mtafuta-maisha
JF-Expert Member
- Nov 5, 2016
- 1,982
- 2,915
Kabla ya yote napenda kuweka wazi kwamba makala hii nimeiandika kutoka vyanzo mbalimbali vya mtandaoni, ikiwemo youtube, bbc documentaries, crime and investigation channel na baadhi ya tovuti mbalimbali, hivyo basi hakuna kilichomo humu ambacho nimekifanyia utafiti binafsi kwakuwa mimi siyo mpelelezi na wala sina njia yoyote ya kuniwezesha kufanya hivyo.
Pia nieleweke kwamba matukio niliyoyaandika hayatokani na filamu za kuigiza bali yanatokanana mahojiano waliofanyiwa wapelelezi waliochunguza mauaji ya marapa ahwa , na watu wa karibu wa wahusika walioishi nao na ambao walikuwa nao maeneo ya matukio kabla ya kuawa kwao na baada ya kushambuliwa.
Makala hii kutokana na sababu kwamba itakuwa ndefu kidogo kuliko makala zangu za awali nitaigawa katika post nne ambazo nitakuwa nikizipost kila baada ya siku kadhaa ila kwa yeyote ambaye angependa kuisoma na kuimaliza mapema anaweza kuipata kwa kuninbox na kuchangia gharama ndogo tu ambayo hata haiwezi kununua soda ya chupa.
Ambao wataweza kusubiri wanaweza kuendela kusubiri hapahapa ambapo nitakuwa nikiupdate post baada ya siku kadhaa mpaka hizo post nne zitakapotimia. Sitoweka ule mfumo wa kubonyeza link ya matangazo maana watu wengi wamekuwa wakilalamika.
Sasa tuendelee…………
Tarehe 9 mwezi wa 3 mwaka 1997 saa 06:45 Usiku
Christopher Wallace a.k.a Biggie Smalls ambaye alikuwa mmoja kati ya marapa maarufu zaidi duniani anashambuliwa kwa kupigwa risasi nne nje ya ukumbi ambapo ilikuwa ikifanyika tafrija huko Los Angels Marekani.
Mpokea simu kitengo cha huduma ya dharura: 911 nini dharura yako.
Mmoja wa watu wapambe wa Biggie: Tunahitaji gari la kubeba wagonjwa hapa kwenye ukumbi wa Rossa Los Angels, kuna mtu kapigwa risasi… tafadhali fanya haraka kuna majeruhi kapigwa risasi.
Hayo ndiyo yalikuwa mazungumzo kati ya mmoja wa wapambe waliokuwa kwenye msafara wa Biggie na mpokea simu kitengo cha dharura.
Kelele zinasikika watu wakiwa wametaharuki huku wengine wakipiga kelele za vilio wakati watu wengine wakipiga kelele za kuomba msaada, huku walinzi wake wakizuia raia kumsogelea eneo alipokuwa Biggie. Ilikuwa ni vurugu na kelele kila mahari watu hawakuweza kusikilizana kabisa kutoka na taharuki iliyotokea hapo.
Mmoja wa wapambe wa Biggie: Mtu kapigwa risasi kwenye gari letu muda huu, tunakaribia kufika hospitali muda huu sijui. (Kwa sauti inayosikika mzungumzaji akiwa kachanganyikiwa)
Mpokea simu wakitengo cha huduma ya dharura: Una maana mwenzako kapigwa risasi kwenye gari lako?
Mmoja wa wapambe wa Biggie: Hapana
Mpokea simu kitengo cha huduma ya dharura: Umesema unaelekea hospitali.
Mmoja wapambe wa Biggie: Ndiyo, nafuatana na gari iliyobeba majeruhi. Lakini mbona hunielewi….
Haya yalikuwa mazungumzo baina ya mhudumu wa kupokea simu za huduma ya dharura na mojawapo wa watu wa msafara wa Biggie aliyekuwa gari lililokuwa likifuata nyuma gari lilikuwa limembeba Biggie wakati akikimbizwa hospitali baada ya shambulio lililotokea.
“Tuko kwenye gari tunamkimbiza hospitali, hatuhitaji kupita Magharibi si ndiyo? Inabidi ugeuze gari Jimmy, umepita barabara ambayo siyo.” Anasikika mojawapo kati ya watu wake Biggie aliyekuwa kwenye gari lililokuwa limembeba likimkimbiza hospitali.
Mara mwingine anadakia. “Una tatizo gani lakini, ona umepita barabara ambayo siyo sahihi.” Anamalizia kwa kutupia tusi.
Mazungumzo na bishano yanaendelea humo kwenye gari huku kila mtu anaonekana kataharuki na kachanganyikiwa, mara dereva akosee barabara mara wabishane njia ya kupita ili mradi vurugu tu humo ndani ya gari wakihangaika kumuwahisha bosi wao hospitali.
Mhudumu wa simu dharura: Ni watu wangapi wameumia.
Mmoja wapambe wa Biggie: Ni mmoja tu ni moja tu aliyeumia…
Mtu mwingine kwenye gari anadakia wakati gari likiingia Hospitali Cedars-Senai Medica Centre.
“Big, unaniskia mwanangu?, Usisimame nenda moja kwa moja mpaka kwenye mlango wa kuingia hospitalini.”
Madaktari waligundua kwamba Biggie alifariki muda mfupi tu baada ya kupigwa risasi. Ndani ya miezi sita tu, dunia ya mziki imepoteza marapa wakubwa wawili kwa kuawa jambo linalowaacha mashabiki wakijiuliza maswali ni nani alimuua Tupac na Biggie.
Hili ni swali ambalo LAPD itamuuliza Greg Kading aliyekuwa mpelelezi toka kitengo cha kuchunguza kesi za mauaji cha Los Angels Police Department (LAPD) na kikosi maalumu cha FBI miaka zaidi ya 10 baadae.
*********************************************..
Chanzo cha ugomvi
Kwenye miaka 1990, Suge Knight akiwa na label yake ya mziki iliyojulikana kama Death Row Records alijikuta katika uhasama mkubwa baina yake na mmiliki wa label ya Bad boys , anayejulikana kama Sean Combs (Puff Daddy kipindi hicho). Ugomvi huu ulizua makundi mawili yaliyojuilikana kama West Coast na East Coast Teams. Pia uhasama baina ya Suge knight na Sean Combs ulikuja kupelekea kuuawa kwa Tupac Shakur na Christopher Wallace, ambao wote wawili walikuwa ni marapa maarufu zaidi duniani kwa wakati huo.
Kuna mtitiriko wa matukio kadhaa ambao umeleta hitimisho kuwa uhasama baina ya label hizi mbili ndiyo ulisababisha mauaji ya marapa hawa.
Tukio la kwanza.
Ilikuwa mwezi wa 11, mwaka 1994 kabla ya Tupac kusaini mkataba na Death Row Records, Tupac alipigwa risasi wakati wa tukio la wizi lilitokea katika studio ya kurekodia mziki huko Newyork. Kwa bahati mbaya Puff Daddy na Biggie walikuwa kwenye jengo hilo hilo wakati tukio hilo linatokea. Hii ilisababisha Tupac kuhisi kuwa rafiki zake wa zamani ndiyo walikuwa wamepanga tukio hilo.
Greg Kading anadai kwamba baadae Tupac alikuja kugundua kuwa Puff na Biggie hata hawakuhusika katika kupanga tukio hilo, ila wakati alipokuja kugundua hilo tayari ugomvi ulikuwa umeshakuwa mkubwa sana baina yao.
Siku moja baada ya Tupac kupigwa risasi katika hilo tukio la wizi kwenye studio za kurekodia mziki huko Newyork, alitakiwa kufika mahakamani alipokuwa ana kesi akituhumiwa kwa unyanyasi wa kingono mwaka mmoja uliopita, ambapo alikuwa anatuhumiwa yeye pamoja na rafiki zake watatu walimbaka binti mwenye umri wa miaka 19 aliyejulikana kama Ayanna Jackson. Kesi ilimalizika wiki kadhaa mbele kwa kukutwa na hatia na alihukumiwa kifungo cha miaka 4 na nusu na hukumu ilimtaka atumikie adhabu hiyo ndipo afikiriwe kupewa msamaha.
Tupac akiwasili mahakamani akiwa kwenye kiti cha kusukumwa
Mwana dada Ayanna Jackson ambaye Tupac, meneja wake pamoja na rafiki zake watatu walikutwa na kosa la kumbaka huku shitaka la kumwingilia nyuma likitupiliwa mbali.
Miezi 9 baadaye ikiwa ni mwezi wa 8 mwaka 1995, Suge Knight anaudhuria utoaji wa tunzo zilizokuwa zikijulikana kama Source awards, Suge akiwa stejini wakati Puff na Biggie wakiwa wamekaa siti za mbele kabisa, inaonekana wazi kuna hali ya kutoelewana baina yao. Hotuba ya Suge aliyoitoa wakati akishukuru kwa tunzo ya wimbo bora uliotumika kwenye filamu(Best Motion Picture SoundTrack), ambapo wimbo kutoka death row ujulikanao kama “Above The Rim” ndiyo ulishinda tunzo hiyo. Katika hotuba hiyo Suge alisema hivi;
“Msanii yoyote huko, anayehitaji kuwa msanii na kuwa maarufu (superstar) bila kuwa na wasiwasi ya Producer kiongozi kutokea kwenye video zake zote, au kwenye nyimbo zote, akicheza. Msanii huyo aje Death row.”
Hayo ndiyo maneno aliyosema Suge alipokuwa jukwaani akiwa na msanii wake Danny Boy huku akiwa na uso mkavu. Maneno haya yalionyesha wazi kuwa ilikuwa ni diss kwa Puff ambaye alikuwa ana tabia yakuonekana kwenye video na kuweka sauti kwenye nyimbo za wasanii wake, na ukumbi mzima ulialipuka kwa kelele za kumzomea Suge.
Kauli hii ilibadirisha kabisa mwelekeo wa mziki wa Hip Hop na kuzidi kuchochea ugomvi baina ya West na East coast.
Wiki kadhaa baadae mwezi wa 9, 1995, Suge Knight na Puff wanajikuta wako katika klabu moja huko Atlanta ambapo ugomvi unaibuka baina ya wapambe wao. Wakati Suge anataka kuondoka, aliyekuwa mlinzi wake na rafiki yake wa karibu aliyekuwa akijulikana Jack Roburous, anapigwa risasi na kufariki. Suge anamlaumu Puff na mlinzi wake aliyekuwa akiitwa Anthony Wolf Jones kuwa ndiyo waliomuua mlinzi wake.
Anthony Wolf Jones aliyekuwa mlinzi wa Puff Daddy.
Suge na Knight (Aliyekaa upande wa kulia) akiwa na mlinzi na rafiki yake wa karibu Jack Joburous (aliyekaa upande wa kushoto)
Wakati huo Tupac yuko gerezani akitumikia adhabu yake ya kifungo kwa miezi kadhaa, akiwa ameshindwa kupata pesa ya kulipia dhamana wakati kesi yake ilipokatiwa rufaa.
Gereza ambalo Tupac alikuwa amefungwa
Cathy Scott, mwandishi wa kitabu kijulikanacho kama Kuawa kwa Tupac Shakur (The Killing of Tupac Shakur), anadai kwamba gereza alilokuwa kafungwa Tupac halikuwa gereza la kawaida kama magereza mengine. Lilikuwa ni gereza ambalo lilikuwa na wafungwa wenye makosa makubwa, ambao walikuwa ni hatari sana na magangwe. Kulikuwa na minong’ono kuwa Tupac akiwa huko gerezani alibakwa jambo ambalo alikuwa akilipinga kwa nguvu zote kuwa siyo kweli. Tupac alikuwa akitaka kutoka huko gerezani na alikuwa akimhimiza mwanasheria wake afanye vyovyote vile ili mradi atoke.
Mwanamama Cathy Scott
Itaendelea Kipande kidogo cha kumalizia sehemu hii ya kwanza……………………
Wale wote waliolalamika kuhusu usumbufu wa link wa makala ya jana nimeipost yote hapo chini kwenye comment #1