Nadhani ni kashfa na siyo matukio.
Wanajamvi kwanini nchi yetu kila kukicha nchi yetu imekuwa ikiandamwa na matukio ya hapa na pale na huzuka na kupotea ebu tukumbushane baadhi ya matukio
1.richmond
2.dowans
3.babu wa loliondo
4.masaburi na uda yake.
Jamani tujazilize matukio mengine mnayoyajua.nawasilisha.
Kwa sababu hatuna viongozi bali "watawala"
ukweli mtupu.Nchi hii inaongozwa na Farao. Sisi ndio wale wana wa Israel walioteswa na wamisri. Subirini kidogo Neema inakuja, this is just the transitional period. Kunguni wanaendelea kuishambulia Ikulu msijali JK ataachia, na neema tutaanza kuipata hata kabla ya 2015. Neema mara nyingi hutanguliwa na dhiki kubwa na nzito ajabu. Sasa tunayoyaona ni madogo, na viongozi wa serikali ya ccm kwa jinsi walivyofungwa akili hawataweza kuitambua hili. Mbarikiwe na bwana!
Mkuu mbona sijakusoma unauliza uelezwe au?maana heading mkuu na content mbona vimesigana??wewe mleta mada hata kuweka tukio moja!!!anyway mimi nakunbuka vita vya Kagera kati ya TZ na UG!!
Kwenye hii dunia hakuna la ajabu hata moja
Pesa za EPA zilirudishwa bila ya kujulikana aliyezirudisha