Matukio yasiyosahaulika aliyoyafanya dikteta Idd Amin Dada

AbouZakariya

JF-Expert Member
Mar 19, 2013
1,445
2,000
Na kula nyama za watu je?
Witness hizi zote ni propaganda si kweli kwamba amin alikula nyama za watu, ni uzushi tu wa wale wapinzani wake.
Kuhusiana na na ombaomba hawakumwagwa ziwani kama baadhi ya wapotoshaji wasemavyo, bali kilichotokea ni kwamba aliwahamisha mjini kampala kwa muda kwani kulikuwa na mkutano mkubwa wa baadhi ya viongozi wa afrika, kwa kuogopea aibu hiyo kutoka kwa wageni wake ndipo akaamua kiwahamisha kwa muda mjini kampala.
 
witnessj

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
25,015

Duuh basi binadamu waongo sana
 
AbouZakariya

JF-Expert Member
Mar 19, 2013
1,445
2,000
Duuh basi binadamu waongo sana
Ni waongo mno, na haswa unapokuwa mpinzani wao watakuzushia vingi mno, nilibahatika miaka ya 2005/2006 kuwa kampala nakumbuka kuna siku ilitoka habari ya mahojiano baina ya mwandishi wa kama sijasahau Daily Nation au gazeti jengine na aliyekuwa mpishi wa field marshal Idd Amin, katika yale aliyoulizwa ilikuwa ni hili swala la Amin kula nyama za watu, mpishi alijibu, si kweli Amin hakuwahi kufanya hivyo, wacha hili kuna mengine mengi yalizushwa lakini si kweli,
Jambo moja wengi tunasahau, kiongozi hata awe mpole vipi ukitia mchanga kitumbua chake hakuachi ng'o lazima akuadabishe, basi na Amin nae alikuwa kiongozi na kuna watu vimbelembele walitaka kutia mchanga kitumbua chake hakuwaacha alipita nao.
 
Santee sana mkuu Kwa maelezo yako mazuri
 
The Sun-of-a Beach

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
1,215
2,000
Ni waongo mno, na haswa unapokuwa mpinzani wao watakuzushia vingi mno, nilibahatika miaka ya 2005/2006 kuwa kampala nakumbuka kuna siku ilitoka habari ya mahojiano baina ya mwandishi wa kama sijasahau Daily Nation au gazeti jengine na aliyekuwa mpishi wa field marshal Idd Amin, katika yale aliyoulizwa ilikuwa ni hili swala la Amin kula nyama za watu, mpishi alijibu, si kweli Amin hakuwahi kufanya hivyo, wacha hili kuna mengine mengi yalizushwa lakini si kweli,
Jambo moja wengi tunasahau, kiongozi hata awe mpole vipi ukitia mchanga kitumbua chake hakuachi ng'o lazima akuadabishe, basi na Amin nae alikuwa kiongozi na kuna watu vimbelembele walitaka kutia mchanga kitumbua chake hakuwaacha alipita nao.
Tuamini ya nani na tuyaache ya nani?

1.Henry Kyemba,aliyewahi kuwa Waziri wa Afya wa Uganda enzi za utawala wa Iddi Amin,anakiri kuonyeshwa na Amin kichwa cha mhanga mmoja wa mauaji kikiwa kwenye fridge.Habari hii ipo kwenye kitabu cha The State Of Blood alichoandika Henry Kyemba as an eye witness.

Henry ameandika mengi ikiwemo mauaji ya Bishop Janan Luwum,Dr.Benedicto Kiwanuka,n.k na jinsi Amin alivyojaribu kumuua Makamu Wake (Mustafa Idriss?) na yeye mwenyewe Henry Kyemba.

2.Kama mnadhani Amin alikuwa anasingiziwa kwa kila kitu,inakuwaje mtoto wake Jaffer Amin amekuwa akizitafuta familia za wahanga wa utawala wa baba yake na kuwaomba msamaha kama sehemu ya reconciliation? Reconciliation ya nini kama baba yake hakuua watu?

3.Umewahi kuongea na makamanda wetu wa JWTZ waliomng'oa Amin kuhusu waliyoyashuhudia pale the Nile Mansions (Ikulu ya Amin) na ofisi za SRB ('Wasiojulikana' wa Amin) zilizoko Nakasero baada ya Amin kutoroka?Nadhani akina Muhidin Kimario wangekueleza kitu.Na JWTZ ilikuwa na Waislamu wengi tu ndani yao ambao hawatamsingizia Muislamu mwenzao (Amin).Hawa wanajua jamaa alikuwa wicked! Nimekwambia hivyo maana najua ungeukataa ushuhuda wa Luteni Jenerali Silas Mayunga kwa kudhani Mayunga 'angemsiliba' Amin kwa sababu ya dini yake.Narudia:waulize Waislamu wenzako walioiteka Kampala.

4.Nyinyi mnaohisi alikuwa anasingiziwa,mmeshajiuliza ni kwanini wananchi wa Uganda waliwapa support kubwa wanajeshi wetu kuliko majeshi yao?Ukiona Wananchi wanamfurahia 'mvamizi' dhidi ya kiongozi wao huna la kujiuliza hapo?

5.Cannibalism ni tabia ya baadhi ya wauaji na wachawi.Hawa hula nyama ya mtu (victim wao) kama sehemu ya masharti wanayopewa na waganga wao:kwamba ukila nyama ya victim wako japo kidogo tu mzimu wake hautakusumbua huko mbeleni.Ni sawa na kuua mtu ukalamba damu yake.It's no wonder yule Amin mshirikina alifanya hivyo pia. Hata Jenerali J.B Bokassa wa Jamhuri ya Afrika ya Kati alikuwa akifanya hivyo.Dictators wengi ni cannibals.

Au unataka kukataa kuwa Bokassa naye alikuwa anaonja minofu ya watu?

6.Halafu hadi leo pale Uganda kuna makabila yanakula nyama za watu.Cannibalism is real! Miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia supu za nyama za watu zikiuzwa Uganda.Bodaboda wetu (kutoka Tanzania) wengi tu wenyeji wa Karagwe,Bukoba,Ngara waliokuwa wakivuka border to Uganda wameliwa minofu huko.Leo unaona ajabu kuhusu Iddi Amin kufanya hayo?Anyway,sina uhakika sana kama watu wa Arua (anakotoka Amin) wana mila za cannibalism ila ninachojua hii kitu Uganda ipo kwa baadhi ya jamii hadi leo.
 
luangalila

JF-Expert Member
Jan 12, 2014
4,049
2,000
Moja kati ya Matukio ya kufedhehesha na ambayo hayatasahaulika aliyoyafanya Idd Amin kule Nchini Uganda ni lile tukio la kuwauwa Omba Omba vilema waliokuwa wakiishi mjini kampala baada ya kuwakusanya na kwenda kuwamwaga ndani ya mto Nile.

Sababu kubwa ya Idd Amin kuwamwaga ombaomba hao ndani ya mto Nile ni kutokana mmoja wa vilema hao Ombaomba kufikia hatua ya kumlaumu Idd Amin hadharani walipokutana uso kwa uso mjini Kampala, Idd Amin alilaumiwa juu ya hatua yake ya kuwafukuza wawekezaji nchini humo bila sababu za msingi.

Idd Amin aliulizwa nchi itaendeleaje bila wawekezaji ? Na sisi s itutakufa kwa njaa kwa sababu ajira hazitakuwepo? watu hawatakuwa na pesa hata zakutusaidia sisi ombaomba, alimalizia kwa kumuambia wewe Idd Amini ni zaidi ya kichaa. Baada ya kumwambia Amin maneno yale makali ndipo Maliyamungu aliyekuwa mtu wa karibu sana na Amin alichomoa silaha aina ya Pistol kwa lengo la kumuua lakini Amin alimtuliza asifanye hivyo kisha wakaondoka.

Siku iliyofuata wanajeshi wa Idd Amin walimtafuta na kumkamata yule ombaomba na kuondoka nae na hapo ukawa mwisho wakujua historia ya ombaomba yule, hata hivyo inasadikika aliuwawa. Wiki moja baadae ndipo taarifa zikatolewa kwamba vilema ombaomba waishio mjini Kampala waripoti kwenye vituo vya polisi ili wapatiwe misaada.

Mamia ya ombaomba walikwenda kuripoti vituo vya polisi ili kusubiri misaada ya Amin lakini walipofika huko mambo yalikuwa tofauti na vile walivyoambiwa, kwani walikusanywa kwa pamoja na kupandishwa kwenye magari Aina ya Tipper kisha kupelekwa hadi lilipokuwa Daraja la Karuma Falls ambapo ni umbali wa km 200 kutoka Kampala kwenda Gulu, Daraja hilo la Nkurumah Falls lipo umbali wa takriban mita 100 kutoka kwenye maporomoko hayo.

Hapo Askari waliamriwa kuwamwaga ombaomba hao wasiojiweza ambapo walisafirishwa na maporomoko hayo hadi Mto Nile na huo ukawa mwisho wa historia yao. Idd Amin alisema kwamba aliamua kufanya Vile ili kuondoa kero na usumbufu wa Ombaomba mjini kampala.

Nb: hizi ninazoandika siyo propaganda ni ukweli kabisa wa matukio aliyoyafanya Amin.
View attachment 1952707
Mimi alinishangaza kwa ujasiri wake wakujifanya marshal ambapo aliamua kuwazuia raia wa israel akizania nanyy angepata mgao wa fedha kirahisi rahisi 😃😃😃
 
AbouZakariya

JF-Expert Member
Mar 19, 2013
1,445
2,000
Tuamini ya nani na tuyaache ya nani?

1.Henry Kyemba,aliyewahi kuwa Waziri wa Afya wa Uganda enzi za utawala wa Iddi Amin,anakiri kuonyeshwa na Amin kichwa cha mhanga mmoja wa mauaji kikiwa kwenye fridge.Habari hii ipo kwenye kitabu cha The State Of Blood alichoandika Henry Kyemba as an eye witness.

Henry ameandika mengi ikiwemo mauaji ya Bishop Janan Luwum,Dr.Benedicto Kiwanuka,n.k na jinsi Amin alivyojaribu kumuua Makamu Wake (Mustafa Idriss?) na yeye mwenyewe Henry Kyemba.

2.Kama mnadhani Amin alikuwa anasingiziwa kwa kila kitu,inakuwaje mtoto wake Jaffer Amin amekuwa akizitafuta familia za wahanga wa utawala wa baba yake na kuwaomba msamaha kama sehemu ya reconciliation? Reconciliation ya nini kama baba yake hakuua watu?

3.Umewahi kuongea na makamanda wetu wa JWTZ waliomng'oa Amin kuhusu waliyoyashuhudia pale the Nile Mansions (Ikulu ya Amin) na ofisi za SRB ('Wasiojulikana' wa Amin) zilizoko Nakasero baada ya Amin kutoroka?Nadhani akina Muhidin Kimario wangekueleza kitu.Na JWTZ ilikuwa na Waislamu wengi tu ndani yao ambao hawatamsingizia Muislamu mwenzao (Amin).Hawa wanajua jamaa alikuwa wicked! Nimekwambia hivyo maana najua ungeukataa ushuhuda wa Luteni Jenerali Silas Mayunga kwa kudhani Mayunga 'angemsiliba' Amin kwa sababu ya dini yake.Narudia:waulize Waislamu wenzako walioiteka Kampala.

4.Nyinyi mnaohisi alikuwa anasingiziwa,mmeshajiuliza ni kwanini wananchi wa Uganda waliwapa support kubwa wanajeshi wetu kuliko majeshi yao?Ukiona Wananchi wanamfurahia 'mvamizi' dhidi ya kiongozi wao huna la kujiuliza hapo?

5.Cannibalism ni tabia ya baadhi ya wauaji na wachawi.Hawa hula nyama ya mtu (victim wao) kama sehemu ya masharti wanayopewa na waganga wao:kwamba ukila nyama ya victim wako japo kidogo tu mzimu wake hautakusumbua huko mbeleni.Ni sawa na kuua mtu ukalamba damu yake.It's no wonder yule Amin mshirikina alifanya hivyo pia. Hata Jenerali J.B Bokassa wa Jamhuri ya Afrika ya Kati alikuwa akifanya hivyo.Dictators wengi ni cannibals.

Au unataka kukataa kuwa Bokassa naye alikuwa anaonja minofu ya watu?

6.Halafu hadi leo pale Uganda kuna makabila yanakula nyama za watu.Cannibalism is real! Miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia supu za nyama za watu zikiuzwa Uganda.Bodaboda wetu (kutoka Tanzania) wengi tu wenyeji wa Karagwe,Bukoba,Ngara waliokuwa wakivuka border to Uganda wameliwa minofu huko.Leo unaona ajabu kuhusu Iddi Amin kufanya hayo?Anyway,sina uhakika sana kama watu wa Arua (anakotoka Amin) wana mila za cannibalism ila ninachojua hii kitu Uganda ipo kwa baadhi ya jamii hadi leo.
Sawa mkuu.
 
Joseph lebai

JF-Expert Member
Jul 19, 2017
6,356
2,000
Baada ya Amini kufariki, kesi imefunguliwa huko ahera na wale ombaomba, sijui hukumu itakuwaje! Kuna mafuta yanaendelea kuchemka ili atumbukizwe huko kama malipizi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom