Matumaini ya kutokuibiwa kura yametokea - bado swali moja dogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matumaini ya kutokuibiwa kura yametokea - bado swali moja dogo

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mtaka Haki, Oct 16, 2010.

 1. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  HABARI ZILIZOANDIKWA KATIKA MAGAZETI MBALIMBALI LEO ZINAONYESHA KUWA KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU KITASAMBAZA WAANGALIZI HURU NA KUJUMLISHA MATOKEO. KILA MKOA KITAKUWA NA MWANGALIZI MMOJA. KULINGANA NA HABARI HII HAPA CHINI INAONEKANA WAANGALIZI NI 1744. Swali dogo je vituo vya kupiga kura mwaka huu ni vingapi kama idadi hiyo ni sawa na ya vituo vilivyoko basi matumaini yetu ni makubwa.
  Hongereni sana.


  HRC kusambaza waangalizi majimboni
  NA RICHARD MAKORE
  16th October 2010
  B-pepe
  Chapa
  Maoni

  Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)
  Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa ndani wanatarajia kuanza kusambaza katika majimbo mbalimbali kunzia Jumatatu ijayo.
  Kaimu Mkurugenzi wa Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Katemana, alisema jana kuwa waangalizi hao wanafikia 1,744 na watakuwa katika mikoa, majimbo na kwenye vituo vya kupigia kura.
  Waangalizi hao wameteuliwa na mtandao wa Asasi za Kiraia (TACCEO) unaoundwa na mashirika 17 ambapo watatumia kompyuta na simu za mkononi kufanya kazi hiyo.
  Kadhalika, mtandao huo umeandaa utaratibu utakaowawezesha wananchi kutuma ujumbe mfupi wa simu (SMS) kwa waratibu wa kitaifa watakaokuwa Dar es Salaam kupitia namba 15540 kwa mitandao ya Vodacom, Tigo, Zain na Zantel ili kutoa taarifa kwao juu ya mambo mbalimbali yatakayotokea katika vituo vya kupigia kura.
  Waangalizi hao watasambazwa katika mikoa yote ya Tanzania bara na Zanzibar kwenye majimbo na vituo vyote vya kupigia kura.
  Katemana alisema waangalizi 270 watakuwa katika majimbo na kila mkoa utakuwa na mratatibu mmoja ambaye atakuwa anaratibu shughuliz zote za uangalizi na kutoa taarifa makao makuu ya mtandao huo yatakayokuwa jijini Dar es Salaam.
  Asasi hizo za kiraia ni pamoja na Tamwa, SAHRINGON Tanzania, WLAC, TANLAP, WILDAF, ForDIA, Haki Madini, MPI, ACCORD, ZLSC, PF, Tahurifo, YPC, LEAT na LHRC.
  Alisema TACCEO imepata kibali cha kufanya kazi hiyo kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kwamba lengo la uangalizi huo ni kuanisha mapungufu yatakayojitokeza wakati wa Uchaguzi Mkuu 2010.
  Kwa mujibu wa Katemana taarifa zitakazokusanywa nchi nzima na kuchambuliwa ili kuweka kumbukumbu na rejea ili ziweze kusaidia kuboresha Uchaguzi Mkuu siku zijazo.
  Maeneo mengine yatakayoangaliwa na waangalizi hao ni pamoja na kiwango cha wananchi kuelewa masuala ya uchaguzi, elimu ya uria kwa wananchi, ushiriki wao, ushiriki wa wadau mbalimbali kama Nec, vyomb o vya habari, vyombo vya usalama na Asasi za kiraia zinavyoelimisha jamii.
  CHANZO: NIPASHE
  0 Maoni | Kuwa wa kwanza kutoa maoni
   
 2. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Hongereni sana.
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Hii itasidia kwa kiasi fulani naiyo namba nishaisave
   
 4. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #4
  Oct 16, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Je kuna mwenye idadi ya vituo vya kura nchi nzima? Tunaweza kuwashauri kama idadi ya vituo ni nyingi kuliko idadi ya watu.
   
 5. K

  King kingo JF-Expert Member

  #5
  Oct 16, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 401
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  vituo vya kupigia kura viko vingi kuliko hiyo idadi ya hao wasimamizi nadhani vituo viko 50,000 na zaidi kama sijakosea ila hata hivyo wamejitahidi sana
   
 6. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #6
  Oct 16, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna mwenye taarifa kamili. Tunaweza kuwaomba wakubali watu watakao vulunteer bila ya kulipwa. Wako watu waaminifu katika kila mkoa. Wako wanafunzi wa vyuo vikuu amabao hawapigi kura wengi wao
   
 7. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #7
  Oct 16, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu awajalie baraka. God Willing Tanzania itazaliwa upya! Mbona nitajivunia kuitwa Mtanzania na kutembea kifua mbele
   
 8. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #8
  Oct 16, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Kidogo itasaidia ila bado mianya ipo ya udanganyifu!
   
 9. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #9
  Oct 16, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  nazidi kupata matumaini makubwa juu ya ushindi wa SLAA maana uchakachuaji ungetudhulumu ila kama wameamua kusaidia hivyo tumefurahi
   
 10. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #10
  Oct 16, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Sina hakika na idadi ila niliwahi kumsikia Kiravu akisema kila kituo kitakuwa na wapiga wasiozidi 500. Akasema kwa idadi hii siyo rahisi kuiba kura
   
 11. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #11
  Oct 16, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  NEC wanaweza kuwakatalia
   
 12. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #12
  Oct 16, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Eneo moja mfano shule moja inaweza kuwa na vituo hata 20 yaani kila darasa ni kituo A,B,C,D,E,F.......kwa hiyo mwangalizi mmoja anaweza kuzungukia vituo hivyo vyote bila shida.
   
 13. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #13
  Oct 16, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  vituuo vya kupigia kura vpo 57000
   
 14. d

  d-walter New Member

  #14
  Oct 16, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dhahiri kama ndivyo itakavokuwa basi itasaidia lakini mi nina wazo moja kwa wenzangu wanaJF kuwa mara nyingi mambo mazuri hayapatikani kwa kujiweka kando,bali kujitoa kwa moyo mmoja,kuvumilia kashikashi na kuwa na imani kuwa lile tunalo amini linawezekana.
  Binafsi ningependa mambo yafuatayo tuyafanye:-
  a)kuhakikisha watu ambao tunadhani wanamsukumo wa mabadiliko wakapige kura
  b)Tuwe wawazi kwa watanzania wenzetu juu ya hisia zetu juu ya mstakabali wa
  nchi yetu kwa kulinganisha mahitaji na maisha tulonayo sasa.
  c)Pia siku ya kupiga kura tukae mita 200 ili kulinda kura zetu na wale ambao ni
  mawakala wetu(chadema) ikibidi tuwape motisha na kuwaeleza tuko nyuma yao,wasiwe
  na mashaka hii pia itakuwa nafasi nzuri katika kuhakikisha kura zetu zinalindwa vizuri.
  d)Kumshirikisha MWENYEZI MUNGU katika kile tunachoamini ni sahihi na kumwomba pia
  asaidie kukilinda maana yeye hakuna limshindalo.
  Ni imani yangu kuwa hili tutaliweka katika kumbukumbu zetu.
   
 15. giraffe

  giraffe JF-Expert Member

  #15
  Oct 16, 2010
  Joined: Jun 6, 2010
  Messages: 504
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Lakini anayetangaza mshindi ni NEC kumbuka kuhesabu kura na kutangaza mshindi hapa kwetu ni vitu viwili tofauti.
   
 16. n

  nyuki dume JF-Expert Member

  #16
  Oct 16, 2010
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 438
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Njia ya muongo ni fupi
   
 17. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #17
  Oct 16, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  hapa na mimi ndo nlipokuwa nawaza!!
   
 18. B

  Bio New Member

  #18
  Oct 16, 2010
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa ufisadi huu hiyo namba itakuwa haifanyi kazi siku ya uchaguzi.
   
Loading...