja ya fao la kujitoa ni hoja ya kambi ya upinzani na ndio maana katika hotuba ya Waziri Kivuli wa Kazi katika bunge la bajeti 2012, Jambo hili lilizungumziwa kwa ufasaha kabisa. Hivyo sioni haja ya Mh. Jafo kuitisha mazungumzo na waandishi habari na kujigamba kuwa hoja hii ni yake.

  HAPA NI SEHEMU YA HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU KAZI NA AJIRA: (Fao la Kujitoa limezungumziwa)

  3.0 MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII Mifuko ya Hifadhi za Jamii nafao la kujitoa.Mheshimiwa Spika.

  kwa mujibu wa Ilani ya uchaguzi ya CCM (2010-2015) kifungu cha 81 kinazungumziaHifadhi ya Jamii na katika Kamusi ya utekelezaji wa ilani ya CCM iliyotolewa naWaziri Mkuu inaeleza kwa kina kuwa ili kutekeleza ilani hiyo Serikali ilipaswakufanya mambo yafuatayo;
  · Zitafanyika tathimini za kina kwenyemifuko ya hifadhi za jamii na kurekebisha viwango vya mafao vinayotoa ilivisipishane sana ,· Kuanzisha na kuimarisha mamlaka yauthibiti na usimamizi wa sekta ya Hifadhi ya Jami·

  Kuchukua hatua za makusudi zakupanua wigo wa kinga ya Hifadhi ya Jamii, ili watanzania walio wengi wawezekufaidika
  Mheshimiwa Spika,pamoja na ahadi hiyo ya Ilani ya CCM , taifa lilishuhudia serikali ya CCM mnamotarehe 13 Aprili 2012 ikipitisha Sheria na Bunge hili baada ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho yaSheria za Hifadhi za Jamii (TheSocial SecurityLaws (Amendments) Act, 2012), pamoja na marekebisho yake kusomwa kwamara ya pili, ambayo pamoja na mambo mengine imesababishausumbufu mkubwa sana kwa wafanyakazi hasa walioko kwenye Sekta binafsi na waleambao wanafanya kazi kwa mikataba.

  Mheshimiwa Spika,wakati waziri wa kazi na ajira anawasilisha mswada huo kusomwa kwa mara ya pilialisema "Mheshimiwa Mwenyekiti, Muswada huuunakusudia kufanya marekebisho katika Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, kwamadhumuni ya kuiwezesha Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii,kufanya kazi yake kikamilifu na kusimamia na kudhibiti Sekta ya Hifadhi yaJamii. Muswada umeandaliwa kwa kuwashirikisha Wadau wote wa Sekta ya Hifadhi yaJamii, wakiwemo Wafanyakazi, Waajiri na Serikali, ikiwemo Mifuko yenyewekupitia Vikao vya Wadau na pia Baraza la Kazi , Uchumi na Jamii yaani LESCO. Kimsingi, wadau wote waliunga mkonomapendekezo yaliyomo katika Muswada huu".

  Mheshimiwa Spika,taarifa ya Waziri kuwa mswada huu uliwashirikisha wadau na hasa wafanyakazi sioza kweli kwani baada ya sheria hii kupitishwa tumeshuhudia wafanyakazi wakiilalamikia na kwa mujibu wa barua ya SSRA ilikiri wazi kuwa watawashirikisha
  wafanyakazi kwenye zoezi la kutunga kanuni , na huu ni uthibitisho kuwa taarifaya waziri Bungeni haikuwa sahihi.


  Aidha Wazirialisema"Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu hii pia inaweka majukumu ya mwajiri, ikiwa nipamoja na kusajili wafanyakazi wapya kwenye Mfuko huu wa PPF kwawale ambao si wanachama wa Mfuko wowote na kuwasilisha michango kamili yawafanyakazi, pale ambapo wafanyakazi hao wamesimamishwa kazi kwa nusu mshahara. Aidha, marekebisho hayo yameweka wazi umri wa kustaafu kwa hiari kwa mwanachamakuwa ni kuanzia miaka 55, isipokuwa uanachama wake utakoma pale ambapomwanachama huyo atatimiza umri wa miaka 60. Inapendekezwa pia kwamba,mwanachama ambaye hajatimiza muda wa kuchangia, yaani qualified period, anapostaafu apewe michango yake na ya mwajiri pamoja nariba".


  Mheshimiwa Spika,
  kwa mujibu wa kumbukumbu rasmi za Bunge (hansard) zinaonyesha kuwa kifungu chakuzuia fao la kujitoa kilihusu mfuko mmoja wa PPF na sio mifuko yote kamaambavyo SSRA ilivyosema kwa mujibu wa barua yake kwa Makamu wa rais wa AfricanBarrick , Kinachohusiana na fao la kujitoa cha mswada huu uliwasilishwa Bungenikatika hatua ya tatu kama "schedule of amendments" ambayo iliwasilishwa naSerikali na haukuwepo kwenye mswada uliosomwa kwa mara ya kwanza mwezi Februari2012, na mara ya pili hapa Bungeni na wala Kamati ya Kudumu ya Bungehaikujadili wala kutolea maoni kifungu cha fao la kujitoa.


  Mheshimiwa Spika,
  uthibitisho kuwa kifungu husika cha "fao la kujitoa" hakikujadiliwa nipamoja na taarifa ya kamati ya kudumu ya Bunge , Kambi ya upinzani na hatawakati wa mjadala hakuna hata mmoja miongoni mwao ambaye alizungumzia kifunguhicho na hii ni kutokana na Serikali kuwasilisha schedule of amendment wakatibunge likiwa limekaa kama kamati na kupitisha vifungu hivyo jambo ambalo nikinyume na kanuni za kudumu za Bunge kifungu cha 88 kinachoelezea jinsi yakujadili na kupitisha majedwali ya mabadiliko.


  Mheshimiwa Spika
  ,kutokana na sababu hizo ndio maana Kambi ya Upinzani inaamini kuwa ni sahihikwa Bunge hili kujadili kwa kina suala hili kupitia kwenye mswada wa mabadilikona ili tuweze kuwatendea haki wafanyakazi ambao wapo kwenye sekta binafsi ,Serikalini na wale ambao wapo kwenye ajira za mikataba .


  Mheshimiwa Spika
  ,wakati kamati ya Bunge ikitoa taarifa yake kuhusiana na mswada huu wa sheriailisema, naomba kunukuu "Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, Kamati inaamini kuwa, Muswadahuu umebeba maoni mengi ya wadau na bila shaka utakapokuwa Sheria kamili,Kamati inaishauri Serikali, Kanuni zitakazotungwa zizingatie maoni ya Wadau naendapo kuna maeneo yanayohitaji marekebisho, Serikali isisite kuleta mabadilikombele ya Bunge hili".
  Kambiya upinzani,inakubaliana na maoni ya kamati na hivyo sasa ni wakati muafaka wa marekebishoya kifungu hiki kwa maslahi ya wafanyakazi na nchi yetu kwani jambo hililikiachwa bila utatuzi litaanza kutishia wawekezaji na uwekezaji kwenye sektaya madini na tunaamini kuwa baadhi ya sekta nyingine nyingi nazo zitaathirika.

  Kwakuwa tunazijua kanuni za Bunge kuwa huwezi kurekebisha kifungu cha sheria kwakutumia hoja binafsi , ndio maana tunaunga mkono hoja ya Mhe.Mnyika yakuwasilisha mswada binafsi kwa hati ya dharura kutokana na unyeti wa sualahili.Mheshimiwa Spika, aidha tunaelewa kuwa Pensheni ni suala la msingisana na hatuwezi kuwaacha wazee wetuwaishi bila Pensheni , vilevile tunatambua kuwa kuna mahitaji ya sasa ambayohayasubiri mpaka mtu azeeke ndipo aweze kuyatatua ndio maana tunaunga mkonowafanyakazi katika kupata fao la kujitoa na tunapendekeza sheria irekebishwe nakuzingatia yafuatayo;i.

  Michangoya wanachama (Employees contribution)iruhusiwe kutolewa namwanachama pindi anapoacha kazi,kufukuzwa kazi ama mkataba wake kumalizika, ilamichango ya waajiri (Employerscontribution) isiruhusiwekuchukuliwa kabla ya mwajiriwa kutimiza umri wa kustaafu kisheria .
  ii. Uanzishweutaratibu wa kuwa na mafao kwa wanachama ambao ama wamekosa kazi kutokana nasababu mbalimbali (Unemployment benefits)kama vile kumalizika kwa mkataba , kuachishwa kazi,kufukuzwa kazi nk kwakipindi cha miezi sita mwanachama wa mfuko husika aweze kulipwa kiasi cha mshahara kamili na miezi sita minginekama hajapata kazi alipwe nusu mshahara namfuko na baada ya mwaka mmoja kama atakuwa hajapata kazi basi mfuko uachekuendelea kumlipa mwanachama huyo.

  Mifuko itenge fungu maalum kwa ajili yakulipia mafao hayo.
  iii. Mifukoitenge fedha kwa ajili ya masomo (Educationfund) kwa ajili ya wanachama wake pindi watakapokuwa wanaenda masomoniwakiwa ni wanachama wa mfuko ,hii itawafanya wanachama kuweza kujiendelezakielimu na hivyo itapunguza idadi yawanachama ambao wanajitoa kwa ajili ya kupata fedha za kusoma.

  Mheshimiwa Spika, aidha Kambirasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kurejea pendekezo letu tuliloishauri katikabajeti ya Wizara hii ya mwaka 2011/2012 katika kuona umuhimu wa kuiunganishamifuko yote ya hifadhi za jamii na kubaki katika wizara moja ambayo ni ya Kazina Ajira. Kambi rasmi ya Upinzani inasisitiza kuwa lengo kuu la kuunganishamifuko hii ya hifadhi za jamii ni katika kuirahisishia Mamlaka ya Usimamizi naUdhibiti wa Hifadhi za Jamii (SSRA) katika kutekeleza Sheria moja na kuundavifungu sawa vya kisheria vitakavyosimamia utekelezaji na uendeshaji wa mifukohii ambapo kwa sasa mifuko hii imekuwa chini ya wizara tofauti na hivyo hatautekelezaji wake unakua mgumu na kuleta ukinzani kwa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi za Jamii.

  Tunasisitiza kuwapendekezo letu ni kuifanya PPF na NSSF iunganishwe na kuwa mfuko mmoja kwaajiliya Sekta Binafsi vilevile LAPF,PSPF na GEPF iunganishwe na kuwa mfuko mmoja kwaajiliya Sekta ya Umma. Pia, kambi ya Upinzani inapendekeza mifuko yote isimamiwechini ya Wizara ya Kazi na Ajira.
  Mheshimiwa Spika,kifungu hiki kinathibitisha taarifa za ukaguzi wa CAG kuwa mifuko hii ipohatarini kufilisika kutokana na miradi iliyowekeza kushindwa kurejesha fedhazake na pia Serikali kuangalia miradi hii kama uwekezaji wa mifuko husika na simikopo kwa Serikali kama ambavyo mifuko inatafsiri.

  Mheshimiwa Spika,
  Katika muendelezo wa kaguzi za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali,taarifa zinaonesha kuwa uwekezaji uliofanywa na NSSF, CAG aligundua mapungufukadhaa katika usimamiaji wa uwekezaji wa mifuko ya hifadhi za jamii ikiwemoNSSF ambayo hajasaini makubaliano na Serikali ya kuwezesha kifedha Ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma kwa awamu yapili. NSSF ilitumia jumla ya shilingi 234,054,000,000 kwenye mradi wa ujenzi wachuo hiki lakini ilisaini makubaliano kwa awamu ya kwanza wa shilingi 35,218,000,000. Ingawa majengo haya yalianza kutumika Septemba 2008 lakini mfukohaujaanza kupata marejesho ya mkopo kutoka Serikalini ambao umeshafikia riba yakiasi cha shilingi 14,157, 000,000.

  Mifuko mingine ambayo imewekeza katikaujenzi wa chuo kikuu cha Dodoma inajumuisha mifuko ifuatayo: PPF imewekezajumla ya shilling 39,987,406,969.60, PSPF shilingi 105,921,805,194, LAPFshilingi 22,030,753,000 na NHIF shilingi 13,403,753,000.
  [1]

  Mheshimiwa Spika,pamoja na mradi huo wa ujenzi wa chuo kikuu cha Dodoma ambao bado NSSF na mifuko mengine haijakusanyamarejesho yake, bado mifuko hii imeendelea kuwekeza katika miradi mikubwaambayo nayo pia imekuwa hairejeshi fedhakama ambavyo makubaliano ya mikataba ya mifuko hii na Serikali inaelekeza. Chakusikitisha ni kuwa, NSSF imeanza awamu ya pili ya ujenzi wa UDOM bila ya kuwana mkataba na serikali , hivyo haki na wajibu wa pande zote mbili haijulikani.

  Kambi rasmi ya Upinzani inaitakawizara hii kutoa maelezo juu ya uwezo wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti waMifuko ya jamii katika kusimamia mifuko hii ili kuhakikisha kuwa mifuko hiiinawashirikisha wanachama wake na pia mifuko inafuata sheria katika kuwekezakwenye miradi.


  Mheshimiwa Spika,
  kutokanana taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti mkuu wa Serikali imeonesha kuwa Mfuko wahifadhi ya jamii umewekeza hisa katika vitega uchumi vitano bila ya kuwepo namatarajio ya kupata gawio kwa siku za baadae na hivyo kuwa hatarini kufilisika.

  Mheshimiwa Spika,imefika mahali sasa lazima Serikali ikiri kuwa imekuwa ikiitumia baadhi yamifuko ya hifadhi za jamii kama njia mojawapo ya kutekeleza ahadi zake kemukemuzilizoahidi wakati wa chaguzi za wabunge na Urais ikiwemo uwekezaji wa mifukohii katika miradi mikubwa, kwa mfano ujenzi wa Daraja la Kigamboni na mradi wauzalishaji wa umeme katika eneo la Mkuranga, ujenzi wa jengo la Mzizima jijiniDar Es Salaam, ujenzi wa Jengo la Maadili, kuendeleza Ujenzi wa makazi ,biashara na ofisi katika eneo la Mchikichini, hii ni baadhi ya miradi michacheya uwekezaji ambayo Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF) imewekeza .

  Mheshimiwa Spika
  ,pamoja na kushindwa kwa baadhi ya miradi ya uwekezaji wa mifuko hii lakini badomifuko inaendelea kuwekeza katika miradi mikubwa bila kuzingatia hitaji lawanachama wa mifuko husika, hivyo inapelekea usumbufu na hata ucheleweshaji wamalipo ya mafao ya hifadhi za jamii kwa wanachama wake. Kambi rasmi ya Upinzaniinataka kujua kiasi cha faida ambacho baadhi ya miradi ya mifuko ya hifadhi zajamii imepata kutokana na uwekezaji wa miradi hiyo ? Na kama la! hakuna faida, nihasara gani imetokana na uwekezaji kwenye miradi hiyo? Je ni kwa kiasi ganihasara hizo za uwekezaji kunaathiri hifadhi za wafanyakazi ambao ndio chanzocha mapato kwa mifuko hii? Na kama kuna hasara za uwekezaji, kwa kuwa mifukohii imewekeza bila kupata maoni ya wafanyakazi wanaochangia, ni hatua gani zakisheria Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi za Jamii itaichukuliamifuko hii?

  Kambi rasmi ya Upinzani,inaitaka mamlaka ya Usimamizi naUdhibiti wa mifuko ya hifadhi za jamii kuizua mifuko ya hifadhi za jamiikuwekeza katika miradi mingine mikubwa mpaka pale itakapotoa taarifa za faidana hasara za mifuko ambayo imewekeza kwenye miradi hii na hajiarejesha faidakama ilivyotarajiwa.
  Mheshimiwa Spika, Kambiya Upinzani inasisitiza kuwaipohaja kubwa ya kuzipitia sheria za usimamizi na udhibiti wa mifuko ya hifadhi zajamii na kudhibiti kwa faida ya wanachama wake na ustawi wa taifa kwa ujumla.


  [HR][/HR][1]Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi: Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu zaSerikali kuhusu ukaguzi wa Mashirika ya Umma kwa mwaka wa Fedha wa 2009/2010
   
 2. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hii ndio TZ bana wabunge waliowengi wanaelekea 60 unategemea nini?

  TZ ni ya viongozi wa binafsi na wanafki sana!

  Muda wa kustaafu ulikuwa 55 wameongeza hadi 60 ubinafsi mtupu, utashangaa sasa hivi wanaongeza hadi 70 hawachelewi hawa.
   
 3. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  aaah masikini senti zetuu. ndugu wafanyakazi wa tz tusikubali kabisa.
   
 4. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  hichi ndicho kitakuwa kifo halali kwa ccm, na kuusuport upinzani wowote utakaoturudishia fao la kujitoa, silly government! i hate ccm, i hate mr.president.
   
 5. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Michango yetu,serikali itulazimshe kuchukua mafao baada ya kufikisha miaka 50!! 2015 mtaisoma Air chadema.
   
 6. bona

  bona JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2012
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  nadhan wafanyakazi wote tunajua haki yetu haitapatikana bungeni bali kwenye sanduku la kura uchaguzi ujao!
   
 7. Mandingo

  Mandingo JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 3,380
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 180
  Naanza kampeni mapema kabisa kama wengine walivyo tangaza nia ya kugombea!hapa ofisini wote lazima wawe upinzani nasema hakya Mungu!yaani hadi nifikishe 55!na kwanza ndio naanza kaajira!!!wana wazimu hawa!
   
 8. papason

  papason JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Kulalama lalama tuu hakusaidii!
  Sijui wafanyakazi tunangoja nini kuingia mabarabarani?
  Kama kuna mtu yoyote anayefikiria hii sirikali ya wamagamba inaweza kulirudisha fao la kujitoa kirahisi rahisi mtu huyo atakuwa mweu!
   
 9. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Haya ndio matunda ya CCM, Watanzania kazi yao ni kulalamika hawajui hata kuingia mitaani na kumfukuza huyu Vasco na serikali yake ya kibabiloni kama walivyofanya waarabu
   
 10. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mr President is powerless
  Mr president is promiseless
  Mr President is trustless
  Mr president is clueless
  Mr president is ..........I feel bad, am about to vomit my kuku which I ate now...He is speakless, He is...oogh my God!!!!!!!! Was he a Trade Unionist before?..
   
 11. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #11
  Oct 17, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Walicheza na madr na walimu sasa wamekuja kwa wafanyakazi ivi hawajui kundi la wafanyakazi ni kubwa ambamo walimu na madr ni kama subset tuu
  Naona Serikali ina hamu na machafuko
   
 12. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #12
  Oct 17, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  mimi ofsini kwetu nilishaharibu vibaya sana...no more gambaz
   
 13. j

  jruru80 Senior Member

  #13
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanazitaka hizo pesa kwa ajili ya kampeni zao labda...si unajua 2015 haipo mbali
   
 14. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #14
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  hivi kikwete na kibaraka wake irene isacka wanatutaka nini lakini! jamani tuingieni mabarabarani, hakika huu ni u.s.e.n.g.erema ULIOTUKUKA!! yaani TUKIAMUA TUNAWEZA, NA CHAMA CHA WAFANYAKAZI KIFE, WANAKULA KODI ZETU BURE, PATHETIC! I HATE CCM, I HATED IT LONG TYM AGO, AND I WILL ALWAYS HATE IT! NONSENSE!
   
 15. Lastname

  Lastname JF-Expert Member

  #15
  Oct 17, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 925
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mnamchukia tu muislamu mwenzetu nyie, mwacheni afanye maamuzi mbona ni swala dogo hilo mnampaka matope? kwani amewanyima pesa zenu si mkifikia 60 mtapewa?
   
 16. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #16
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  UKICHANGANYA NA MACHAFUKO YA UDINI! TANZANIA WATABAKI SAMAKI TU MAJINI, HATA WANYAMA MIKUMI WATATEKETEA NASI! YOTE HII NI SABABU YA kikwete, huyu ****** huyu, sina hamu naye!
   
 17. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #17
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  nasikia toka una mwaka mmoja, ulianza kukalia vitu vyenye ncha kali!!! achana na sisi, hata hiyo 60 tukifika asitupe, akae nazo, zitampeleka peponi! mfyuuuuuuuu!
   
 18. S

  SAJIGWA NIKUPALA New Member

  #18
  Oct 17, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kwa kweli inasikitisha! hivi ni kwa nini mswada huu unakuwa na matatizo? au ni kimradi cha mtu?
   
 19. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #19
  Oct 17, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Poor Tanzania
   
 20. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #20
  Oct 17, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  kidumu chama cha mapinduzi.....

  Ccm oyeeeeeeeeeeeeeeeee
   
Loading...